Ili tuendelee tunahitaji watu ardhi siasa safi na uongozi bora Tanzania tunakisa siasa safi na uongozi bora

MKWEAMINAZI

JF-Expert Member
May 28, 2023
930
1,299
Maneno hayo SIO yangu ni ya Mpendwa Wetu HAYATI BABA wa TAIFA Mwl.NYERERE.

BABA wa TAIFA aliamini Uwepo wa hivyo VITU 4 Nchi lazima Ipate MAENDELEO.

Kwa TANZANIA tuna ARDHI ya kutosha yenye Mito na Mabonde yanayofaa kwa KILIMO
Tuna idadi KUBWA ya WATU kwa Mujibu wa SENSA Tanzania ina Watu MIL.60


Kuhusu SIASA hapo pana TATIZO KUBWA kwani kuna CHAMA kinatumia KATIBA yake kuongoza NCHI

Chama hicho kinateua Viongozi wote ambao ni Wanachama wake hata kwenye Maeneo ya UCHAGUZI jambo ambalo sio HAKI kwa Mfumo wa Vyama vingi.

Vile vile Msajili wa Vyama ni Kada wa Chama Tawala na anateuliwa na Mwenyekiti wa Chama Tawala ambaye hata Chama Tawala kikifanya Makosa HAWEZI kukichukulia Hatua za Kisheria kama Vyama vingine.
Kuhusu UONGOZI BORA hapo napo pana MATATIZO MAKUBWA

Viongozi wote wanapatikana kwa Teuzi na hakuna USHINDANI wa SIFA Unafanyika Matokeo yake ni kuwa na VIONGOZI wabovu ambao Utendaji kazi wao unalindwa na Uanachama wao hata Akiiba Chama kitamtetea
Na pia baadhi ya Viongozi wanatumia Madaraka Yao kuvionea Vyama vya Upinzani ktk CHAGUZI .
Ushauri
1 Tuwe na Tume huru ya Uchaguzi itakayojumuisha VYAMA VYOTE
2 WATENDAJI wa TUME wapatikane kwa kuomba hizo NAFASI na Kuvishirikisha Vyama vyote na Wathibitishwe na Bunge.
3.Watendaji wote ambao ni WATALAAMU Nafasi zo ZITANGAZWE ili waombaji wenye SIFA waombe na kuwe na CHOMBO cha kuwachunguza waombaji wote ili wenye SIFA ndio Wapitishwe na Kuhakikiwa na BUNGE.
Naamini Tutapata Viongozi Wenye SIFA ya kuiletea NCHI MAENDELEO.
Kinyume chake tutaendelea kuwa hivi hivi kwa Miaka mingine 60
 
Back
Top Bottom