Tume ya Uchaguzi iwe na mfuko wake na fedha zake

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,016
9,885
Katika mkutano wa wadau wa demokrasia nchini ulioandaliwa na TCD. Joseph Selasini amesema Tume ya Uchaguzi iwe na fedha zake, iwe na watu wake na namna yake ya kuajiri badala ya kutegemea fedha kutoka hazina.

Aidha amesema suala la uchaguzi wa serikali za mtaa na uchaguzi mkuu ufanyike kwa siku moja ili kuepuka gharama.

Akizungumzia hoja hiyo, Maftaha kutoka CUF amesema suala la chaguzi kuwa moja au tofauti sio hoja, kinachotakiwa ni uchaguzi huru na haki. Kwa kuwa uchaguzi wa serikali za mtaa unasimamiwa na TAMISEMI.

Shida sio kuteua au kutoteuliwa, bali ni vyama kutokuwa na usawa.
 
Katiba ibadilishwe tupate katiba bora. Hili likifanyika kila kitu kutakuwa bora ikiwemo tume ya uchaguzi
 
Katika mkutano wa wadau wa demokrasia nchini ulioandaliwa na TCD. Joseph Selasini amesema Tume ya Uchaguzi iwe na fedha zake, iwe na watu wake na namna yake ya kuajiri badala ya kutegemea fedha kutoka hazina.

Aidha amesema suala la uchaguzi wa serikali za mtaa na uchaguzi mkuu ufanyike kwa siku moja ili kuepuka gharama.

Akizungumzia hoja hiyo, Maftaha kutoka CUF amesema suala la chaguzi kuwa moja au tofauti sio hoja, kinachotakiwa ni uchaguzi huru na haki. Kwa kuwa uchaguzi wa serikali za mtaa unasimamiwa na TAMISEMI.

Shida sio kuteua au kutoteuliwa, bali ni vyama kutokuwa na usawa.
Hizo fedha zake wanazitoa wapi?Mnataka wafanye biashara?
 
Nchi zingine zilizopiga hatua kiuchumi na kijamii. Na zilizo na democracy halisi wanafanyaJe ?!.

Pesa hata kama zitatoka hazina. Zisiwe chini ya wizara fulani na hisani ya serikali kuu. Zitungiwe sheria zake . Na tume iweze kuajiri kulingana na mahitaji yake. Siyo hii ya kuteuliwa na Rais na kuapishwa na Rais ambaye pia ni mgombea.

Ngazi ya halmashauri wakurugenzi ambao na wateule wa Rais na watumishi wa tamisemi wasihusike kabisa na chaguzi.
 
Back
Top Bottom