Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,391
- 39,484
Tanzania tuna counterfeits nyingi sana; Yaani vitu ambavyo vinaonekana kama vitu original kumbe ni counterfeits. Tatizo ni kuwa kwa mtu wa pembeni akiviangalia vitu hivyo si rahisi kwake kugundua kuwa ni feki kwani vimefanana sana na vitu halisi.
Hali hii ya kununua na kutumia vitu feki imefika mahali hadi tumeanza kuanzisha taasisi za kubiri. Zinaonekana na sura nzuri na zina majina ambayo yanafanya ziaminike kuwa si za kugeza lakini kwa yeyote mwenye kuziangalia anaweza kuona ubiri wake.
Miongoni mwa taasisi hizo ni Tume ya Maadili ya Viongozi ambayo ina Sekretariati ya kudumu ambayo jukumu lake ni kusimamia utekelezaji (compliance) ya sheria ya Maadili ya 1995 as ammended.
Tatizo kubwa la Tume/Sekretariati hii ni kuwa wao hawawezi kuanzisha uchunguzi wa uvunjaji wa maadili kwa viongozi hadi pale mtu au chombo kingine kilete malalamiko rasmi dhidi ya kiongozi huyo. Bila malalamiko hakuna uchunguzi. Yaani, kisheria hakuna "trigger mechanism" kuwa jambo fulani likitokea basi Tume inafanya hivi au vile.
So, where is the joke and who is the joker?