Tumpongeze Rais Samia kwa hili la Ndugai, Spika aliyejiuzulu

APA CHICAGO

JF-Expert Member
Oct 20, 2019
259
293
Ni kawaida ya binadamu kusahau huo ndiyo ubinadamu wenyewe lakini kwa bahati mbaya kabisa Watanzania tu wasahaulifu kupita kiasi, au ni siasa tu kwa kila jambo hapo sielewi vizuri.

Kwa maoni yangu Mhe. Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sakata hili la Spika yuko sahihi kwani binadamu tunasirika ya kujisahau sana pindi tinapokuwa na madaraka fulani. Watanzania wenzangu mtaniwia radhi ikiwa nitawakosea au kuwakwaza lakini ukweli nitausema.

Mwenzetu alifikia mahali akajisahau kabisa kuwa yeye ni binadamu kama wengine. Huyu ni kati ya maspika wa hovyo kuwahi kutokea katika nchi yetu maana alitumia vibaya madaraka yake ya uspika angekwa nchi zilizo endelea alipaswa kushitakiwa kwa kosa la matumizi mabaya ya madaraka, sema yuko Africa tena Africa yenyewe Tanzania.

Kwa bahati mbaya amepata watetezi wanaomuonea huruma wamesahau mara hii jeuri yake na kiburi akiwa na madaraka ndani na nje ya bunge huku akitumia vibaya kabisa madaraka yake ya uspika. Siwalaumu sana watetezi wake maana ni haki yao kikatiba lakini wanapaswa kupima mema aliyotenda na mabaya aliyotenda akiwa kama spika kabla ya kumtetea na kumuonea huruma.

Nihitimishe kwa kumpongeza mhe Rais SSH kwa zawadi hii ya mwaka mpya 2022, tumuombee kwa Mungu amzidishie hekima na busara za kuliongoza taifa letu.
 
Tuna kipi cha kushangilia mkuu wa mhimili mmoja kufurushwa kinyume cha katiba?
Yeye alitenda kipi cha kumuonea huruma? Prof. Assad alitumia Uhuru wake wa kutoa maoni yeye akamuita kumhoji akitumia madaraka yake ya uspika.
 
Yeye alitenda kipi cha kumuonea huruma? Prof. Assad alitumia Uhuru wake wa kutoa maoni yeye akamuita kumhoji akitumia madaraka yake ya uspika.

Tena alimwambia asipokuja mwenyewe .... ataletwa kwa pingu kitu kama hicho
 
Ni kawaida ya binadamu kusahau huo ndiyo ubinadamu wenyewe lakini kwa bahati mbaya kabisa watanzania tu wasahaulifu kupita kiasi, au ni siasa tu kwa kila jambo hapo sielewi vizuri.Kwa maoni yangu mhe,Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sakata hili la Spika yuko sahihi kwani binadamu tunasirika ya kujisahau sana pindi tinapokuwa na madaraka fulani.Watanzania wenzangu mtaniwia radhi ikiwa nitawakosea au kuwakwaza lakini ukweli nitausema.Mwenzetu alifikia mahali akajisahau kabisa kuwa yeye ni binadamu kama wengine.Huyu ni kati ya maspika wa hovyo kuwahi kutokea katika nchi yetu maana alitumia vibaya madaraka yake ya uspika angekwa nchi zilizo endelea alipaswa kushitakiwa kwa kosa la matumizi mabaya ya madaraka, sema yuko Africa tena Africa yenyewe Tanzania.Kwa bahati mbaya amepata watetezi wanaomuonea huruma wamesahau mara hii jeuri yake na kiburi akiwa na madaraka ndani na nje ya bunge huku akitumia vibaya kabisa madaraka yake ya uspika.Siwalaumu sana watetezi wake maana ni haki yao kikatiba lakini wanapaswa kupima mema aliyotenda na mabaya aliyotenda akiwa kama spika kabla ya kumtetea na kumuonea huruma. Ni hitimishe kwa kumpongeza mhe Rais SSH kwa zawadi hii ya mwaka mpya 2022,tumuombee kwa Mungu amzidishie hekima na busara za kuliongoza taifa.
Ninapata kujifunza mengi kupitia mitandao ya kijamii lakini kubwa zaidi ninajifunza ni jinsi gani? Wengi wetu sisi watanzania tusivyotunza kumbukumbu au tunavutwa kushabikia jambo Fulani kwa sababu ya masrahi binafisi?.Haiwezekani mtu aliyemdhalilisha Prof.Assad aliyetoa maoni yake kuhusu bunge letu aliitwa kuhojiwa.Spika aliyejihudhuru alisababisha Prof Assad kuondolewa ofsini kwa sababu ya kutoa maoni yake.Leo hii spika huyo huyo katoa maoni yake ameshughulikiwa kuna watu wanasema ameadhibiwa kwa kutoa maoni yake. Je?Watanzania hatujui tunahitaji kitu gani? Mama endelea kuchapa kazi.
 
Ni kawaida ya binadamu kusahau huo ndiyo ubinadamu wenyewe lakini kwa bahati mbaya kabisa watanzania tu wasahaulifu kupita kiasi, au ni siasa tu kwa kila jambo hapo sielewi vizuri.Kwa maoni yangu mhe,Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sakata hili la Spika yuko sahihi kwani binadamu tunasirika ya kujisahau sana pindi tinapokuwa na madaraka fulani.Watanzania wenzangu mtaniwia radhi ikiwa nitawakosea au kuwakwaza lakini ukweli nitausema.Mwenzetu alifikia mahali akajisahau kabisa kuwa yeye ni binadamu kama wengine.Huyu ni kati ya maspika wa hovyo kuwahi kutokea katika nchi yetu maana alitumia vibaya madaraka yake ya uspika angekwa nchi zilizo endelea alipaswa kushitakiwa kwa kosa la matumizi mabaya ya madaraka, sema yuko Africa tena Africa yenyewe Tanzania.Kwa bahati mbaya amepata watetezi wanaomuonea huruma wamesahau mara hii jeuri yake na kiburi akiwa na madaraka ndani na nje ya bunge huku akitumia vibaya kabisa madaraka yake ya uspika.Siwalaumu sana watetezi wake maana ni haki yao kikatiba lakini wanapaswa kupima mema aliyotenda na mabaya aliyotenda akiwa kama spika kabla ya kumtetea na kumuonea huruma. Ni hitimishe kwa kumpongeza mhe Rais SSH kwa zawadi hii ya mwaka mpya 2022,tumuombee kwa Mungu amzidishie hekima na busara za kuliongoza taifa letu.
Umeongea hisia zaidi kuliko uhalisia. Au pengine hujui kitu ,Rais hapaswi kuingilia mhimili mwingine bunhe ni mhimili mwingine sawa na mahakama so kisheria rais kakosea sana
 
Umeongea hisia zaidi kuliko uhalisia. Au pengine hujui kitu ,Rais hapaswi kuingilia mhimili mwingine bunhe ni mhimili mwingine sawa na mahakama so kisheria rais kakosea sana
Ila mhimili mwingine una haki ya kufanya kama unavyotaka bila kuhojiwa ?
 
naunga mkono hoja
P
Paschal kwa hili Mhe Rais wetu kaupiga mwingi na nasema Mhe,Rais Kazi iendelee ili watu watambue madaraka huwa Ni ya muda tu.Huyu spika amefanya maamuzi ya hovyo sana mengi yanayoligharimu taifa mamilioni ya shilingi huku watoto wetu hawana madawati mashuleni.
 
Yeye alitenda kipi cha kumuonea huruma? Prof. Assad alitumia Uhuru wake wa kutoa maoni yeye akamuita kumhoji akitumia madaraka yake ya uspika.

Makosa 2 hayafanyi 1 kuwa sahihi.

Ndugai angefurushwa kwa mujibu wa sheria kwa makosa yake (ikiwamo hata kumkejeli Assad) ilikuwa halalii.

Mama Samia kumfurusha Ndugai kinyume cha sheria kwa kutoa maoni yake tu, hiyo siyo ndugu chawa!
 
Umenikumbusha mbali mkuu Black sniper halfu kuna watu wamesahau yote haya ama kweli sisi watanzania tunasahau sana

..Ndugai alipaswa kufukuzwa au kulazimishwa kujiuzulu kwa kutumia madaraka yake ya Uspika vibaya.

..Kuwa na maoni au msimamo tofauti na serikali kuhusu mikopo sio kosa la kumfukuzisha kazi Spika wa bunge.

..Mama amemshambulia Spika kwa kusikiliza clip ambayo imekatwa. Angesikiliza clip nzima / original asingepandwa na hasira namna ile.
 
Makosa 2 hayafanyi 1 kuwa sahihi.

Ndugai angefurushwa kwa mujibu wa sheria kwa makosa yake (ikiwamo hata kumkejeli Assad) ilikuwa halalii.

Mama Samia kumwitisha Ndugai kinyume cha sheria kwa kupoa maoni yake hiyo siyo ndugu chawa!
Ndugu yangu vyovyote utakavyoamua kuniita ama kunguni au kupe ila mimi kwa jinsi alivyotumia madaraka yake vibaya na kukejeli watu wengine "The end justify the means".
 
Ni kawaida ya binadamu kusahau huo ndiyo ubinadamu wenyewe lakini kwa bahati mbaya kabisa Watanzania tu wasahaulifu kupita kiasi, au ni siasa tu kwa kila jambo hapo sielewi vizuri.

Kwa maoni yangu Mhe. Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sakata hili la Spika yuko sahihi kwani binadamu tunasirika ya kujisahau sana pindi tinapokuwa na madaraka fulani. Watanzania wenzangu mtaniwia radhi ikiwa nitawakosea au kuwakwaza lakini ukweli nitausema.

Mwenzetu alifikia mahali akajisahau kabisa kuwa yeye ni binadamu kama wengine. Huyu ni kati ya maspika wa hovyo kuwahi kutokea katika nchi yetu maana alitumia vibaya madaraka yake ya uspika angekwa nchi zilizo endelea alipaswa kushitakiwa kwa kosa la matumizi mabaya ya madaraka, sema yuko Africa tena Africa yenyewe Tanzania.

Kwa bahati mbaya amepata watetezi wanaomuonea huruma wamesahau mara hii jeuri yake na kiburi akiwa na madaraka ndani na nje ya bunge huku akitumia vibaya kabisa madaraka yake ya uspika. Siwalaumu sana watetezi wake maana ni haki yao kikatiba lakini wanapaswa kupima mema aliyotenda na mabaya aliyotenda akiwa kama spika kabla ya kumtetea na kumuonea huruma.

Nihitimishe kwa kumpongeza mhe Rais SSH kwa zawadi hii ya mwaka mpya 2022, tumuombee kwa Mungu amzidishie hekima na busara za kuliongoza taifa letu.
Utopolo!
 
Ndugu yangu vyovyote utakavyoamua kuniita ama kunguni au kupe ila mimi kwa jinsi alivyotumia madaraka yake vibaya na kukejeli watu wengine "The end justify the means".

Mtu wa namna gani wewe usiyeweza kuona tofauti ya kosa na haki za awaye yote?

Kumbe Ndugai angeweza kufurushwa hata kwa sababu ya kwenda kujisaidia chooni tu ila kwa sababu alikuwa na makosa mengine basi ndiyo kimeumana?

Uitwe jina gani wewe lenye kukupa utambulisho kamili?

Nchi huongozwa kwa mujibu wa sheria.

Siyo kwa mihemko, kununa, chuki, visasi, hasira wala vya namna hiyo.
 
Back
Top Bottom