Tumfundishe siasa Humphrey Polepole: Watumishi nchini, mpuuzeni huyu kijana na CCM yake

Yote juu ya yote, ahadi za viongozi (ilani za uchaguzi za vyama) wakati wa kuomba kura, ndizo hutumika kwenye kuendesha serikali. Mtumishi wa serikali ambaye hukiuka ilani ya uchaguzi ya chama kilichopata ridhaa ya kuongoza nchi, moja kwa moja ni muhujumu wa chama hicho kiasi cha kukikosanisha na wananchi (wwapiga kura).
Kwa hali yoyote ile, lazima chama tawala kiwe macho na viongozi / watumishi wa serikali katika kuhakikisha kwamba kile kilichoahidiwa kinatekelezwa.
Inawezekana Polepole akanukuliwa vibaya lakini naamini alikuwa sahihi!

TE="Massanda OMtima Massanda, post: 25330432, member: 440907"]Yote juu ya yote, ahadi za viongozi (ilani za uchaguzi za vyama) wakati wa kuomba kura, ndizo hutumika kwenye kuendesha serikali. Mtumishi wa serikali ambaye hukiuka ilani ya uchaguzi ya chama kilichopata ridhaa ya kuongoza nchi, moja kwa moja ni muhujumu wa chama hicho kiasi cha kukikosanisha na wananchi (wwapiga kura).
Kwa hali yoyote ile, lazima chama tawala kiwe macho na viongozi / watumishi wa serikali katika kuhakikisha kwamba kile kilichoahidiwa kinatekelezwa.
Inawezekana Polepole akanukuliwa vibaya lakini naamini alikuwa sahihi![/QUOTE]
Hapo ndo mnapokosea, mtumishi wa umma anafanyakazi kwa miongozo ya serikali. Anaajiriwa kwa taaluma yake na analipwa kwa ajira yake. Hawatakiwi kufanya kazi kwa matamanio ya mtu. Mnataka daktari awe mwanaccm halafu sindano amchome ccm mwenzie akija chadema akatae asema wewe unampenda Tundu Lissu kwahiyo hatukutibu. Waacheni watumishi wa umma wafanyekazi kwa mjibu wa taratibu za serikali. Mambo ya kuhujumu yanakujaje si atakuwa ameenda nje ya job description zake na atawajibishwa. Uzalendo wa nchi hapimwi kwa kuwa mwanaccm tu.
 
Aiseee kwa kauli kama ya Polepole nilikua sihamini jamaa ana matatizo makubwa sana anaitaji msaada wa haraka sana huwezi kulazimisha watu wote wawe CCM au chadema kuna watu hatuna vyama
 
Mawazo ya kitoto hayo sasa. Hizo ofisi za umma hazina taratibu ya matangazo gani yanaruhusiwa kubandika na nani anaruhusiwa kubandika??
Kwani lazima kupata kibali? Unabandika unasepa, mpaka wanalitoa wengi watakuwa wamesoma na kujielewa
 
Mkuu;
Hii elimu ungeanza kwanza kumpa Mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Pwani, Sumaye ambaye alituambia kuwa tukitaka mambo yetu yanyoke lazima kwanza tujiunge CCM.

Inawezekana Polepole amepata hoja zake kutoka kwa Sumaye!

Kwa kukuelisha zaidi nadhani unashindwa kuelewa kuwa chama tawala ndicho kimeiweka serikali madarakani kupitia kura za wananchi wengi.

Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, Uwezekano wa kumfukuza Rais na serikali yake ni mkubwa ndani ya chama kuliko bunge pale anaposhindwa kutekeleza ilani ya chama kama ambavyo chama kilipewa ridhaa na watanzania wengi.

Mfanyakazi wa serikali lazima atekeleze sera za chama tawala hata kama hazipendi. Kutokutekeleza sera za chama tawala ni sababu tosha ya kufukuzwa kazi kwa sababu atakuwa amevunja mkataba wake.

Kwa mfano, Serikali ikija na sera ya matibabu bure katika hospitali za serikali halafu kukatokea daktari wa hospitali hizo na kuanza kutoza pesa, huyo daktari atakuwa anavunja sheria na anaweza kufukuzwa kazini.

Kumbuka sera hutungiwa sheria na kanuni ili zitumike kisheria.

Kumbuka wakuu wa wafanyakazi serikalini ni wateuliwa wa Rais,
Ndo umeandika nini sasa aise mtu mzima alafu siyo mtoto kumbukakumbuka nyingi umeishia kuandika nonsese
 
Tayari keshaokoka na hata wana wa Nchi hii nadhani walishamsamehe mintarafu kauli Ile.
Isitoshe ile ilikuwa ni ulevi tu wa Madaraka, umeshamtoka. He is completely sober.
Basi haya,lakini unataarifa kuwa wiki ijayo ana ziara ya sifa pale karibu na soko la samaki??Yuko timamu kabisa mkuu.
 
Kwa kauli hii ya Polepole, maana yake kila mtumishi wa umma anatakiwa kuwa na kadi ya chama tawala.
 
Yericko Nyerere mdogo wangu hebu liweke hili bandiko lako kwa mfumo wa PDF ili tu-print na kulibandika kila mahali watu wajisomee! Pole pole ni nyoko sana!
 
Wiki jana nimeona kuna video ikimuonyesha mtu aliyejitambulisha kuwa ni Humphrey Polepole Katibu wa Itikadi na Ueneze CCM, Katika video hii anaonekana akiwatishia watumishi wa umma nchini kwamba lazima wote wawe wanaccm, anasisitiza watakao kaidi watashughulikia kwakupoteza ajira zao au hila nyingine nyingi watafanyiwa.

Naomba kwa ridhaa yenu wadau, nimfundishe siasa kidogo Ndugu yangu Polepole na Chama chake cha Mapinduzi ili waache ulaghai na vitisho kwa watumishi wa Umma nchini. Nafanya hivyo kwakutambua dhana ya vitisho hivyo ambavyo kimsingi vinatokana na ama kutojua siasa na mantiki zake zote.

Kwanza kabisa Polepole namfundisha jambo muhimu kwamba Tanzania ni nchi ya mfumo wa vyamba vingi, na kubwa zaidi afahamu mfumo wa serikali iliyotokana na mfumo wa vyama vingi ni tofauti sana kiutendaji na mfumo wa chama kimoja ambao huwa unataka watumishi wote katika nchi kuwa wanachama wa chama kilichoshika hatamu. Hapa tu ndio Polepole na ccm wanapolewa madaraka kwasababu katba ya ccm mpaka leo ina elements za Chama kimoja nchini na inawapumbaza wanaccm wengi ikiwemo Polepole kuhisi upinzani ni haramu nchini hali inayofikia wakalipuka kwa kauli za kitoto kama hizi kwamba watumishi wote wawe wanaccm, hata azimio la Zanzibar la 1992 lililozaa mfumo wa vyama vingi ccm hawalielewi au hawalitaki kabisa

Siasa ni itikadi inayofuatwa na kundi au jamii fulani ambayo ni msingi kuendesha uchumi, utamaduni na mwenendo mzima maisha ya jamii hiyo. Siasa maana yake ni njia azitumiazo mtu au kundi la watu kupata nguvu na madaraka, na ikitokea mtu akapata nguvu hizo huendelea na hatua ya pili ya njia hizo ili kuhahihisha anabaki na nguvu zake au na madaraka yake kwa lengo la kuendelea kufanya kile alichokikusudia. Kinachogomba hapo ni mamlaka/madaraka/nguvu azipatazo mwanasiasa anazitumia kwa maslahi ya nani. Hapa ndipo Polepole na CCM walipo, wao maslahi ni ya chama zaidi kuliko taifa.

Kifalsafa Mwanasiasa ni adui wa uzalendo, simuumini wa uzalendo, huamini katika itikadi ya siasa yake. Uzalendo na siasa hukinzana lakini uzalendo huo huhanikizwa katika siasa.
Chama cha kisiasa ni maungano ya watu wanaotafuta mamlaka katika dola na hasa serikali kwa kusudi la kutekeleza shabaha za kisiasa au za kifalsafa pamoja na faida kwa ajili ya vikundi fulani, faida zao za binafsi.

Vyama mara nyingi hutamka mwelekeo au itikadi fulani inayoandikwa katika ilani yao. Katika mfumo wa vyama vingi kila chama kinagombea nafasi za bunge au serikali dhidi ya vyama vingine. Wakati wa uchaguzi kila chama kinapaswa kujieleza, kutetea matendo yake ya nyuma na kuonyesha jinsi kinavyotaka kuboresha mambo tofauti na vyama vingine. Kwa njia hii kila chama huchangia harakati ya kujenga nia ya jamii inamofanya kazi kama inashinda au kushindwa kwenye uchaguzi.

Penye mfumo wa chama kimoja kazi ya chama itakuwa tofauti. Historia ina mifano ya kwamba chama pekee katika nchi, kinaelekea kwenye udikteta kwa viwango tofauti. Vyama hutofautiana sana kuhusu kiasi cha tofauti za maoni zinazoruhusiwa ndani yao, uhusiano kati ya viongozi na wanachama, kiasi cha uwezo wa wanachama kuathiri mwelekeo wa chama na umuhimu wa ilani.

Madhumuni ya kuwa na vyama vingi vya siasa ni kuleta ushindani wa kisiasa, ili kuleta maendeleo ya nchi upinzani wa kisiasa sio uadui kama watu wengi kwenye nchi zinazoendelea wanavyodhani (hususani Tanzani wanaccm), kuwa na vyama vingi ni kuongeza wigo wa demokrasia katika jamii huska. Chama kinaposhika madaraka kinaunda serikali, baada tu ya kuunda serikali, basi serikali ile KAMWE haitaongozwa kwa sheria, katiba, kanuni, mfumo wa chama wala kuingiliwa katika utendaji wake.

Nchini Tanzania serikali huanza kutenda kazi zake kwa mjibu wa Katiba, Kanuni na Sheria za nchi pale tu inaposhika madaka yake na sio Katiba ya CCM au sheria za CCM.
Wizara ya utumishi wa umma ndio inayoratibu watumishi wa umma wote, kila mtumishi atafanya kazi kwakuzingatia sheria ya utumishi wa umma na miiko ya utumishi wa umma tu, na sio miiko na miongozo ya ccm. Vilevile serikali itatekeleza sera za kiinchi kwakufuata sera zilizopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi,Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu. Hii ndio wizara inayohusika na Sera za kitaifa.

Kifungu cha 3 cha Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003, na Kifungu cha 1(26) cha Kanuni za Kudumu za mwaka 2009 vinatoa tafsiri ya neno mtumishi wa umma, kuwa ni yule aliyeajiriwa,kuteuliwa au kuchaguliwa kufanya kazi katika mihimili yote mitatu ya Tanzania ambayo ni serikali ya Jamhuri ya Muungano, Bunge na Mahakama, na ni yule anayelipwa mshahara na serikali ya Jamhuri ya Muungano. Katika maelezo hayo ya tafsiri, ccm ya Polepole haijatajwa popote.

Mpaka hapo ukiangalia hata kwa mantiki ya kitoto tu, huoni ccm ikiingizwa katika utumishi wala sera kiutendaji, Unawza kujiuliza Polepole ametumia sheria ipi kutoa kauli ile ya kichama? Je anajua anachokizungumza au anazungumza kutishia tu watumishi nchini?

Kwakumsaidia tu Polepole namna chama chake kinavyoweza kuingia na kujua serikali yake inatekelezaje mapendekezo ya ilani ya ccm, ni pale tu ambapo vikao vya chama vinapokaa ndipo katiba ya ccm inasema wajumbe wa kata,wilaya, mkoa na taifa ambao wapo kwenye utumishi wa umma, (DC, RC na Rais) hawa wanatakiwa kupeleka mrejesho wa namna serikali ilivyotumia mapendekezo ya ilani yake.

Hapa kumbuka, Serikali iliyoundwa na chama tawala hailazimishwi kutumia 100% ya ilani na sera zilizonadiwa na chama hicho kwenye uchaguzi. HAKUNA sheria ya kuilazimisha kutumia ilani hiyo. Mfano mzuri ni Serikali ya Rais Magufuli ununuzi wa ndege, ujenzi wa uwanja Chato nk, mengi inayoyatenda hayapo kwenye Ilani ya ccm, wakati huo ccm hana uwezo wakuwajibisha serikali hii kwakuwa hakuna kifungu cha sheria za nchi kitakachotafsiri kuwa serikali imekivunja kwakutotumia ilani ya ccm.

Wajibu pekee wa kisiasa wa chama cha mapinduzi ni kuishauri serikali yake kutekeleza ilani na sera zake, Narudia ni kushauri tu na sio vinginevyo, yaani kushauri kuna mambo mawili, ama ushauri upokelewe, ama upigwe chini. Hakuna ushauri wa lazima. Ndio malengo na nadharia halisi ya mfumo wa vyama vingi.

Hivyo porojo za Hamfrey Polepole ni porojo za mzee Kimweri mjukuu wa Abunuwasi, Watumishi wa Umma mpuuzeni Polepole na CCM yake hawana uwezo wakuwafukuza kazi wala kuwagusa, ccm sio mamlaka yenu ya uajiri, ccm inaishia kwenye kuunda serikali tu, bada ya hapo ikafie Lumumba kule sio kuvuruga watumishi wala kuwatisha, Mamlaka ya watumishi ni wizara ya Utumishi na sio CCM ya Polepole.

Na Yericko Nyerere
Huyu Polepole huwa sihangaiki naye sababu namjua vizuri ni ZWAZWA tangu nikiwa naye Azania sekondari nilishangaa kwa nini aliteuliwa kuwa mjumbe katika tume ya kukusanya maoni yaliyohusu kupata katiba mpya. Huyu hana tofauti na kinyonga
 
MsemajiUkweli Mimi sikuzisikia hoja za Polepole, lakini kwa makala ya Yericko, ni kama vile aliagiza watumishi wote wa Umma wawe wanachama wa CCM. Kama ni hivyo Yericko yuko sawa. Kama alimaanisha watumishi wa Umma kutekeleza ilani ya CCM, wewe upo sawa.
 
Awamu ya Washamba na Malimbukeni wa madaraka hii.

Wamejaa chuki, ubinafsi, ukatili, woga na unafiki! Hayo maneno ya Polepole yanavunja Zaidi ya 75% ya Sheria za Nchi na Katiba ya nchi, lakini yuko huru anadunda!

Hawa akina Polepole ni fungu la walioshindwa tu, ambao kwa upumbavu wao hawajui wala kukubali kuwa wameshashindwa 100%, sasa wanatumia nguvu kubwa na rasilimali za nchi kutafuta uhalali, ikibidi hata sababu mfu za pembezoni za kushindwa kwao na anguko, wanazitumia.
 
Mkuu inaonekana ulik
Mkuu;
Hii elimu ungeanza kwanza kumpa Mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Pwani, Sumaye ambaye alituambia kuwa tukitaka mambo yetu yanyoke lazima kwanza tujiunge CCM.

Inawezekana Polepole amepata hoja zake kutoka kwa Sumaye!

Kwa kukuelisha zaidi nadhani unashindwa kuelewa kuwa chama tawala ndicho kimeiweka serikali madarakani kupitia kura za wananchi wengi.

Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, Uwezekano wa kumfukuza Rais na serikali yake ni mkubwa ndani ya chama kuliko bunge pale anaposhindwa kutekeleza ilani ya chama kama ambavyo chama kilipewa ridhaa na watanzania wengi.

Mfanyakazi wa serikali lazima atekeleze sera za chama tawala hata kama hazipendi. Kutokutekeleza sera za chama tawala ni sababu tosha ya kufukuzwa kazi kwa sababu atakuwa amevunja mkataba wake.

Kwa mfano, Serikali ikija na sera ya matibabu bure katika hospitali za serikali halafu kukatokea daktari wa hospitali hizo na kuanza kutoza pesa, huyo daktari atakuwa anavunja sheria na anaweza kufukuzwa kazini.

Kumbuka sera hutungiwa sheria na kanuni ili zitumike kisheria.

Kumbuka wakuu wa wafanyakazi serikalini ni wateuliwa wa Rais,


Mkuu inaonekana ulikuwa mzito sana darasani maana Yericko kaelezea kinagaubaga uhusiano wa chama kinachounda serikali na serikali yenyewe kisha nafasi ya watumishi wa umma katika serikali, lakini kwako bado kabisa.

Hakuna kwa vyovyote ccm inaweza kumfukuza mtumishi wa umma kazi, huo mfano wako unaotoa kuhusu Daktari cjui kutoza pesa wala hauna mahusiano hapa. Kinachotunga sera kwamba watu watibiwe bure na kuweka sheria ni SERIKALI na daktari kama mtumishi wa umma anatekeleza sera na sheria zinazotungwa na serikali katika sehemu yake, sasa huyo dakatari akitoza pesa wakati serikali imesema matibabu ni bure anatakiwa kuwajibishwa na SERIKALI /MUAJIRI WAKE na siyo CCM.

Kazi ya ccm ni kuhakikisha serikali yao inatekeleza yale waliyoyahahidi kupitia ilani na serikali uhakikisha hayo kupitia watumishi wa umma, kwa mantiki hiyo ccm inaweza kushughulikia serikali yao na serikali inaweza kuwashughulikia watumishi wanaokwamisha ilani ILA CCM haiwezi kujiingiza kwa watumishi.
 
Back
Top Bottom