Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,987
- 20,271
Wiki jana nimeona kuna video ikimuonyesha mtu aliyejitambulisha kuwa ni Humphrey Polepole Katibu wa Itikadi na Ueneze CCM, Katika video hii anaonekana akiwatishia watumishi wa umma nchini kwamba lazima wote wawe wanaccm, anasisitiza watakao kaidi watashughulikia kwakupoteza ajira zao au hila nyingine nyingi watafanyiwa.
Naomba kwa ridhaa yenu wadau, nimfundishe siasa kidogo Ndugu yangu Polepole na Chama chake cha Mapinduzi ili waache ulaghai na vitisho kwa watumishi wa Umma nchini. Nafanya hivyo kwakutambua dhana ya vitisho hivyo ambavyo kimsingi vinatokana na ama kutojua siasa na mantiki zake zote.
Kwanza kabisa Polepole namfundisha jambo muhimu kwamba Tanzania ni nchi ya mfumo wa vyamba vingi, na kubwa zaidi afahamu mfumo wa serikali iliyotokana na mfumo wa vyama vingi ni tofauti sana kiutendaji na mfumo wa chama kimoja ambao huwa unataka watumishi wote katika nchi kuwa wanachama wa chama kilichoshika hatamu. Hapa tu ndio Polepole na ccm wanapolewa madaraka kwasababu katba ya ccm mpaka leo ina elements za Chama kimoja nchini na inawapumbaza wanaccm wengi ikiwemo Polepole kuhisi upinzani ni haramu nchini hali inayofikia wakalipuka kwa kauli za kitoto kama hizi kwamba watumishi wote wawe wanaccm, hata azimio la Zanzibar la 1992 lililozaa mfumo wa vyama vingi ccm hawalielewi au hawalitaki kabisa
Siasa ni itikadi inayofuatwa na kundi au jamii fulani ambayo ni msingi kuendesha uchumi, utamaduni na mwenendo mzima maisha ya jamii hiyo. Siasa maana yake ni njia azitumiazo mtu au kundi la watu kupata nguvu na madaraka, na ikitokea mtu akapata nguvu hizo huendelea na hatua ya pili ya njia hizo ili kuhahihisha anabaki na nguvu zake au na madaraka yake kwa lengo la kuendelea kufanya kile alichokikusudia. Kinachogomba hapo ni mamlaka/madaraka/nguvu azipatazo mwanasiasa anazitumia kwa maslahi ya nani. Hapa ndipo Polepole na CCM walipo, wao maslahi ni ya chama zaidi kuliko taifa.
Kifalsafa Mwanasiasa ni adui wa uzalendo, simuumini wa uzalendo, huamini katika itikadi ya siasa yake. Uzalendo na siasa hukinzana lakini uzalendo huo huhanikizwa katika siasa.
Chama cha kisiasa ni maungano ya watu wanaotafuta mamlaka katika dola na hasa serikali kwa kusudi la kutekeleza shabaha za kisiasa au za kifalsafa pamoja na faida kwa ajili ya vikundi fulani, faida zao za binafsi.
Vyama mara nyingi hutamka mwelekeo au itikadi fulani inayoandikwa katika ilani yao. Katika mfumo wa vyama vingi kila chama kinagombea nafasi za bunge au serikali dhidi ya vyama vingine. Wakati wa uchaguzi kila chama kinapaswa kujieleza, kutetea matendo yake ya nyuma na kuonyesha jinsi kinavyotaka kuboresha mambo tofauti na vyama vingine. Kwa njia hii kila chama huchangia harakati ya kujenga nia ya jamii inamofanya kazi kama inashinda au kushindwa kwenye uchaguzi.
Penye mfumo wa chama kimoja kazi ya chama itakuwa tofauti. Historia ina mifano ya kwamba chama pekee katika nchi, kinaelekea kwenye udikteta kwa viwango tofauti. Vyama hutofautiana sana kuhusu kiasi cha tofauti za maoni zinazoruhusiwa ndani yao, uhusiano kati ya viongozi na wanachama, kiasi cha uwezo wa wanachama kuathiri mwelekeo wa chama na umuhimu wa ilani.
Madhumuni ya kuwa na vyama vingi vya siasa ni kuleta ushindani wa kisiasa, ili kuleta maendeleo ya nchi upinzani wa kisiasa sio uadui kama watu wengi kwenye nchi zinazoendelea wanavyodhani (hususani Tanzani wanaccm), kuwa na vyama vingi ni kuongeza wigo wa demokrasia katika jamii huska. Chama kinaposhika madaraka kinaunda serikali, baada tu ya kuunda serikali, basi serikali ile KAMWE haitaongozwa kwa sheria, katiba, kanuni, mfumo wa chama wala kuingiliwa katika utendaji wake.
Nchini Tanzania serikali huanza kutenda kazi zake kwa mjibu wa Katiba, Kanuni na Sheria za nchi pale tu inaposhika madaka yake na sio Katiba ya CCM au sheria za CCM.
Wizara ya utumishi wa umma ndio inayoratibu watumishi wa umma wote, kila mtumishi atafanya kazi kwakuzingatia sheria ya utumishi wa umma na miiko ya utumishi wa umma tu, na sio miiko na miongozo ya ccm. Vilevile serikali itatekeleza sera za kiinchi kwakufuata sera zilizopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi,Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu. Hii ndio wizara inayohusika na Sera za kitaifa.
Kifungu cha 3 cha Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003, na Kifungu cha 1(26) cha Kanuni za Kudumu za mwaka 2009 vinatoa tafsiri ya neno mtumishi wa umma, kuwa ni yule aliyeajiriwa,kuteuliwa au kuchaguliwa kufanya kazi katika mihimili yote mitatu ya Tanzania ambayo ni serikali ya Jamhuri ya Muungano, Bunge na Mahakama, na ni yule anayelipwa mshahara na serikali ya Jamhuri ya Muungano. Katika maelezo hayo ya tafsiri, ccm ya Polepole haijatajwa popote.
Mpaka hapo ukiangalia hata kwa mantiki ya kitoto tu, huoni ccm ikiingizwa katika utumishi wala sera kiutendaji, Unawza kujiuliza Polepole ametumia sheria ipi kutoa kauli ile ya kichama? Je anajua anachokizungumza au anazungumza kutishia tu watumishi nchini?
Kwakumsaidia tu Polepole namna chama chake kinavyoweza kuingia na kujua serikali yake inatekelezaje mapendekezo ya ilani ya ccm, ni pale tu ambapo vikao vya chama vinapokaa ndipo katiba ya ccm inasema wajumbe wa kata,wilaya, mkoa na taifa ambao wapo kwenye utumishi wa umma, (DC, RC na Rais) hawa wanatakiwa kupeleka mrejesho wa namna serikali ilivyotumia mapendekezo ya ilani yake.
Hapa kumbuka, Serikali iliyoundwa na chama tawala hailazimishwi kutumia 100% ya ilani na sera zilizonadiwa na chama hicho kwenye uchaguzi. HAKUNA sheria ya kuilazimisha kutumia ilani hiyo. Mfano mzuri ni Serikali ya Rais Magufuli ununuzi wa ndege, ujenzi wa uwanja Chato nk, mengi inayoyatenda hayapo kwenye Ilani ya ccm, wakati huo ccm hana uwezo wakuwajibisha serikali hii kwakuwa hakuna kifungu cha sheria za nchi kitakachotafsiri kuwa serikali imekivunja kwakutotumia ilani ya ccm.
Wajibu pekee wa kisiasa wa chama cha mapinduzi ni kuishauri serikali yake kutekeleza ilani na sera zake, Narudia ni kushauri tu na sio vinginevyo, yaani kushauri kuna mambo mawili, ama ushauri upokelewe, ama upigwe chini. Hakuna ushauri wa lazima. Ndio malengo na nadharia halisi ya mfumo wa vyama vingi.
Hivyo porojo za Hamfrey Polepole ni porojo za mzee Kimweri mjukuu wa Abunuwasi, Watumishi wa Umma mpuuzeni Polepole na CCM yake hawana uwezo wakuwafukuza kazi wala kuwagusa, ccm sio mamlaka yenu ya uajiri, ccm inaishia kwenye kuunda serikali tu, bada ya hapo ikafie Lumumba kule sio kuvuruga watumishi wala kuwatisha, Mamlaka ya watumishi ni wizara ya Utumishi na sio CCM ya Polepole.
Na Yericko Nyerere