Tumefikaje hapa tulipo?

Tumefikaje hapa tulipo?

Hii siyo mbinu mpya hata kidogo kwa watu wa mlengo wako.
Sina tatizo kabisa na hilo kwa sababu siogopi kulizungumzia. Watu ninaowasema juu ya imani yao ni kundi la aina yenu, mnaojifichaficha, au mnakuwa wawazi kwama walevi kwa imani. Unapojipambanua kuwa kundi la aina hiyo, sina tatizo lolote la kukujadili; kwa sababu maslahi yenu ni kinyume na maslahi ya waTanazia wanaotaka mshikamano baina yao bila ya kujali imani zao.

Kwa hiyo usiwe na shaka, ukiwa upande wa ulevi wa imani, nitakujadili tu, bila ya hofu ya kusemwa juu ya kuchambua watu.
Hata mimi sina tatizo na watu kama nyie mnaopenda kuzungumzia WATU. Mimi nimekuwa issue yako wewe, while mimi nazungumzia Events na Idea. Hatufanani. Niseme utakavyo hainibadilishi wala haiweki mkate mezani kwangu, Uwe na siku njema..
 
Kifupi Mkuu wewe unamkubali Tundu Lissu kwa sababu zako nami nilimkubali Magufuli kwa sababu alifanya exactly Chadema walivyojitangaza kabla ya Uchaguzi wa 2010 - 2015 baada ya kuona nchi hii haitawaliki pasipo kumpata rais DIKTETA. Rais anayeweza kufanya maamuzi magumu na sera zikaandaliwa ambazo Magufuli alizifuata.

Ukiniuliza kama Udikteta ule ulikuwa mzuri nitasema YES! na watu kama Shangazi na Tundu Lissu ambao hata baada ya rais kutangaza hali ya Vita vya Kiuchumi wao wakawa upande wa maadui sikupenda kabisa utove wa Uzalendo kiasi kile.

Na bahati mbaya sana kwao nilikuwa nawajua vizuri kiasi kwamba sikuweza kubadilisha msimamo wangu.

Anyway tuache kuzungumzia hisia zetu maana haziwasaidii Watanzania katika adha tuliyopo. Kama sikosei tulionana Ohio 2008 kwenye Old Skools..am I right?

Maasalaam
Hakijabadilika kitu, mkuu 'Mkandara'!
Tuyaachie hapa yabaki yalivyo kati yetu.
Lakini nililo hakika nalo, mabadiliko makubwa hayazuiliki tena Tanzania.
 
Hata mimi sina tatizo na watu kama nyie mnaopenda kuzungumzia WATU. Mimi nimekuwa issue yako wewe, while mimi nazungumzia Events na Idea. Hatufanani. Niseme utakavyo hainibadilishi wala haiweki mkate mezani kwangu, Uwe na siku njema..
Hakuna kilichoharibika, maadam tumeelezana na kuelewana.
 
Mjomba ulichoshauri hapo mwishoni hakitekelezeki. Mimi natamani kuona muungano unavunjika ili na sisi Watanganyika tujivunie uwepo wa nchi yetu ya Tanganyika, kama wafanyavyo Wazanzibari kwa Zanzibar yao. Kwa kufanya hivi nchi yetu haitokuja kutawaliwa tena na vilaza, mafisadi, wahuni, au watu wasio na chembe ya uzalendo.
Mtanganyika Magufuli ndio alianzisha huu ushenzi wa kuiba chaguzi nchi nzima, kuteka na kuua wapinzani,huyu mnywa damu wa sasa kaanza kuwageukia wenzake, Nyerere aliongelea haya mambo pamoja na ukabila,solution sio Tanganyika ni katiba mpya ambayo itafanya huu ushenzi unaoendelea impossible
 
Utovu kama huu, .hata mimi nakuvunja miguu tuu 😂😂😂
 
Leo hii nimechukua zaidi ya masaa manne kuwasikiliza viongozi wastaafu, maprofesa na wadau mbali mbali katika mdahalo uloandaliwa na TLS.

Hakika nimejifunza mengi na yanilazimu kuwashukuru sana Mzee wetu Jaji Warioba, Profesa Shivji, Mwanasheria kutoka Kenya, Profesa Tibaijika, viongozi wa vyama vya Siasa na taasisi nyinginezo hususani TLS wenyewe. Wote kwa ujumla wao wamezungumzia mambo muhimu kwa mustakabali wa Taifa letu.

Pamoja na yote yale wameniachia maswali magumu zaidi nimekaa na kujiuliza hivi tatizo hasa lipo wapi? Na tumefika hapa kwa sababu gani?

Kubwa zaidi lilojitokeza kwangu linatokana na hotuba ya Profesa Shivji alipozungumzia Misingi mikuu ya Demokrasia akifafanua juu ya pande mbili yaani upande Wananchi na upande wa Utawala. Na kilichojitokeza wazi kwangu ni Kupotea thamani na heshima ya UTU wetu. UTU ndio kiashiria cha ujenzi na usimamizi wa Uhuru na Usalama.

Taifa letu limepoteza UTU kiasi kwamba Utawala hauthamini wala kuheshimu Wananchi na Wananchi hawawathamini wala kuheshimu Viongozi wake. Haiishi hapo, tumefikia kiasi kwamba Utawala hauheshimu viongozi wenzao na Wananchi hawathamini wala kuheshimu Wananchi wenzao.

Na katika hali hii, Uhuru na Usalama wa wananchi upo hatarini kama ilivyo kwa viongozi wenyewe hawaaminiani wala hawaheshimiani isipokuwa kwa yule mwenye nguvu ya utawala na fedha, hii ndio Tanzania ya leo (status quo)

Swali linakuja tumefikaje hapa? Naamini kila mtu ana mtazamo wake lakini binafsi yangu akili yangu inanambia yote haya yametokana utovu wa nidhamu katika miiko na maadili ya UTU wetu kwa kuiga mifumo ya kigeni ambayo ilidhalilisha mila na tamaduni zetu kama ni misingi ya kale (primitive) ilopitwa na wakati.

Mifumo ya Demokrasia tuloichukua ndio chanzo cha kuharibika kwa misingi ya Demokrasia kupitia mabadiliko ya Katiba ya mwaka 1984 na 1992 upande wa Jamhuri pia Uandishi wa Katiba ya Zanzibar mwaka 1984 na mabadiliko yalofuatia mwaka 2002. Isipokuwa nitaacha pembeni Katiba ya Zanzibar, hii inahitaji mada nyingine tofauti kabisa.

Najua hoja yangu inahitaji mjadala mpana zaidi lakini niseme kwamba mabadiliko haya ndio mwanzo wa matatizo yote yanayofuatia katika miongo tofauti ya Kiutawala kufikia leo hii.

Katika makosa makubwa yalofanyika ni kuondolewa kwa Miiko na Maadili ya Viongozi hivyo kupoteza Sifa zinazotakiwa za viongozi wetu Kitaifa. Kwa nafasi walizokuwa nazo viongozi serikalini, Wabunge na hata majaji wakaanza kumiliki utajiri pasi kuulizwa wamepataje mali na utajiri huo, hii njia panda ndio ikawa mwanzo wa mmomonyoko wa maadili na chachu ya rushwa kuzaliwa.

Jambo la pili lilikuwa ujio mfumo wa Vyama Vingi ambavyo havikuzingatia misingi ya Demokrasia ( Uhuru, Utu na Usalama) bali ilikuwa ni tiketi ya jicho la Uheshimiwa na kuingia Ikulu kutawala (mfumo wa Vyama vingi). Vyama vingi ndivyo viloweka nadharia ya kina nani watakuwa Waheshimiwa kati ya Wananchi wote na hii ikazaa tamaa ya utukufu wa nyadhifa hizo. Hakuna Chama hata kimoja kinachosimamia itikadi na Sera zake wakati wote ila kulingana na fursa zinazojitokeza.

Katika mukhtadha huo tulipoteza Siasa safi za vyama Kiitakadi, hasada ikachukua nafasi baina ya vyama vya Siasa, viongozi kwa viongozi, Wananchi na vyama pinzani na kibaya zaidi rushwa na upendeleo vikatumiwa kama zana katika teuzi toka chaguzi za ndani ya Vyama vya Kisiasa hadi Viongozi wa Kitaifa – Yakaibuka makundi ya timu za Wana, hasada ikazaa Chuki na Uadui matokeo yake UZALENDO kwa Taifa letu UKAPUKUTIKA.

Kwa hiyo tukiacha hoja ya Katiba Mpya pembeni, sisi Watanzania tuna wivu na chuki za kuhasimiana wenyewe kwa sababu ya fursa za madaraka na utajiri zimeletwa kupitia vyama vingi.

Viongozi waliopo madarakani hujiona wapo katika nafasi adimu sana ya Utajiri wa hadhi na mali na wanajua kuna macho ya wivu dhidi yao hata kama wanayofanya nia njema ama kinyume cha misingi ya demokrasia, bado utachikiwa tu. Siasa zetu zimekuwa ni za Ukinzani ambazo kiitikadi hazifanani kabisa na Upinzani kwa nia, dhamira na malengo ya Demokrasia.

Tujiulize wenyewe mpaka hapa tumefika ni viongozi wangapi wameuawa kwa ajali, risasi au sumu na hakuna watu walotiwa hatiani wala kuchukuliwa hatua. Nini hasa sababu za viongozi hao kuuawa? Bila shaka ni kunatokana na UADUI wa kisiasa walojenga dhidi ya kiongozi ama viongozi wengine iwe kwa nia safi au mbaya.

Wivu na Chuki sii lazima vitumike kwa wale washindani tu bali inaweza toka chini kwa wale wanaotaka kufika pale kiongozi alipofika ama kiongozi kulinda maslahi yake dhidi ya wale wanaotaka nafasi yake.

Kwa hiyo tunapozungumzia leo Maombolezi, Maridhiano na sijui Katiba Mpya ni muhimu kwanza sisi wenyewe tukubali mapungufu yetu kimaadili ili TUBADILIKE - Heshima ya Utu wetu na Uzalendo kwa Taifa ni utamaduni ulopitwa na wakati.

Hatuwezi fanya maombolezi ambayo baadhi yetu hawaoni umuhimu wala sababu. Hatuwezi fanya Maridhiano kwa kuwekeana masharti yasiyojali Utu wetu na Uzalendo kwa Taifa hili bali maslahi ya mtu au chama.

Mwisho hatuwezi kuwa na Katiba mpya inayotokana na maoni ya Wananchi wenye wivu, chuki na uadui isipokuwa Katiba lazima iwe ni mwongozo wa Wananchi hao bila kujali tofauti zao - Katiba ni ya Wananchi iheshimiwe na wote.

Maasalaam

Nashangaa umeandika yote hayo, lakini haujagusia yaliyotokea October 29. Hauoni kuwa hiyo ni moja ya sababu iliyoligawa taifa?
 
Kwa hiyo wewe kujitoa kwa wadau wa UKAWA na taasisi nyingine unaamini Katiba ile Pendekezwa ndio ilipata maamuzi halali kabisa ya Bunge lile?

Umewahi wasikia Mzee Warioba na hata Polepole wakizungumzia Katiba Pendekezwa! Umewahi wasikia Wananchi wakizungumzia Katiba Pendekezwa dhidi ya Rasimu ya Katiba? Mimi naamini Bunge lile halikufikia muafaka na hata jana Prof. Tibaijuka kazungumzia.

Yawezekana mimi nina mitazamo tofauti sana na watu wengi hapa na hainishangazi kwa sababu hata zamani nilipokuwa hapa nilipitia Upinzani mkubwa kwa sababu watu wanazumgumza hoja zao kwa hisia za UCHAMA ilihali mimi natazama Uhalisia.
Nasisitiza acha upotoshaji, bunge lile lilikwenda hadi mwisho japo kuna waliosusia. Na katiba pendekezwa ilikuwa unasubiri kura ya maoni, ni bahati tu Magufuli aliigomea, na hakuigomea kwasababu wapinzani walitoka, bali alitaka atawale kwa katiba hii hii ambayo rais ni Mungu mtu. Kwa taarifa yako Magufuli angetaka kura ya maoni ingepigwa, na ingepita kwa matakwa ya serekali, na sio lazima wananchi. Hakuna mtu anayekupinga boss, bali ninakutaka uache upotoshaji.

Kama unaongelea uhalisia ni huu niliokumbia, na sio kutaka kujifichia kwenye hisia za uvyama wala nini.
 
Kifupi Mkuu wewe unamkubali Tundu Lissu kwa sababu zako nami nilimkubali Magufuli kwa sababu alifanya exactly Chadema walivyojitangaza kabla ya Uchaguzi wa 2010 - 2015 baada ya kuona nchi hii haitawaliki pasipo kumpata rais DIKTETA. Rais anayeweza kufanya maamuzi magumu na sera zikaandaliwa ambazo Magufuli alizifuata.

Ukiniuliza kama Udikteta ule ulikuwa mzuri nitasema YES! na watu kama Shangazi na Tundu Lissu ambao hata baada ya rais kutangaza hali ya Vita vya Kiuchumi wao wakawa upande wa maadui sikupenda kabisa utovu wa Uzalendo kufikia kiasi kile.

Na bahati mbaya sana kwao nilikuwa nawajua vizuri kiasi kwamba sikuweza kubadilisha msimamo wangu.

Anyway tuache kuzungumzia hisia zetu maana haziwasaidii Watanzania katika adha tuliyopo. Kama sikosei tulionana Ohio 2008 kwenye Old Skools..am I right?

Maasalaam
Umerukaruka kujificha weee! Mwisho umejiweka hadharani. Hongera kwa Kalamu kumfichua huyu mnafiki.

Umeshindwa kujibu vipi kuhusu Samia?
 
Hili la "wafuasi wa CCM" tuwe wakweli wenyewe.
Ni wafuasi gani hawa wa CCM wanaokubali viongozi wao wanayoyafanya sasa. Hao wafuasi wa CCM kweli wapo; au na wao wamelazimishwa kama sisi sote tunavyolazimishwa kukubali haya yanayoendelea.

Wewe, mkuu 'Drifter' hata kweli hukuona hata uteuzi tu wa watia nia ndani ya chama, hadi ngazi ya Rais ilivyovurugwa maksudi, kuwanyima ushiriki hao hao wafuasi wa CCM?

Ni hoja yangu kwamba tunawahusisha tu kwa makosa hao wafuasi wa CCM na hili kundi ambalo limeamua kukitumia chama (jina) vibaya.
Mkuu wewe unachoongea hapa ni matokeo tu. Ni consequences za mfumo mbovu uliowezesha utawala wa ovyo kukamata uRais wa JMT na kuutumia kufanya mambo ya ovyo sana. Hilo kundi baya halikuzuka tu. Kwa miaka mingi CCM imetengeneza na kulea mazingira yanayowezesha watu wa ovyo kushika madaraka ya nchi. Wote tunatakiwa kupambana kuondoa hayo mazingira ya ovyo. Shida kubwa ni watumainia fursa na wajinga (ignorants) wengi waliojazana kwenye ufuasi wa CCM ngazi zote.

JF ni kielelezo kikubwa. Mifano kadhaa. Kuna wadau hapa waliunga mkono sana hatua za utawala wa 5 za kubana uhuru wa shughuli za kisiasa kwa vyama vya upinzani, uhuru wa vyombo vya habari na utoaji maoni, kinyume cha kkatiba na sheria na kutumia vitisho na hit squads (watu wasiojulikana) kutishia, kutesa na kuua wakosoaji wakidai ni "wasaliti" na "wahaini". Walifumbia macho hujuma kubwa iliyofanywa kwenye chaguzi za 2019 na 2020. Leo hii watu hao hao wanaulaani sana utawala wa awamu ya sita kwa kukithiri zaidi katika mambo ya aina ile ile. Kama vile ni kitu kipya na cha kushangaza sana kwao.

Wengi hawaoni tatizo la msingi ndani ya CCM. Bali wanajiaminisha na kutaka kutuaminisha kuwa tatizo kubwa ni uongozi wa awamu hii TU na kumlaani Mabeyo kwa kazi aliyofanya kumwezesha Rais aliyepo kuingia madarakani. Wamesahau kwamba ni wao waliokuwa wakiunga mkono uamuzi wa awamu ya tano kuhusu kupuuzia marekebisho ya katiba na kuminya mifumo na michakato yote ya kidemokrasia. Hata huku mitaani tunawasikia sana. Wanalaani kweli kweli utawala uliopo lakini hawaoni kabisa uozo wa tawala zilizopita. Wanataka tuamini kuwa kabla ya sasa mambo yalikuwa mazuri.

Kuna wengi leo hii ikitokea Rais wa awamu hii akaondoka madarakani (kwa namna yoyote ile) halafu mmoja wa inner circle ya awamu iliyopita akachukua nafasi yake, hawatakuwa na tatizo tena. Hata madai ya kutaka mabadiliko ya katiba na mfumo wa uongozi wa nchi hayatakuwa kipaumbele chao tena. That's really troubling.

This is a systemic problem. Everyone should see it as such. Lakini ni tatizo ambalo limekwamishwa muda mrefu sana na wasaka fursa (opportunists) waliojazana ndani ya CCM na uelewa mdogo wa wananchi wengi.
 
Nashangaa umeandika yote hayo, lakini haujagusia yaliyotokea October 29. Hauoni kuwa hiyo ni moja ya sababu iliyoligawa taifa?
Ukinisoma vizuri ya October 29 ni matokeo Utovu wa UTU na UZALENDO kwa Taifa.
 
Shukran, it goes like this-
Tuna MFUMO mbovu wa Demokrasia Usiozingatia MISINGi ya Demokrasia.
 
Mjomba ulichoshauri hapo mwishoni hakitekelezeki. Mimi natamani kuona muungano unavunjika ili na sisi Watanganyika tujivunie uwepo wa nchi yetu ya Tanganyika, kama wafanyavyo Wazanzibari kwa Zanzibar yao. Kwa kufanya hivi nchi yetu haitokuja kutawaliwa tena na vilaza, mafisadi, wahuni, au watu wasio na chembe ya uzalendo.
100%✔️
 
Leo hii nimechukua zaidi ya masaa manne kuwasikiliza viongozi wastaafu, maprofesa na wadau mbali mbali katika mdahalo uloandaliwa na TLS.

Hakika nimejifunza mengi na yanilazimu kuwashukuru sana Mzee wetu Jaji Warioba, Profesa Shivji, Mwanasheria kutoka Kenya, Profesa Tibaijika, viongozi wa vyama vya Siasa na taasisi nyinginezo hususani TLS wenyewe. Wote kwa ujumla wao wamezungumzia mambo muhimu kwa mustakabali wa Taifa letu.

Pamoja na yote yale wameniachia maswali magumu zaidi nimekaa na kujiuliza hivi tatizo hasa lipo wapi? Na tumefika hapa kwa sababu gani?

Kubwa zaidi lilojitokeza kwangu linatokana na hotuba ya Profesa Shivji alipozungumzia Misingi mikuu ya Demokrasia akifafanua juu ya pande mbili yaani upande Wananchi na upande wa Utawala. Na kilichojitokeza wazi kwangu ni Kupotea thamani na heshima ya UTU wetu. UTU ndio kiashiria cha ujenzi na usimamizi wa Uhuru na Usalama.

Taifa letu limepoteza UTU kiasi kwamba Utawala hauthamini wala kuheshimu Wananchi na Wananchi hawawathamini wala kuheshimu Viongozi wake. Haiishi hapo, tumefikia kiasi kwamba Utawala hauheshimu viongozi wenzao na Wananchi hawathamini wala kuheshimu Wananchi wenzao.

Na katika hali hii, Uhuru na Usalama wa wananchi upo hatarini kama ilivyo kwa viongozi wenyewe hawaaminiani wala hawaheshimiani isipokuwa kwa yule mwenye nguvu ya utawala na fedha, hii ndio Tanzania ya leo (status quo)

Swali linakuja tumefikaje hapa? Naamini kila mtu ana mtazamo wake lakini binafsi yangu akili yangu inanambia yote haya yametokana utovu wa nidhamu katika miiko na maadili ya UTU wetu kwa kuiga mifumo ya kigeni ambayo ilidhalilisha mila na tamaduni zetu kama ni misingi ya kale (primitive) ilopitwa na wakati.

Mifumo ya Demokrasia tuloichukua ndio chanzo cha kuharibika kwa misingi ya Demokrasia kupitia mabadiliko ya Katiba ya mwaka 1984 na 1992 upande wa Jamhuri pia Uandishi wa Katiba ya Zanzibar mwaka 1984 na mabadiliko yalofuatia mwaka 2002. Isipokuwa nitaacha pembeni Katiba ya Zanzibar, hii inahitaji mada nyingine tofauti kabisa.

Najua hoja yangu inahitaji mjadala mpana zaidi lakini niseme kwamba mabadiliko haya ndio mwanzo wa matatizo yote yanayofuatia katika miongo tofauti ya Kiutawala kufikia leo hii.

Katika makosa makubwa yalofanyika ni kuondolewa kwa Miiko na Maadili ya Viongozi hivyo kupoteza Sifa zinazotakiwa za viongozi wetu Kitaifa. Kwa nafasi walizokuwa nazo viongozi serikalini, Wabunge na hata majaji wakaanza kumiliki utajiri pasi kuulizwa wamepataje mali na utajiri huo, hii njia panda ndio ikawa mwanzo wa mmomonyoko wa maadili na chachu ya rushwa kuzaliwa.

Jambo la pili lilikuwa ujio mfumo wa Vyama Vingi ambavyo havikuzingatia misingi ya Demokrasia ( Uhuru, Utu na Usalama) bali ilikuwa ni tiketi ya jicho la Uheshimiwa na kuingia Ikulu kutawala (mfumo wa Vyama vingi). Vyama vingi ndivyo viloweka nadharia ya kina nani watakuwa Waheshimiwa kati ya Wananchi wote na hii ikazaa tamaa ya utukufu wa nyadhifa hizo. Hakuna Chama hata kimoja kinachosimamia itikadi na Sera zake wakati wote ila kulingana na fursa zinazojitokeza.

Katika mukhtadha huo tulipoteza Siasa safi za vyama Kiitakadi, hasada ikachukua nafasi baina ya vyama vya Siasa, viongozi kwa viongozi, Wananchi na vyama pinzani na kibaya zaidi rushwa na upendeleo vikatumiwa kama zana katika teuzi toka chaguzi za ndani ya Vyama vya Kisiasa hadi Viongozi wa Kitaifa – Yakaibuka makundi ya timu za Wana, hasada ikazaa Chuki na Uadui matokeo yake UZALENDO kwa Taifa letu UKAPUKUTIKA.

Kwa hiyo tukiacha hoja ya Katiba Mpya pembeni, sisi Watanzania tuna wivu na chuki za kuhasimiana wenyewe kwa sababu ya fursa za madaraka na utajiri zimeletwa kupitia vyama vingi.

Viongozi waliopo madarakani hujiona wapo katika nafasi adimu sana ya Utajiri wa hadhi na mali na wanajua kuna macho ya wivu dhidi yao hata kama wanayofanya nia njema ama kinyume cha misingi ya demokrasia, bado utachikiwa tu. Siasa zetu zimekuwa ni za Ukinzani ambazo kiitikadi hazifanani kabisa na Upinzani kwa nia, dhamira na malengo ya Demokrasia.

Tujiulize wenyewe mpaka hapa tumefika ni viongozi wangapi wameuawa kwa ajali, risasi au sumu na hakuna watu walotiwa hatiani wala kuchukuliwa hatua. Nini hasa sababu za viongozi hao kuuawa? Bila shaka ni kunatokana na UADUI wa kisiasa walojenga dhidi ya kiongozi ama viongozi wengine iwe kwa nia safi au mbaya.

Wivu na Chuki sii lazima vitumike kwa wale washindani tu bali inaweza toka chini kwa wale wanaotaka kufika pale kiongozi alipofika ama kiongozi kulinda maslahi yake dhidi ya wale wanaotaka nafasi yake.

Kwa hiyo tunapozungumzia leo Maombolezi, Maridhiano na sijui Katiba Mpya ni muhimu kwanza sisi wenyewe tukubali mapungufu yetu kimaadili ili TUBADILIKE - Heshima ya Utu wetu na Uzalendo kwa Taifa ni utamaduni ulopitwa na wakati.

Hatuwezi fanya maombolezi ambayo baadhi yetu hawaoni umuhimu wala sababu. Hatuwezi fanya Maridhiano kwa kuwekeana masharti yasiyojali Utu wetu na Uzalendo kwa Taifa hili bali maslahi ya mtu au chama.

Mwisho hatuwezi kuwa na Katiba mpya inayotokana na maoni ya Wananchi wenye wivu, chuki na uadui isipokuwa Katiba lazima iwe ni mwongozo wa Wananchi hao bila kujali tofauti zao - Katiba ni ya Wananchi iheshimiwe na wote.

Maasalaam

Wakati wa kampeni tulikuwa tunasema CCM OYEEEEEEEE...MAMA anaupiga mwingi sana hadi unamwagika hadi Magari yetu tukaweka T 2030 SSH.

Hii tuliipenda wenyewe na bado Mama atetewe...leo mtasemaje tumefikaje????

CCM BABA LAO tukutane 2030
 
Mkuu wewe unachoongea hapa ni matokeo tu. Ni consequences za mfumo mbovu uliowezesha utawala wa ovyo kukamata uRais wa JMT na kuutumia kufanya mambo ya ovyo sana. Hilo kundi baya halikuzuka tu. Kwa miaka mingi CCM imetengeneza na kulea mazingira yanayowezesha watu wa ovyo kushika madaraka ya nchi. Wote tunatakiwa kupambana kuondoa hayo mazingira ya ovyo. Shida kubwa ni watumainia fursa na wajinga (ignorants) wengi waliojazana kwenye ufuasi wa CCM ngazi zote.
Sijui ni wapi tunaposigana mkuu 'Drifter'.
"Muundo mbaya ndani ya CCM", ambao ndio umetufikisha hapa leo uliwekwa nyakati zile kwa sababu maalum; za kuepuka yanayotokea leo. Badala yake, ukawa wa kudumu, na hao waliokuwa wadhibitiwe na muundo huo, sasa wamepata fursa ya kuutumia na kushika hatamu ya chama.

"...kulea mazingira yanayowezesha watu wa hovyo kushika madaraka ya nchi." Maneno mazito na sahihi kabisa yanayoendana na kauli zilizozoeleka ndani ya chama, kama :"Huyu ni Mwenzetu"; mwenzetu katika nini katika uongozi wa chama?

Imenilazimu jana kutumia muda kuangalia watu walioko kwenye Kamati Kuu ya Chama na Halmashauri ya Taifa (NEC) ya chama hicho!
Hawa siyo watu waliowekwa huko na hawa wanachama wa kawaida wa CCM tunaowahusisha sasa na ubovu wa chama chao. Na hivi ndio vyombo muhimu vinavyoamua maswala mazito ya chama, na hatimaye ya nchi nzima!

Kwa hiyo, kimsingi tunakubaliana kati yetu juu ya ubovu wa chama kutokana na mfumo mbaya unaowezesha kuingiza viongozi wabovu kwenye uongozi; na kwamba baadhi (kundi kubwa la wana CCM) wamo ndani ya chama kwa sababu tu za kimaslahi yanayotokana na kuwa mwanachama wa chama tawala.

Sehemu ambayo huenda bado kuna tofauti kubwa kati yangu na wewe ni upande wa uhusika wa wanachama wengi wa CCM kukubali matokeo ya uongozi wa chama kama yalivyo sasa.
Ni hoja yangu kwamba, pangetokea fursa ya kuwapa uhuru wa kueleza maoni yao juu ya chama chao leo hii, wengi wa wanachama hawa wasingetofautiana sana na sisi waTanzania wengine tusiokuwemo kwenye chama hicho
 
Mtanganyika Magufuli ndio alianzisha huu ushenzi wa kuiba chaguzi nchi nzima, kuteka na kuua wapinzani,huyu mnywa damu wa sasa kaanza kuwageukia wenzake, Nyerere aliongelea haya mambo pamoja na ukabila,solution sio Tanganyika ni katiba mpya ambayo itafanya huu ushenzi unaoendelea impossible
Hakuna sababu ya uwepo wa Muungano tena. Nafikiri hili ndilo jambo la muhimu zaidi sasa hivi kuliko hata hiyo Katiba Mpya.
Tanganyika irudi, na watu waendelee na shughuli zao badala ya kupoteza muda na Muungano usiokuwa na faida yoyote.
 
Back
Top Bottom