Tumlaumu nani? Watu, ardhi, siasa safi au uongozi bora?

ML.NYERERE ALIWAHI KUSEMA KWAMBA" ILI NCHI IENDELEE INAHITAJI WATU, ARDHI, SIASA SAFI NA UONGOZI BORA"

Kwa kuwa uongozi bora na siasa safi ni zao la watu, hivyo basi ili nchi iendelee inahitaji WATU, ARDHI, WATU, na WATU(watu inajitokeza mara tatu kuashiria umuhimu wa watu katika maendeleo)
Kwa kifupi unaweza sema ili nchi iendelee inahitaji WATU na ARDHI. To prove this chukua mfano wa nchi ya Japan. Japan ina ardhi na watu tu , haina madini mafuta wala gesi ila kwakuwa wana "watu" Japan ni super power.

Tanzania ina Ardhi kubwa ,yenye rutuba na kila aina ya kito chenye thamani je ni kwanini hatuendelei? Tatizo la Tanzania ni WATU. Tatizo la Tanzania ni WATANZANIA. Tatizo la Tanzania ni mimi wewe na yule.

Watu huwa hawamuelewi M.h Mbatia anapokuwa anataja vipaumbele vya nchi kuwa ni 1)ELIMU 2)ELIMU 4)ELIMU 5)ELIMU 6)ELIMU 7)ELIMU 8)ELIMU 9) ELIMU, 10) na kuendelea , Afya, Miundombinu etc. Sina uhakika huwa anamaanisha nini ila naamini huwa anamaanisha umuhimu wa kumuandaa Mtanzania kuikabili ardhi ili kuleta maendeleo binafsi na Taifa kwa ujumla.. Hapa elimu ni zaid ya kukaa darasani na kutunukiwa cheti ni kujifunza discipline, patriotism, etc

Kwakuwa tatizo la Tanzania ni WATU tusibweteke tukimini maliasili zetu kama madini ,gesi ,bandari na vivutio vya utalii vitatuletea maendeleo kama wanao manage mali hizi ni watanzania (kwa kusema watanzania simaanishi maliasili ziwe managed na watu wa nje).

Kuna ka nchi kadogo kamekwisha ng`amua hilo na wanafanya massive investment kwenye elimu ya watu wake. Kwenye hako ka nchi nasikia kila mtoto wa primary ana Laptop... Na kwa uwekezaji wa namna hii usitegemee big resurt now, ni uwekezaji wa kama 30 years ndio unaanza kuona matokeo..Tusije kushangaa hako ka nchi kanakuja kutawala East Africa
 
Back
Top Bottom