Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi mnasemaje tuhuma za Mwigulu, Bashe, Makamba na Mbarawa?

Stuka

JF-Expert Member
Jul 19, 2022
282
906
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ni Idara ya Serikali inayojitegemea chini ya Ofisi ya Rais iliyopewa mamlaka ya kuchunguza tabia na mwenendo wa kiongozi wa umma yeyote kwa madhumuni ya kuhakikisha kuwa masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma yanazingatiwa ipasavyo. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ilianzishwa chini ya Ibara ya 132 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Sekretarieti ya Maadili imepewa mamlaka ya kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya 1995 sura 398. Sheria hii ilianza kutumika tarehe 01 Julai 1995 na inatumika Tanzania Bara pamoja na Zanzibar kwa viongozi wenye madaraka katika Serikali ya Muungano.

Moja ya Jukumu kubwa la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ni pamoja na Kuanzisha na kufanya uchunguzi wowote wa tuhuma za ukiukwaji wa maadili yaliyobainishwa na Sheria, leo ni zaidi ya miaka 2 sasa Mawaziri hawa wanatuhumiwa kwa rushwa, matumizi mabaya ya madaraka lakini hadi leo Sekretarieti ya Maadili iko kimya.

Mawaziri hao ninaowakumbuka kwa haraka pamoja na Mwigulu Nchemba, Makame Mbarawa, Januari Makamba, Hussein Bashe ambapo pia wamekuwa wakitajwa katika ripoti za CAG katika miaka yote hiyo 2 lakini wenzetu tuliowapa madaraka ya kuwachunguza na kuwachukulia hatua wako kimya hadi leo taifa linaangamia.
 
Kama taifa lingeshughulika na kufutwa kwa kamati ya misamaha kwa sababu haijulikali iko kwa makusudi gani. Pili katiba yetu inamwegemea raisi tuu badala ya wananchi .
 
Back
Top Bottom