Tumewekwa njia panda

Mlisoma Uzi humu una kwenda kwa jina LA utata kifo cha Dr Omar? Mule kuna code iko inahusu tuko hili LA EL kwenda ikulu
 
Mshana Jr, umeandika vizuri mno. All in all, Lowasa kuja CDM kwa watu, wenye akili , philosophical ones, tulijua kuwa huyu mtu ana mapungufu mengi tu kuwa Rais, ila kwa wakati ule ilikuwa inalipa kupata wabunge wengi. Na hilo lilifanikiwa. Alikuwa na wafuasi wengi sana, usingeliweza kumwacha mtu kama huyo. Kwa siasa za ujima kama za kwetu, maamuzi ya kumchukua yalikuwa muafaka.
Na kama isingelikuwa huu udikiteita/dictator kutawala, bado Lowasa angeliendelea kuwa na nafasi ya kuimarisha CDM. Haya yanayotokea, kwa nchi zinazotawaliwa na madikiteita ndivyo athali zake, haya yalitokea Uganda also wakati wa Idd amin. Tuliokuwa huko tuliyashuhudia.
Na bado, mikutano ya siasa ikiruhusiwa CDM ikaongea na wananchi, Lowasa will be nothing! na kurudi kwake CCM
 
CCM na CDM ni pande mbili tofauti za nyoka mmoja.... Upande wowote utakaoushika bado utakua umeshika nyoka... Tatizo ni kuwa kuna upande ukiushika lazima ungatwe...!
 
Hi yo kesho ikiwa tofauti utasema nini
Mwananke anapobeba mimba hutegemea kuzaa mtoto mzuri asiye na kasoro na mara zote ni aidha wa kike au wa kiume ama mapacha wa jinsia mbili tofauti au zinazofanana... Hii huwa furaha ya wazazi ndugu na jamaa
Lakini si mara zote matokeo huja kama matarajio ya wazazi.. Sometimes kuna vifo ama kuzaa mlemavu... Matokeo yakiwa na tofauti hii utafanya nini? Tafakari!
 
Mshana, likelihood ya kuwa tofauti ni ndogo. Kitendo cha kwenda huko KINYEMELA bila kumfahamisha mwenyekiti wake, kina uhaini mkubwa sana. Walikuwa pamoja kumwona Kingunge, waliongea sana, walijadiliana. Kwa nini alimficha ziara kama hiyo ambayo ni sensitive. Let him go, na Magufuli alivyo, atampa hata cheo kikubwa kuukomoa upinzani. Kuna mtu amesema kuwa agenda kubwa ya Magufuli ni kupambana na wapinzania/upinzani, KUUA UPINZANI/WAPINZANI. Yuko tayari kufanya LOLOTE, NASEMA LOLOTE, kuona upinzani unaumia.
 
Kwenye soka huwa tunasajili mchezaji, anaweza kuwa nyota ama sio!

Tunaposajili mchezaji mpya huwa tunaamini kuna vitu anakuja navyo, kocha aliviona na pengine mashabiki pia tuliviona! Sio mara zote shabiki wanaona kile alichoona kocha!

Mchezaji mhamiaji ana options mbili. Ima acheze kwa mfumo wake aliokuja nao, acheze kwa mfumo mpya atakaoukuta!

Yote mawili haya yanalala katika mbinu, ujuzi na maarifa ya kocha. Kocha lazima ajue jinsi ya "kumuintegrate" mchezaji huyu ktk mfumo wake ikibidi kwa kutumia experience za mchezaji huyu alizotoka nazo huko alikotoka!

Kuna baadhi ya sajiri zinalipa na kuibeba timu, zingine zinashindwa kufikia matarajio yaliotarajiwa na wengi ktk mashabiki! Na hapa ndio kwenye matatizo! Mashabiki hawakubali kujiangalia wao na mapungufu ya timu yao kabla ya usajili wa "striker" wao! Wakijitahidi kidogo wataishia kumlaumu kocha kwa usajili usiozaa matunda! Kocha hatalaumiwa kwa kushindwa "kumuintegrate" mchezaji huyu ktk mfumo wa timu!

Yote kwa yote, mashabiki tuna namna yetu ya kujifariji. Huwa tunasema "Hakuna Mchezaji mkubwa kuzidi timu!" Na huwa tunaenda mbali zaidi na Kusema "timu ilikuwepo, ipo na itakuwepo!" Na kufikia hapo napo, mashabiki haiwahusu kuwa ubingwa ushapotea kwa mara nyingine tena!
 
Wana JF kumbukeni hili ...'ukicha mipango ya pamoja km kikundi/chama ,muhimu kuwa na mipango yako binafsi' Ahsanteni
 
ccm ni cancer kwa taifa.
 
Sisi tutaendelea kupiga deki, ulipo tupo!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…