KWANZA KABISA, wafuasi wa CCM watambue na kukubali kuwa chama chao ambacho ni chama dola kimeunda na kulea mfumo wa kiimla (authoritarian) ambao una kasoro za msingi zilizoleta madhara makubwa sana kwa taifa na wananchi kwa ujumla. Ni mfumo ambao umetumika kuongoza nchi hii tangu awamu ya kwanza. Muda wote huo umekuwa ukitegemea utashi wa mtu mmoja, Rais, na kundi lake (inner circle). Mtu mmoja katika kiti cha uRais wa JMT (na uenyekiti wa CCM) amekuwa na mamlaka yote juu la nchi na vyote vilivyomo absolute power.
Ni kukosa uelewa au hila kutaka kulinganisha CCM na vyama huru vya siasa.
Rais (wa CCM) akiwa mwema na mzalendo kwa nchi yake kama alivyokuwa JKN (Nyerere) - benevolent dictator - wananchi wanakuwa na amani na kushiriki shughuli za maendeleo kwa juhudi kubwa. Rais akiruhusu utawala wa sheria na uwazi kama awamu za pili, tatu na nne, angalau watu wanaongea, taasisi zinafanya kazi na taarifa muhimu zinasambaa kiasi chake. Rais akiamua kupuuza katiba, kupuuza utawala wa sheria, kuzuia uwazi na kutawala kwa hofu, vitisho, mateso, udhalilishaji, hata mauaji kwa kutumia vikundi vya mauaji (hit squads), nchi inaingia gizani, unafiki, uchawa, na ujinga (idiocy) vinatamalaki. Hizo ni awamu za 5 & 6.
Endapo, wafuasi wa CCM hawataona hayo kuhusu chama hicho na kukimbilia kujificha kwenye udini, muungano, jinsia, watu fulani fulani (individuals), CHADEMA, n.k., hakika safari itakuwa ndefu sana kuelekea kwenye ufumbuzi.