Tumeshahamia Dodoma lakini...

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,275
12,568
Wazo la taifa kuhamishia shughuli zake Dodoma ni la siku nyingi tangu serikali ya awamu ya kwanza. Sababu kubwa ya kuhamia tuliyoelezwa ni kuwa Dodoma ni katikati ya nchi, hivyo Watanzania wengi ingewawia rahisi kufika Dodoma na kuhudumiwa kwa haraka.

Wakati wazo hili linatolewa miaka hiyo kulikuwa na maendeleo hafifu sana ya mawasiliano na usafiri kama ilivyo leo. Hivyo watu walihitaji kusafiri hadi makao makuu ya Wizara ili kupata huduma.

Kutokana na maendeleo ya njia za kupeana habari kama vile simu, internet, computer, redio, television, teleconference, ndege, reli na barabara za kisasa yalivyo sasa huenda sababu na gharama za kuhamishia makao makuu Dodoma ni ghali sana kuliko kuimarisha mifumo ya kidigitali hadi vijijini ili wananchi wahudumiwe hukohuko wakiwa mikoani, wilayani, tarafani, katani na vijijini kuliko kusafiri kwenda hadi Dodoma.

Huenda fedha za kukamilisha zoezi hili zingetosha kabisa kuimairisha miundombinu ya e-government (umeme, internet) nchi nzima hadi kwenye wilaya na vitongoji na kuondoa kabisa ulazima wa watu kusafiri hadi makao makuu ya Wizara Dodoma na kujikita zaidi kwenye zile activities zinazohusika moja kwa moja na kuongeza uchumi.

Je, wewe unaonaje, tuendelee na mpango huu wa kuwatayarisha watu kwenda Dodoma kuhudumiwa au tuimarishe e-government ili watu wahudumiwe bila kulazimika kwenda makao makuu ya wizara?
 
Haya Ndugu Zangu Nimekuja Hapa Kigamboni Kufanya Ziara Ya Kikazi. Mjue Dar es salaam Kwasasa Ni Mkoa Kama Mikoa Mingine. 😄😅😃😂😁

Nakumbuka Mtu Anakwenda Nyumba Za Kulala Wageni
Kwenye Daftari Anaandika
Unatoka Dar es salaam, Unakokwenda Dar es salaam 🙄😏😐😶🤨😑
 
Kila Mtanzania anauliza kwa nini mzee baba haendi kuishi dodoma?
 
Vyote ulivyovitaja (umeme, internet n.k) vinaenda kwa kasi zaidi kuzidi huo uhamisho. Hivyo nadhani maamuzi ya kuhamia hayajaathili kitu, wacha tuhamie maana Dodoma nako ni kwetu hatujatoka nje ya Tz.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuhamia Dodoma lilikuwa wazo la 1970s kutokana na hali ilivyokuwa kipindo hicho. Hiki ni kile cha Posta na Simu kwelikweli, kipindi cha usafiri wa treni, mabasi ya Leyland CD, kuandika barua na kutuma pesa kwa telegram, kuchapa kwa typewriter. Hivyo kuhamia katikati ya nchi lilikiwa wazo mujarabu kabisa. Lakini leo hii wazo kama lile ni zilipendwa kutokana na dunia kugeukia sera za kiuchumi zaidi kuliko siasa na maendeleo ya kidigitali
 
Wakati dunia inaendekea kuwa kijiji kimoja sisi tunawaza kinyume chake. Ninawaza tu namna nguvu zetu hizi za kuhamia Dodoma tungezitumia kwenye eneo lingine la kimkakati
 
Ndo tushahamia hivyo, kingine?
Historia na vizazi vyetu vitakuja kusema kuhusu sisi kwenye hili. Wazo lilikuwa sahihi enzi zile za mwalimu lakini sio sasa.

Nadhani tuishie hapo tulipokwishafika kutekeleza wazo la mzee wetu la 70s, chenchi iliyobaki tuiwekeze kwenye kasi ya ujenzi wa miundombinu ya umeme na internet ya uhakika, elimu, na usafiri wa haraka na rahisi nchi nzima na kuzitawanya Wizara kulingana na geografia yetu. Mfano, Wizara ya madini ijengwe Mwanza, Wizara ya kilimo ijengwe Morogoro, Wizara ya utalii ijengwe Arusha, Wizara ya elimu Dar es Salaam, nk na teleconferencing itumike kuendesha vikao mbalimbali kama ikibidi badala ya kukusanyika wote kwenye ukumbi mmoja na kueneza Corona (CoViD)
 
Tumehamia kiakili ila kimoyo tupo DARISALAAMA.ikulu tuliyoambiwa itakuwa jumba la MAONESHO mkubwa analeta wanyama pori kupaimarishaaa.kalagabaho, kwamba anahamisha Makao kwenda dodoma kwa kujenga ofisi za serikali tuuu.

Bila kuimarisha huduma za kijamii kama shule, makanisa,misikiti, masoko nk.ni akili za mpumbavu kama mwenyekiti tuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
De

Mawazo chany haya. Wizara kuwekwa kikanda itaweza kuongeza ufanisi zaidi
Sio Wizara zooooote kuwekwa kwenye mji mmoja. KWANI kama itatokea shida kama CORONA kwenye huo mji basi tabu itakuwa kubwa sana, lakini watu wote kwenda kwenye mji mmoja kupata huduma nako ni kurudia makosa tuliyoyafanya Dar es Salaam tulipoziweka huduma zote City centre
 
Dar tamu bwashee!!Huna jinsi karibu Dom na nadhani msongo wa mawazo umeisha.Hamishia mkeo huko Dom uta-enjoy.Usije ukabebwa na wagogo wa Mvumi na mkeo akaganda kwa muuza genge pale soko la urafiki.

Hahahahaha!!
Kuhamia Dodoma lilikuwa wazo la 1970s kutokana na hali ilivyokuwa kipindo hicho. Hiki ni kile cha Posta na Simu kwelikweli, kipindi cha usafiri wa treni, mabasi ya Leyland CD, kuandika barua na kutuma pesa kwa telegram, kuchapa kwa typewriter. Hivyo kuhamia katikati ya nchi lilikiwa wazo mujarabu kabisa. Lakini leo hii wazo kama lile ni zilipendwa kutokana na dunia kugeukia sera za kiuchumi zaidi kuliko siasa na maendeleo ya kidigitali
 
Back
Top Bottom