Teknolojia Ya AKILI BANDIA (AI) Inaweza KUIBA PASSWORD ZAKO

Eugen TZA

Member
Aug 7, 2023
61
98
Wahalifu wa kimtandao (Hackers) Inasemekana kuwa wamebuni mbinu mpya kupitia teknolojia ya akili bandia (AI) yenye uwezo wa kuiba nywila,(Password) za mtu kwenye simu au kompyuta kwa kusikiliza mlio wa Keyboard yako.
-
Watafiti kupitia chuo cha Cornell's University wameeleza kuwa kupitia teknolojia ya akili bandia wezi mtandao wanaweza kuiba password za mtu kwa mafanikio ya asilimia 95%, Modeli hiyo ina-focus na sauti inayotoka kwenye Keyboard tu.
-
Hii inamaanisha kuwa unaweza kuibiwa Password ukiwa Mubashara kupitia Zoom kama uta-type nywila yako kwa asilimia 93%, Katika mtandao wa Skype ni asilimia 91.7%, Na hii ni kwa Keyboard zote hata za kisasa, Hivi majuzi FBI walionya kuhusu uhalifu kufanyika kupitia ChatGPT.
-
Ikumbukwe kuwa jumuiya ya KIMATAIFA hivi karibuni walikutana kushauriana kuhusu namna bora ya ku-control teknolojia ya akili bandia (AI) kutokana na teknolojia hiyo kukua kwa kasi sana ikihofiwa kutumika vibaya katika uhalifu au kijeshi kupitia nyuklia huenda ikawa atari zaidi kwa binadamu.
-
#PeaceOverInterest
 
Imekuja kuuwa music na moves, kampuni za move haziahitaji watu ili kutengeneza moves bali program tu
 
Ni kimbembe hii kitu juzi nilikua nasikiliza goma la Tupac ft DMX iliyotengenezwa kupitia AI huwezi amini utazani ni Tupac na DMX halisi kabisaa
Huwa najaribu kuipa maswali fulani complicated kidogo hiyo ChatGPT,

inarespond chap na kwa ufasaha
 
Back
Top Bottom