Tumfundishe siasa Humphrey Polepole: Watumishi nchini, mpuuzeni huyu kijana na CCM yake

TANGAZO:
INGEPENDEZA SANA ANDIKO HILI KILA MTU ALI PRINT NA KWENDA KUBANDIKA KWENYE NOTICE BOARD ZA OFISI ZA UMMA ILI KILA MTU ASOME NA KUELEWA
Mawazo ya kitoto hayo sasa. Hizo ofisi za umma hazina taratibu ya matangazo gani yanaruhusiwa kubandika na nani anaruhusiwa kubandika??
 
Mawazo ya kitoto hayo sasa. Hizo ofisi za umma hazina taratibu ya matangazo gani yanaruhusiwa kubandika na nani anaruhusiwa kubandika??
Mnaogopa watumishi watauona mwanga siyo? Nilisema hapo juu, mtaji wenu ni ujinga na woga wa watumishi wa umma. Kwasababu ya ujinga na woga wao mnawaaminisha kuwa ni watumishi wa ccm. Siku wakijitambua mtaumbuka....
 
Mnaogopa watumishi watauona mwanga siyo? Nilisema hapo juu, mtaji wenu ni ujinga na woga wa watumishi wa umma. Kwasababu ya ujinga na woga wao mnawaaminisha kuwa ni watumishi wa ccm. Siku wakijitambua mtaumbuka....
Usichanganye mambo. Hamna ofisi yoyote inayojitambua ambayo notice board anabandika yoyote na chochote. That was my point, period
 
Chama kinachoshika mamlaka ya dola katika Nchi kinapaswa kuichunga serikali yake na kuishauri, kuionya na kuikosoa serikali katika utekelezaji wa majukumu yake ya kuhudumia wananchi.

Inashangaza kuona chama kinashindwa kujitofautisha na serikali hivyo na chenyewe kuwa kama Serikali.

Kwa mfano kuna kauli kama [HASHTAG]#ccmmpya[/HASHTAG] na [HASHTAG]#tanzaniampya[/HASHTAG] katika muktadha MPANA nashindwa kujua nani Kati ya ccm na Tanzania nani awe mpya ili mwananchi wa nchi hii apate maendeleo ya moja kwa moja.

Kwa maoni yangu binafsi sioni haja ya upya wa ccm ili nchi ipate maendeleo isipokuwa serikali inatakiwa kuwekeza rasilimali zake kuhudumia matarajio ya wananchi. Ilhali hiyo ccm mpya ikifanya shughuli zake za ki-ccm huku ikiitazama serikali ili kutimiza malengo ya ilani ya uchaguzi.

Kwa kuhitimisha tushughulike zaidi na upya wa Tanzania kuliko upya wa CCM. Hata Rais Trump pamoja na Serikali yake anashughulika na ile anayoiita [HASHTAG]#MAGA[/HASHTAG] kwa manufaa ya Nchi yake na siyo [HASHTAG]#MAGA[/HASHTAG] kwa manufaaa ya GOP.
Mungu ibariki Afrika,
Mungu ibariki Tanzania
Tatizo ni Uwaledi Wa viongozi wetu.Yaani wamesoma ila wanaonekana kama hawajasoma,they are too local,JK alikuwa ana PhD ya kupewa but at least was professional ila hawa du. Nashukuru Mungu hawatoki nje ya Tz,hii ndo salama yetu
 
vip kamati kuu ya cdm imeshamfukuza kwenye chama fisadi lowasa kwa kumsifia Rais kuwa anafanya kazi nzuri sana??

Na wewe! Kaenda mwenyewe ikulu tena sehemu yenye ulinzi mkali ajabu na mwenye majeshi yote na magereza yote alikuwepo na wakanywa chai wote! Ni kwanini hakumkamata kama kweli fisadi?

Upoyoyo wako wa kuendelea kuimba ukasuku ulioaminishwa bila wewe kutafiti ndio unaokuaibisha leo hapa. Lowasa ni msafi kuliko yeyote ndani ya CCM!
 
Mnaogopa watumishi watauona mwanga siyo? Nilisema hapo juu, mtaji wenu ni ujinga na woga wa watumishi wa umma. Kwasababu ya ujinga na woga wao mnawaaminisha kuwa ni watumishi wa ccm. Siku wakijitambua mtaumbuka....
Mimi ninavyojua kuajiriwa serikalini lazima uwe na elimu ya angalau kidato cha nne,sasa kama kuna mtu amesoma na still hajitambui basi Serikali ina haki kuwanyima nyongeza ya mshahara na stahili zao nyingine
 
Watakuja kuelewa tu kuwa siasa za bunduki sio siasa bali nikupanda juwaani. Hata Bw Yule ameanza kuelewa na usujeshangaa kewatelekeza wapayukaji wote na kujikuta hawana wakuwatetea tena.
 
Usichanganye mambo. Hamna ofisi yoyote inayojitambua ambayo notice board anabandika yoyote na chochote. That was my point, period
Kwasababu mmeshaua chama cha wafanyakazi mahali pa kazi. Maana ya notice board unaijua? Ndondocha kweli wewe. Hiyo ni stress ya kulipwa hela ya kununulia mboga za majani kwa mwezi. Na bado hugunduwi tu utoke hapo.
 
Mawazo kama akina polepole ndio yanayorudisha nyuma uzalendo wa wananchi wetu. Mtumishi wa umma atatimiza sera za CCM ambazo zitapitia katika miongozo ya serikali kupitia ofisi ya waziri mkuu ambaye ndie mtendaji mkuu wa serikali na ndiye mpokea maagizo na mtoa taarifa za utendaji wa serikali kwenye chama.

Watumishi kuwalazimisha kuwa wanaccm mnaifarakanisha jamii ktk mfumo wa vyama vingi. Watumishi wa umma hawazidi laki 5 lkn wananchi wako zaidi milion 40 je kama wewe mtumishi ni CCM utamshawishi vp mwananchi ambaye hapendi ushabiki wa siasa au ni ACT ashiriki kwenye shughuli ya maendeleo ambayo anahisi ni advantage ya chama badala ya kuwa ya serikali.

Tunawatoa watumishi kwenye uzalendo wa nchi yao kwa kuwalazimisha kuwa CCM. Ofisa wa TRA unataka ajisifie kuwa yeye ni CCM halafu walipa kodi mnataka wawe wazalendo walipe kodi kwa hiari. Hiari itakujaje wakati mnamjenga mwananchi aone kodi inaenda CCM badala ya serikalini kunufaisha watu wote!

Acheni watumishi wa umma wafanyekazi kwa job description zao matokeo ya kazi ndo nyinyi CCM mwende mkajisifie lakini sio kuwalazimisha watumishi wawe wanasiasa ndo mnafikiri mnaleta maendeleo. Wabunge na madiwani wanatosha sana kufanya siasa.
 
Wiki jana nimeona kuna video ikimuonyesha mtu aliyejitambulisha kuwa ni Humphrey Polepole Katibu wa Itikadi na Ueneze CCM, Katika video hii anaonekana akiwatishia watumishi wa umma nchini kwamba lazima wote wawe wanaccm, anasisitiza watakao kaidi watashughulikia kwakupoteza ajira zao au hila nyingine nyingi watafanyiwa.

Naomba kwa ridhaa yenu wadau, nimfundishe siasa kidogo Ndugu yangu Polepole na Chama chake cha Mapinduzi ili waache ulaghai na vitisho kwa watumishi wa Umma nchini. Nafanya hivyo kwakutambua dhana ya vitisho hivyo ambavyo kimsingi vinatokana na ama kutojua siasa na mantiki zake zote.

Kwanza kabisa Polepole namfundisha jambo muhimu kwamba Tanzania ni nchi ya mfumo wa vyamba vingi, na kubwa zaidi afahamu mfumo wa serikali iliyotokana na mfumo wa vyama vingi ni tofauti sana kiutendaji na mfumo wa chama kimoja ambao huwa unataka watumishi wote katika nchi kuwa wanachama wa chama kilichoshika hatamu. Hapa tu ndio Polepole na ccm wanapolewa madaraka kwasababu katba ya ccm mpaka leo ina elements za Chama kimoja nchini na inawapumbaza wanaccm wengi ikiwemo Polepole kuhisi upinzani ni haramu nchini hali inayofikia wakalipuka kwa kauli za kitoto kama hizi kwamba watumishi wote wawe wanaccm, hata azimio la Zanzibar la 1992 lililozaa mfumo wa vyama vingi ccm hawalielewi au hawalitaki kabisa

Siasa ni itikadi inayofuatwa na kundi au jamii fulani ambayo ni msingi kuendesha uchumi, utamaduni na mwenendo mzima maisha ya jamii hiyo. Siasa maana yake ni njia azitumiazo mtu au kundi la watu kupata nguvu na madaraka, na ikitokea mtu akapata nguvu hizo huendelea na hatua ya pili ya njia hizo ili kuhahihisha anabaki na nguvu zake au na madaraka yake kwa lengo la kuendelea kufanya kile alichokikusudia. Kinachogomba hapo ni mamlaka/madaraka/nguvu azipatazo mwanasiasa anazitumia kwa maslahi ya nani. Hapa ndipo Polepole na CCM walipo, wao maslahi ni ya chama zaidi kuliko taifa.

Kifalsafa Mwanasiasa ni adui wa uzalendo, simuumini wa uzalendo, huamini katika itikadi ya siasa yake. Uzalendo na siasa hukinzana lakini uzalendo huo huhanikizwa katika siasa.
Chama cha kisiasa ni maungano ya watu wanaotafuta mamlaka katika dola na hasa serikali kwa kusudi la kutekeleza shabaha za kisiasa au za kifalsafa pamoja na faida kwa ajili ya vikundi fulani, faida zao za binafsi.

Vyama mara nyingi hutamka mwelekeo au itikadi fulani inayoandikwa katika ilani yao. Katika mfumo wa vyama vingi kila chama kinagombea nafasi za bunge au serikali dhidi ya vyama vingine. Wakati wa uchaguzi kila chama kinapaswa kujieleza, kutetea matendo yake ya nyuma na kuonyesha jinsi kinavyotaka kuboresha mambo tofauti na vyama vingine. Kwa njia hii kila chama huchangia harakati ya kujenga nia ya jamii inamofanya kazi kama inashinda au kushindwa kwenye uchaguzi.

Penye mfumo wa chama kimoja kazi ya chama itakuwa tofauti. Historia ina mifano ya kwamba chama pekee katika nchi, kinaelekea kwenye udikteta kwa viwango tofauti. Vyama hutofautiana sana kuhusu kiasi cha tofauti za maoni zinazoruhusiwa ndani yao, uhusiano kati ya viongozi na wanachama, kiasi cha uwezo wa wanachama kuathiri mwelekeo wa chama na umuhimu wa ilani.

Madhumuni ya kuwa na vyama vingi vya siasa ni kuleta ushindani wa kisiasa, ili kuleta maendeleo ya nchi upinzani wa kisiasa sio uadui kama watu wengi kwenye nchi zinazoendelea wanavyodhani (hususani Tanzani wanaccm), kuwa na vyama vingi ni kuongeza wigo wa demokrasia katika jamii huska. Chama kinaposhika madaraka kinaunda serikali, baada tu ya kuunda serikali, basi serikali ile KAMWE haitaongozwa kwa sheria, katiba, kanuni, mfumo wa chama wala kuingiliwa katika utendaji wake.

Nchini Tanzania serikali huanza kutenda kazi zake kwa mjibu wa Katiba, Kanuni na Sheria za nchi pale tu inaposhika madaka yake na sio Katiba ya CCM au sheria za CCM.
Wizara ya utumishi wa umma ndio inayoratibu watumishi wa umma wote, kila mtumishi atafanya kazi kwakuzingatia sheria ya utumishi wa umma na miiko ya utumishi wa umma tu, na sio miiko na miongozo ya ccm. Vilevile serikali itatekeleza sera za kiinchi kwakufuata sera zilizopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi,Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu. Hii ndio wizara inayohusika na Sera za kitaifa.

Kifungu cha 3 cha Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003, na Kifungu cha 1(26) cha Kanuni za Kudumu za mwaka 2009 vinatoa tafsiri ya neno mtumishi wa umma, kuwa ni yule aliyeajiriwa,kuteuliwa au kuchaguliwa kufanya kazi katika mihimili yote mitatu ya Tanzania ambayo ni serikali ya Jamhuri ya Muungano, Bunge na Mahakama, na ni yule anayelipwa mshahara na serikali ya Jamhuri ya Muungano. Katika maelezo hayo ya tafsiri, ccm ya Polepole haijatajwa popote.

Mpaka hapo ukiangalia hata kwa mantiki ya kitoto tu, huoni ccm ikiingizwa katika utumishi wala sera kiutendaji, Unawza kujiuliza Polepole ametumia sheria ipi kutoa kauli ile ya kichama? Je anajua anachokizungumza au anazungumza kutishia tu watumishi nchini?

Kwakumsaidia tu Polepole namna chama chake kinavyoweza kuingia na kujua serikali yake inatekelezaje mapendekezo ya ilani ya ccm, ni pale tu ambapo vikao vya chama vinapokaa ndipo katiba ya ccm inasema wajumbe wa kata,wilaya, mkoa na taifa ambao wapo kwenye utumishi wa umma, (DC, RC na Rais) hawa wanatakiwa kupeleka mrejesho wa namna serikali ilivyotumia mapendekezo ya ilani yake.

Hapa kumbuka, Serikali iliyoundwa na chama tawala hailazimishwi kutumia 100% ya ilani na sera zilizonadiwa na chama hicho kwenye uchaguzi. HAKUNA sheria ya kuilazimisha kutumia ilani hiyo. Mfano mzuri ni Serikali ya Rais Magufuli ununuzi wa ndege, ujenzi wa uwanja Chato nk, mengi inayoyatenda hayapo kwenye Ilani ya ccm, wakati huo ccm hana uwezo wakuwajibisha serikali hii kwakuwa hakuna kifungu cha sheria za nchi kitakachotafsiri kuwa serikali imekivunja kwakutotumia ilani ya ccm.

Wajibu pekee wa kisiasa wa chama cha mapinduzi ni kuishauri serikali yake kutekeleza ilani na sera zake, Narudia ni kushauri tu na sio vinginevyo, yaani kushauri kuna mambo mawili, ama ushauri upokelewe, ama upigwe chini. Hakuna ushauri wa lazima. Ndio malengo na nadharia halisi ya mfumo wa vyama vingi.

Hivyo porojo za Hamfrey Polepole ni porojo za mzee Kimweri mjukuu wa Abunuwasi, Watumishi wa Umma mpuuzeni Polepole na CCM yake hawana uwezo wakuwafukuza kazi wala kuwagusa, ccm sio mamlaka yenu ya uajiri, ccm inaishia kwenye kuunda serikali tu, bada ya hapo ikafie Lumumba kule sio kuvuruga watumishi wala kuwatisha, Mamlaka ya watumishi ni wizara ya Utumishi na sio CCM ya Polepole.

Na Yericko Nyerere
Yote juu ya yote, ahadi za viongozi (ilani za uchaguzi za vyama) wakati wa kuomba kura, ndizo hutumika kwenye kuendesha serikali. Mtumishi wa serikali ambaye hukiuka ilani ya uchaguzi ya chama kilichopata ridhaa ya kuongoza nchi, moja kwa moja ni muhujumu wa chama hicho kiasi cha kukikosanisha na wananchi (wwapiga kura).
Kwa hali yoyote ile, lazima chama tawala kiwe macho na viongozi / watumishi wa serikali katika kuhakikisha kwamba kile kilichoahidiwa kinatekelezwa.
Inawezekana Polepole akanukuliwa vibaya lakini naamini alikuwa sahihi!
 
Kwasababu mmeshaua chama cha wafanyakazi mahali pa kazi. Maana ya notice board unaijua? Ndondocha kweli wewe. Hiyo ni stress ya kulipwa hela ya kununulia mboga za majani kwa mwezi. Na bado hugunduwi tu utoke hapo.
Lugha yako imetosha kabisa kueleza upeo wa akili yako. Eti hela ya mboga za majani!
 
Yote juu ya yote, ahadi za viongozi (ilani za uchaguzi za vyama) wakati wa kuomba kura, ndizo hutumika kwenye kuendesha serikali. Mtumishi wa serikali ambaye hukiuka ilani ya uchaguzi ya chama kilichopata ridhaa ya kuongoza nchi, moja kwa moja ni muhujumu wa chama hicho kiasi cha kukikosanisha na wananchi (wwapiga kura).
Kwa hali yoyote ile, lazima chama tawala kiwe macho na viongozi / watumishi wa serikali katika kuhakikisha kwamba kile kilichoahidiwa kinatekelezwa.
Inawezekana Polepole akanukuliwa vibaya lakini naamini alikuwa sahihi!
Chama kinatakiwa kumsimamia Rais ambaye amebeba ilani ya chama na siyo chama kudeal na watumishi wa umma.
 
mshahara wa watumishi wa umma unatokana na kodi za watumishi wa umma na wasio wa umma. polepole angelijuwa hilo asingeongea huo ubwege.
 
Niliiona hii clip tangu wiki iliyopita nikataka kuandikia ingawa kwa namna tofauti na ulivyoiweka. Lakini nikakumbuka kuwa wengine hatutakiwi kuanzisha thread kwenye hili Jukwaa zaidi ya ku comment tu,(kwa experience ya nyuzi zangu zinavyi nyofolewa au kuunganishwa) ikanibidi niahirishe. Nikasema si mbaya almwingine akiiona ataianzishia thread.
 
Mimi ninavyojua kuajiriwa serikalini lazima uwe na elimu ya angalau kidato cha nne,sasa kama kuna mtu amesoma na still hajitambui basi Serikali ina haki kuwanyima nyongeza ya mshahara na stahili zao nyingine
Kwani umeshasikia wakidai? Tafakari hilo
 
Back
Top Bottom