Tumezidi ushamba

Safi wambie na wasukuma wenzio akina Bashite waache kick za kishamba
 
Sio poa hata kama tunadaiwa,huu mtindo wa kuzuia ndege ni kama utekaji.ina maana sheria zinaruhusu kuzuia ndege pale nchi daiwa inaposhindwa kulipa deni? Na bora deni tungekuwa na tumekopa fedha hivi karibuni kwa masuala ya maendeleo,sasa deni la miaka 37 iliyopita,si unajua awamu hiii inajitahidi kufanya hili na lile ili tuweze kusonga mbele kiuchumi,bila kujali mapungufu ya hapa na pale.kwahiyo hili la ndege yetu kuzuiwa halijakaa poa,linaumiza,

Kuhusu kuandamana ,si jambo baya wala ushamba,kuandamana ni namna tu ya kufikisha ujumbe sehemu husika.kila mtu ana haki ya kufanya jambo anavyojisikia,ahakikishe tu havunji sheria.
 

Deni la miaka 37, umesema.

Kwa nini halijalipwa miaka yote hiyo?
 
Unajifanya hukumbuki wanaijeria walifanya nini kwa wasauzi. Napongeza vijana walioandamana

Kila siku wapinzani wakitaka kuandamana si kuonyesha kutotengewa haki si huwa mnaponda? Je ni kipi kinawafanya muone maandamano haya ni sawa? Nadhani sasa mmeona madhara ya kushabikia hujuma.
 
Kuandamana dhidi ya uhalifu ni jambo jingine kabisa.

Lakini kuandamana kwa sababu ndege yenu imeshikiliwa kwa sababu hamjalipa deni, ni ujinga na ushamba.

Mnaandamania nini hasa?
Kumbuka hawa ni vijana wa mtaani na ni haki yao! Hata wewe umetoka shamba hivyo sote ni washamba maana wa mjini ni watoto wa wenye ukoma wanaozaliwa mjini. Hii inaonesha jinsi Magufuli na sera zake anavyopendwa mitaani ingawa wapuuzi wa JF wanaona hapendwi
 
Noma sana!

Wengine waloandamana nimewaona wamebeba mabango ya sijui kwamba sisi tuliwasaidia hao Wasauzi enzi wakipigania haki zao.

Kwa hiyo kama tuliwasaidia, huo msaada unahusiana nini na tatizo lililopo?

Tumezidi ushamba.
Yaani kwa aibu niliyonayo sasa hivi, hata nikisafiri nje natamani nisijitambilishe uraia wangu. Kwa ushamba huu! We acha tu.
 
Kila siku wapinzani wakitaka kuandamana si kuonyesha kutotengewa haki si huwa mnaponda? Je ni kipi kinawafanya muone maandamano haya ni sawa? Nadhani sasa mmeona madhara ya kushabikia hujuma.
Mtu anayemshabikia TL ni mufilisi, huwezi kuwa unajielewa ukajadiliana naye Pole
 
K
Deni la miaka 37, umesema.

Kwa nini halijalipwa miaka yote hiyo?
Kunaweza kuwa na sababu mbalimbali zilizosababisha kushindwa kulipa deni kwa wakati,tuna madeni mengi tu kama nchi,si hilo tu la huyo mkulima wa kizungu, but kuzuia ndege sidhani kama ni sahihi,labda tu kama sheria za huko south zinaruhusu kukamata mali za mdaiwa,hii sio poa.
 
We are small minded.

Tunawaza tu today.. and within limited boundaries.

Yaani tunawaza mtaa wa pili.... hatuwazi boundaries beyond Ilala Temeke na Ilala

So tunakimbilia media in local dialect yelling over shit we don't understand ourselves.

Usenge tu.
 

Ushawahi kuchukua mkopo wa mortgage au mkopo wa kununulia gari?
 

Wewe....watch that potty mouth. I'll wash it with hydrogen peroxide. 😀
 
Ushawahi kuchukua mkopo wa mortgage au mkopo wa kununulia gari?
Hapana. Nadhani sheria za mikopo ni tofauti na ishu ya huyu mzungu,huyu mzungu hatukumkopa,tulimtaifisha .kwahiyo nadhani haiwezi kutumika sheria ya hiyo mikopo ya mortgage.
 
You are right, watz tumekuwa very very PRIMITIVE, yaani watu wanaadama bila hata kuelewa kwa nini ndege imesikiliwa, hii ndege haitaachiliwa mpaka tz ilipe ile deni ya pounds 33m ambazo yule mkulima anadai tz, hata watu waadamane aje, wavue nguo mpaka suruali, wavuje ubalozi au waamurise ubalozi ufungwa NGO ndege haitaachiliwa mpaka deni ilipwe PERIOD, niliona hao watz wenzetu wanatutia aibu kubwa sana mbele ya macho ya dunia, lakini ni ukosefu wa elimu bora miongoni wa watz wengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…