Wakati wa utawala wa awamu ya Kwanza tuliambiwa ili Tanzania iendelee inahitaji watu(think tanks), Ardhi(maliasili), Siasa safi(sera na mikakati) na Uongozi bora(visionaire). Miaka 50 imepita lakini bado tuko hatua moja tu mbele ilihali tulipaswa tuwe tumeshafika mbali kama nchi. Wasomi wa kutosha wapo, Maliasili tunazo kuliko nchi nyingi tu hapa duniani, Sera na mikakati mingi tu ipo na viongozi ndio hao kila baada ya miaka 5 tunafanya uchaguzi mkuu na tunapata viongozi.
Kumekuwa na hoja kwamba tatizo letu ni kukosa viongozi wazalendo wenye muono wa mbali, hilo nakubaliana nalo kwa kiasi lakini mbona tulikuwa na akina Nyerere(great son of Africa) na bado hatukusonga. Wengine husema sera za kijamaa na kujitegemea zimetugharimu sana kwa miaka mingi lakini bado sio suala kwani baada ya kuukumbatia ubepari ndio kwanza tunapigwa bao katika nyanja ya uchumi. Sasa nimekuwa najiuliza tatizo ni nini?
Mimi nadhani watanzania tuna tatizo la utamaduni (cultural issue). Hatufunguki(openness), tuna unafiki mwingi na ni waoga. Tangia mtoto anazaliwa hadi anakua anakutana na jamii iliyojikita katika hayo niliyoyataja hapo juu. Nae anakuwa hivyo hivyo sababu akijitahidi kujipambanua ataambiwa jamii yetu haiko hivyo wewe mtoto wa wapi. Watanzania utawakuta wanatabasamu ilihali moyoni kua machungu. Mtu hataki kitu lakini anasema sawa!! KWa vile suala hili limejikita mno ndani ya jamii linaathiri uwezo wa kufanya maamuzi kwa mtu binafsi na jamii kwa ujumla. Viongozi wanakuwa hivyo hivyo na hatimae mambo hayaendi kama yanavyopaswa. Mwishowa yote mfumo mzima katika jamii unagubikwanawingu zito ambalo kuliondoa ni tabu!!
Ili tuweze kuendelea tunahitaji kukabiliana na utamaduni mbovu kwanza. Tutafanyaje? - anza kumfundisha mwanao kuwa honest, transparent, No to means a no and Yes to means a Yes, boldness, fighting for ones right is not sin, justice etc
Nawasilisha!!