Tumlaumu nani? Watu, ardhi, siasa safi au uongozi bora?

shilanona

Member
Oct 31, 2010
55
95
12_10_2m1b95.jpg

Wakati wa utawala wa awamu ya Kwanza tuliambiwa ili Tanzania iendelee inahitaji watu(think tanks), Ardhi(maliasili), Siasa safi(sera na mikakati) na Uongozi bora(visionaire). Miaka 50 imepita lakini bado tuko hatua moja tu mbele ilihali tulipaswa tuwe tumeshafika mbali kama nchi. Wasomi wa kutosha wapo, Maliasili tunazo kuliko nchi nyingi tu hapa duniani, Sera na mikakati mingi tu ipo na viongozi ndio hao kila baada ya miaka 5 tunafanya uchaguzi mkuu na tunapata viongozi.

Kumekuwa na hoja kwamba tatizo letu ni kukosa viongozi wazalendo wenye muono wa mbali, hilo nakubaliana nalo kwa kiasi lakini mbona tulikuwa na akina Nyerere(great son of Africa) na bado hatukusonga. Wengine husema sera za kijamaa na kujitegemea zimetugharimu sana kwa miaka mingi lakini bado sio suala kwani baada ya kuukumbatia ubepari ndio kwanza tunapigwa bao katika nyanja ya uchumi. Sasa nimekuwa najiuliza tatizo ni nini?

Mimi nadhani watanzania tuna tatizo la utamaduni (cultural issue). Hatufunguki(openness), tuna unafiki mwingi na ni waoga. Tangia mtoto anazaliwa hadi anakua anakutana na jamii iliyojikita katika hayo niliyoyataja hapo juu. Nae anakuwa hivyo hivyo sababu akijitahidi kujipambanua ataambiwa jamii yetu haiko hivyo wewe mtoto wa wapi. Watanzania utawakuta wanatabasamu ilihali moyoni kua machungu. Mtu hataki kitu lakini anasema sawa!! KWa vile suala hili limejikita mno ndani ya jamii linaathiri uwezo wa kufanya maamuzi kwa mtu binafsi na jamii kwa ujumla. Viongozi wanakuwa hivyo hivyo na hatimae mambo hayaendi kama yanavyopaswa. Mwishowa yote mfumo mzima katika jamii unagubikwanawingu zito ambalo kuliondoa ni tabu!!

Ili tuweze kuendelea tunahitaji kukabiliana na utamaduni mbovu kwanza. Tutafanyaje? - anza kumfundisha mwanao kuwa honest, transparent, No to means a no and Yes to means a Yes, boldness, fighting for ones right is not sin, justice etc

Nawasilisha!!
 
Buyengwa

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
14,083
2,000
Wote. Watu kwa kuchagua CCM,na kusubiri kila jambo wafanyiwe na serikali,yani hata kuzibua mitaro ilio mbele za nyumba zao. Siasa chafu kwa kuchakachukua mfumo mzima wa uchaguzi. Uongozi mbovu kwa kukosa vipaumbele na kukaidi mipango miji,na kupokea rushwa kwa kugawa maeneo ambayo ni sehemu ya mkondo wa maji na yenye mitaro mikubwa iendayo bahirini.
 
MANI

Platinum Member
Feb 22, 2010
7,298
2,000
Leo yamebaki masaa kama 48 tu ili ile siku ya uchaguzi Arumeru ifanyike. Kama ambavyo kichwa cha maneno kinavyosema hapo juu ambayo ni moja ya nukuu za Mwalimu JK wakati wa uongozi wake alikuwa akiisema mara kwa mara. Kati ya vyote hivyo tumejaliwa kupata ardhi kubwa yenye kila rasilimali pamoja na rutuba,hali kadhalika watu pia tunao na wakutosha.

Lakini kwa kipindi kirefu sasa tumepungukiwa na vitu viwili vya mwisho,yaani siasa safi na uongozi bora. Na vitu hivi ni lazima vishahadiane kwani huwezi kupata siasa safi bila kiongozi bora. Kwa karibu miongo mitatu sasa tumejaliwa kupata bora viongozi ndio maana tuko hapa tulipo. Matatizo yetu mengi kwa asilimia kubwa yanachangiwa na ukosefu wa uongozi bora utakaotuletea siasa safi na kupata maendeleo.

Ni tegemeo langu kuwa kwa kadiri kampeni zilivyoendeshwa nyinyi wakazi Arumeru ni jukumu lenu sasa kutufungulia njia ya kupata viongozi bora watakaotuletea siasa safi na maendeleo. Hima wananchi wote kipindi cha kubadilika ni hiki onyesheni njia kwa ajili ya ukombozi wa nchi yetu.

Mungu awajalie hekima ya kutubadilshia maisha kwa kupitia sanduku la kura.
 
SASATELE

Senior Member
Sep 12, 2011
168
0
Wakati wa utawala wa awamu ya Kwanza tuliambiwa ili Tanzania iendelee inahitaji watu(think tanks), Ardhi(maliasili), Siasa safi(sera na mikakati) na Uongozi bora(visionaire). Miaka 50 imepita lakini bado tuko hatua moja tu mbele ilihali tulipaswa tuwe tumeshafika mbali kama nchi. Wasomi wa kutosha wapo, Maliasili tunazo kuliko nchi nyingi tu hapa duniani, Sera na mikakati mingi tu ipo na viongozi ndio hao kila baada ya miaka 5 tunafanya uchaguzi mkuu na tunapata viongozi.

Kumekuwa na hoja kwamba tatizo letu ni kukosa viongozi wazalendo wenye muono wa mbali, hilo nakubaliana nalo kwa kiasi lakini mbona tulikuwa na akina Nyerere(great son of Africa) na bado hatukusonga. Wengine husema sera za kijamaa na kujitegemea zimetugharimu sana kwa miaka mingi lakini bado sio suala kwani baada ya kuukumbatia ubepari ndio kwanza tunapigwa bao katika nyanja ya uchumi. Sasa nimekuwa najiuliza tatizo ni nini?

Mimi nadhani watanzania tuna tatizo la utamaduni (cultural issue). Hatufunguki(openness), tuna unafiki mwingi na ni waoga. Tangia mtoto anazaliwa hadi anakua anakutana na jamii iliyojikita katika hayo niliyoyataja hapo juu. Nae anakuwa hivyo hivyo sababu akijitahidi kujipambanua ataambiwa jamii yetu haiko hivyo wewe mtoto wa wapi. Watanzania utawakuta wanatabasamu ilihali moyoni kua machungu. Mtu hataki kitu lakini anasema sawa!! KWa vile suala hili limejikita mno ndani ya jamii linaathiri uwezo wa kufanya maamuzi kwa mtu binafsi na jamii kwa ujumla. Viongozi wanakuwa hivyo hivyo na hatimae mambo hayaendi kama yanavyopaswa. Mwishowa yote mfumo mzima katika jamii unagubikwanawingu zito ambalo kuliondoa ni tabu!!

Ili tuweze kuendelea tunahitaji kukabiliana na utamaduni mbovu kwanza. Tutafanyaje? - anza kumfundisha mwanao kuwa honest, transparent, No to means a no and Yes to means a Yes, boldness, fighting for ones right is not sin, justice etc

Nawasilisha!!
 
POMPO

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
6,690
1,195
Tanzania ina watu wa kutosha, Ardhi ya kutosha tunakusa hivyo vitu viwilil...
Tunachokikosa ni UONGOZI Bora. tuna Bora Viongozi na watawala...
 
Biznocrats

JF-Expert Member
Apr 5, 2011
452
170

Dira hiyo ndio chanzo cha sisi kama Taifa kushindwa kupiga hatua ya maendeleo kwa kipindi chote cha zaidi ya miaka 50 tangu tupate uhuru. Hii inathibitisha kwamba CCM hawana vision since day one ya kulitoa taifa letu kwenye umasikini. Unawezaje kupanga mikakati ya maendeleo ya Taifa lako bila kuweka elimu mbele? Watu tayari wapo na ardhi ipo tangu tupate uhuru. Kilichokosekana ni elimu ya kuwawezesha watanzania kutawala mazingira yao. Porojo za siasa safi na uongozi bora sio key issue kwenye maendeleo ya taifa lolote lile duniani. Main issue ni elimu ambayo kwenye dira hiyo ya CCM haipo.

Juu ya kwamba Watanzania wazawa tulikuwa tunachukuliwa kama watu wa daraja la tatu kwenye nchi yetu wakati wa ukoloni, lakini bado elimu ya wakati huo iliyotolewa kwa watanzania ilikuwa bora mno ukilinganisha na elimu ya sasa hivi. Mtu alikuwa akimaliza darasa la nne basi anakuwa na uwezo mkubwa wa kutawala mazingira yake katika nyanja mbalimbali za maisha wakati huo. Sasa hivi vijana wetu wanamaliza mpaka Form Six kama sio chuo kikuu lakini hawana uwezo wa kifalsafa wa kutawala mazingira yao!!!!

Kwa sababu dira yao haina kipengele cha elimu, mara baada ya kupata uhuru wakaanza kuingiza siasa ndani ya elimu. Wakabadilisha mitaala ya kufundishia kutoka kiingereza kwenda kiswahili wakati hakukuwa na miundo mbinu iliyotayarishwa kwa ajili ya kufundishia kwa lugha hiyo. Kwa mfano waalimu wa wakati huo walisomea kwenye mazingira ya kiingereza hivyo hawakuwa na uwezo wa kufundishia kwa kutumia kiswahili; Lugha ya kiswahili haikuwa na maneno ya kutosha ya kumwelezea mtu falsafa ikaeleweka; vitabu vya kufundishia kwa kiswahili vilikuwa havipo vya kutosha. Tukaanza kuzalisha watanzania walioingia madarasani lakini wajinga. Matatizo haya yanaendelea mpaka hii leo!!!

Kuendelea kuruhusu CCM waendelee kuwepo madarakani ili waendelee kutekeleza dira zao za giza ni janga la kitaifa. It is shame on us Watanzania kuruhusu hilo liendelee. PIGA UA, 2015 CCM wafunge virago na wapinzani waingie madarakani ili Taifa letu liondokane na hii aibu ya kuwa taifa ombaomba milele chini ya usimamizi wa CCM. Kwa kweli wametudhalilisha kiasi cha kutosha kwani viongozi wetu wakuu wanazunguruka dunia nzima kutembeza bakuli la kutuombea kwa niaba yetu wakati Tanzania sio nchi ya kuombaomba kiasi hicho kutokana na utajiri tulionao. Cha ajabu ni kwamba wakinyimwa misaada kwa sababu yeyote ile basi wanaanza kulialia ("kwa niaba yetu"!!!!) na kuwaambia wafadhili kwamba ni wajibu wao kutusaidia, ni wajibu wao kutimiza ahadi za misaada waliotupa kwani ahadi ni deni!!!!! Miaka zaidi ya 50 kama Taifa bado unaona una haki ya kusaidiwa wakati taifa haliko vitani au kupata janga kubwa lolote bila haya!!!!

Ndugu zangu Watanzania. CCM ni mzigo ambao hatustahili kuendelea kuubeba tena na tuwe tayari kuinasua nchi yetu kutoka kwa wasanii hawa wa kisiasa kwa gharama yeyote ile.
 
emalau

JF-Expert Member
Apr 25, 2009
2,743
2,000
Tanzania ina watu wa kutosha, Ardhi ya kutosha tunakusa hivyo vitu viwilil...
Tunachokikosa ni UONGOZI Bora. tuna Bora Viongozi na watawala...

Hapo kwenye red, unaweza ukawa na watu wengi lakini hawana ujuzi wowote, kwa mfano tulifanya semina siku moja Arusha mheshimiwa Zitto Kabwe alisema mpaka sasa hivi nchi haina mtaalamu hata mmoja anayeweza kufanya welding ndani ya bahari, matokeo yake wanaofanya exploration ya mafuta wanalazimika kuchukua watu toka nje ya nchi. Kwa hiyo tunabaki kama watazamaji kwenye suara la mafuta kwa kuwa hakuna value chain, tunabaki kuangalia pato la kodi tu.

Ukichukua hotuba ya Kaburu P.W. Botha ya mwaka 1985 ndani ya bunge la Africa kusini alisema mtu mweusi hana uwezo wa kuona mbali, mawazo yake ni kwenye ngoma, wake wengi, ngono na hafikirii juu ya kesho. Maneno haya watu waliyachukulia ni ya kibaguzi lakini ukweli anglau kidogo upo vision inakosekana katika viongozi wengi wa kiafrika.

Hapo ulipo umekaa jiangalie vitu vilivyokuzunguka, hiyo computer unayotumia inatoka America au Japan - Hp,Toshiba etc, printer the same n.k. Hii ina maana gani? kwamba sisi tunategemea technology ya nje kwa kiwango kikubwa. Kwa mtaji huu as long as Afrika haiwekezi kwenye technology itabaki nyuma mpaka yesu arudi kama tunavyoamini sisi wakristu.
 
kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,171
2,000
Mmenena wakuu, mliyoyataja yote ni sawa kabisa. Lakini tunatakiwa kubadili kifikira na kiutendaji.
 
Kakende

JF-Expert Member
Aug 18, 2012
2,741
2,000
Ili Tanzania iendelee inahitaji elimu bora. Hakuna njia yoyote ya kutuendeleza kama hatuwekezi kwenye elimu. Offcourse desturi inatugharimu lakini tukiwa na elimu yote yatakwisha.

Asilimia 80 ya wapiga kura Tz wameishia darasa la saba au hawajasoma kabisa ndiyo maana utaona watu kama akina Chenge, Lowassa na watuhumiwa wengine bado wanapata ushindi mkubwa kwenye majimbo yao ya uchaguzi kwa sababu wapiga kura ni mbumbumbu. Wakati kwa nchi zilizoendelea kiongozi anapigwa nje na wapiga kura kwa kosa dogo kwenye debate.

Kwa kukosa elimu WaTZ wanadanganywa kidogo tu kwamba chama fulani ni cha dini fulani nao wanaamini na kuendelea kuneemesha mafisadi wa CCM
 
Njaare

JF-Expert Member
Sep 26, 2010
1,081
1,500
Tanzania ina watu wa kutosha, Ardhi ya kutosha tunakusa hivyo vitu viwilil...
Tunachokikosa ni UONGOZI Bora. tuna Bora Viongozi na watawala...

Tatizo ni watu kwa maana kuwa ni watu wa aina gani, uwezo wao wa kuchanganua mambo ukoje? Kama una watu wanaoishi kwa shida miaka minne na miezi minane halafu ndani ya miezi minne wanapewa pilau na tishet za kijani wanamrudisha tena kiongozi yule yule mtaendeleaje?
 
Ronal Reagan

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
4,890
2,000
Ili tuweze kuendelea tunahitaji kukabiliana na utamaduni mbovu kwanza. Tutafanyaje? - anza kumfundisha mwanao kuwa honest, transparent, No to means a no and Yes to means a Yes, boldness, fighting for ones right is not sin, justice etc

i.e. ELIMU BORA.
 
Ronal Reagan

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
4,890
2,000
Ndani ya Elimu Bora kuna maadili mema, maarifa, utu, weledi nk

Ili tufike pale tunakotaka (hasa kijamii na kiuchumi) basi ni budi tuwe na kipindi cha mpito kisiasa, kijamii na kiuchumi. Tusishawishike kupita njia ya mkato. Mwalimu Nyerere alijaribu kuweka misingi (kwamba alifaulu au la hilo ni jambo jingine) ili wengine wajenge Taifa kuelekea kuwashinda maadui watatu lakini pia kwa kufanya hivyo kuleta maendeleo na ustawi kwa raia mmoja mmoja na nchi kwa ujumla.

Tumepotea kama Taifa zaidi ya miaka 25 sasa. Tuendako hatupajui. Leo maendeleo yanapimwa kwa vitu, ilihali watu wamezidi kudidimia. MKUKUTA ni aibu inayosubiri muda tu itimie.

Nchi hii kisera na kimkakati ni aibu, kisiasa ndio usiseme. We simply need a proper overhauling and NOW.
 
Buyengwa

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
14,083
2,000
Sijui...ila wanasemaga necessity is the mother of invention.

Kabisa.
Lakini, kwani Tanzania hatuna mahitaji ya kutufanya tuwe wabunifu na wavumbuzi?
Hapa tunapokuwa na mahitaji 'yanayoonekana' kuzidi 'uwezo' wetu, suluhisho ni kutembeza bakuli au kuhemea njaa kama anavyosema kiranja mkuu.

Chifu, yaani sisi tunafaida ya kurahisishiwa mambo na vitu na mataifa yaliyoendelea; kitu tunachokihitaji ni kuhamisha huo uvumbuzi na ubunifu ambao tayari umeshafanywa na wavumbuzi na wabunifu kutoka mataifa ya Ulaya na Marekani, na kuuweka uvumbuzi na ubunifu huo katika mazingira ya Tanzania (transfer of technology).
Ni ajabu hadi leo CoET (College of Engineering and Technology, UDSM) wanatengeneza manual mashines za vitu mbalimbali. Siku moja nilikuwa naangilia kipindi cha mambo ya teknoloji, basi kuna profesa mmoja wa CoET, anajitapa amegundua mashine (nimesahau ilikuwa ya kitu gani), ila kilichonisikitisha ni aina ya mashine yenyewe, jinsi ilivyo ya kizamani kwa muunekano na hata kwa materials zilizotumika kuitengeneza. Mashine kama ile imetumika Ulaya karne za 16 hadi 18; lakini leo karne ya 21, profesa mzima anajitapa nayo.
Yaani, CoET wanashindwa kuhamisha uvumbuzi na ubunifu unaofanywa na watu kule Ujerumani, Marekani, Uingereza, Japan n.k. na kuuleta Tanzania, kisha kuuretrofit ili uweze kuendana na mazingira ya Tanzania?

Lakini, tukienda katika upande mwingine, unakuta serikali haitoi kipaumbele katika R&D (research and development); bajeti ya R&D Tanzania ni kichekesho. Ingawa kiukweli, wakati mwingine juhudi za taasisi husika katika kufanya tafiti na kutafuta mashirikiano uwa zinahitajika, nguvu za serikali katika masuala ya uvumbuzi na ubunifu ni za lazima.

Sasa nikienda kwa mtazamo huo, nasema kwa uhakika kabisa kwamba, kwa sasa Tanzania tunahitaji UONGOZI BORA ili tuendelee.
 
Buyengwa

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
14,083
2,000
Viongozi wetu wanaakisi wananchi hao hao wanaowaweka madarakani!

Hakika. Hakuna uongozi, kama hamna watu wa kuongozwa!
Kwani ninavyosema uongozi bora, namaanisha pia namna ambayo watu wanapata kuwa viongozi: wanachaguliwaje? Watu wanaowachagua, wanawachagua wakiwa katika hali gani ya uelewa? Ni msukumo upi umewafanya wachaguliwe na watu hao?

Hivyo basi ninavyosema tatizo letu ni ukosefu wa uongozi bora, ninapenda nieleweke kwamba namna viongozi wetu wanavyochaguliwa bado si bora pia.

Tukishakuwa na misingi bora ya kuchagua viongozi, hakika taifa litapata uongozi bora.

Wasalaam.
 
Nenda Kaskazini nenda Kusini. Nenda Magharibi rudi Masharik. Utagundua kwamba kama tunataka kuset priority katika ufumbuzi wa matatizo yetu, basi kitu pekee ni ELIMU. Watu wakiwa na elimu watachagua viongozi bora na huwezi kumpata kiongozi bora kama watu hawana elimu. Ndio maana nasema hakuna taifa lililoendelea kwa ajili ya uongozi bora. ELIMU ndio trigger ya vyanzo vyote vya maendeleo kwenye taifa husika.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom