APA CHICAGO
JF-Expert Member
- Oct 20, 2019
- 259
- 293
Ni kawaida ya binadamu kusahau huo ndiyo ubinadamu wenyewe lakini kwa bahati mbaya kabisa Watanzania tu wasahaulifu kupita kiasi, au ni siasa tu kwa kila jambo hapo sielewi vizuri.
Kwa maoni yangu Mhe. Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sakata hili la Spika yuko sahihi kwani binadamu tunasirika ya kujisahau sana pindi tinapokuwa na madaraka fulani. Watanzania wenzangu mtaniwia radhi ikiwa nitawakosea au kuwakwaza lakini ukweli nitausema.
Mwenzetu alifikia mahali akajisahau kabisa kuwa yeye ni binadamu kama wengine. Huyu ni kati ya maspika wa hovyo kuwahi kutokea katika nchi yetu maana alitumia vibaya madaraka yake ya uspika angekwa nchi zilizo endelea alipaswa kushitakiwa kwa kosa la matumizi mabaya ya madaraka, sema yuko Africa tena Africa yenyewe Tanzania.
Kwa bahati mbaya amepata watetezi wanaomuonea huruma wamesahau mara hii jeuri yake na kiburi akiwa na madaraka ndani na nje ya bunge huku akitumia vibaya kabisa madaraka yake ya uspika. Siwalaumu sana watetezi wake maana ni haki yao kikatiba lakini wanapaswa kupima mema aliyotenda na mabaya aliyotenda akiwa kama spika kabla ya kumtetea na kumuonea huruma.
Nihitimishe kwa kumpongeza mhe Rais SSH kwa zawadi hii ya mwaka mpya 2022, tumuombee kwa Mungu amzidishie hekima na busara za kuliongoza taifa letu.