GE2025 Tume ya Afrika yalaani vikali unyanyasaji wa wapinzani na Wanaharakati Tanzania, yataka haki za binadamu uhuru wa Habari na Mitandao kipindi Uchaguzi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,743
Reaction score
2,599
Tume ya Afrika kuhusu Haki za Binadamu na Watu (ACHPR), imeeleza wasiwasi wake kwa Tanzania kuhusu kukiuka haki za binadamu, hususani uzimaji wa intaneti wakati wa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu Oktoba 2025.

Azimio kuhusu Hali ya Haki za Binadamu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililotolewa Agosti 6, 2025 lililotokana na kikao cha ACPHR cha 84 cha Kawaida, kilichofanyika kwa njia ya mtandao, limetaja matukio ya uvunjifu wa haki za binadamu yakiwemo madai ya kunyanyaswa kwa wanaharakati wa Kenya na Uganda waliohudhuria kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Mei 19, 2025.

"Ikiwa na wasiwasi zaidi kuhusu vikwazo katika upatikanaji wa taarifa, uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kujieleza nchini Tanzania, ikiwemo kuzuiwa kwa mitandao ya kijamii kama X (zamani Twitter) tarehe 04 Juni 2025, pamoja na kuzuiwa kwa upatikanaji wa Youtube (baadhi ya maudhui), na kutofikika kwa Clubhouse na Telegram bila kutumia mitandao ya kibinafsi (VPN).

Katika hilo ACHPR imerejea azimio lake 580(LXXVIII) 2024 kuhusu Kuzimwa kwa Mtandao na Uchaguzi barani Afrika, ambalo linazitaka Nchi Wanachama kuchukua hatua za kisheria na nyingine zinazofaa kuhakikisha upatikanaji wa intaneti ulio wazi na salama kabla, wakati na baada ya uchaguzi, ikiwemo kuhakikisha kuwa watoa huduma za mawasiliano na intaneti wanachukua hatua madhubuti kutoa huduma bila vikwazo wala kukatizwa;

ACPHR pia imeeleza wasiwasi wake kuhusu taarifa za ukandamizaji wa maandamano na mikusanyiko mingine ya umma kwa nguvu, ikiwemo tukio la tarehe 09 Aprili 2025 kufuatia kukamatwa kwa Bw. Tundu Lissu, na tukio la tarehe 24 Aprili 2025 katika Mahakama ya Kisutu ambapo viongozi wa upinzani na wafuasi wao walizuiwa kuhudhuria kesi ya Bw. Lissu;" imesemantaarifa hiyo.

Pia imeeleza wasiwasi wake kuhusu tuhuma za kupotezwa kwa watu kwa nguvu, mateso, na ukamataji kiholela, ambazo zimekashifiwa na wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, Bunge la Ulaya, na wadau wengine.

"Ikilaani vikali taarifa za kufukuzwa nchini kwa aliyekuwa Waziri wa Sheria na aliyekuwa Jaji Mkuu wa Kenya pamoja na timu yao tarehe 18 Mei 2025, pamoja na kuwekwa kizuizini bila sababu za kisheria na kunyanyaswa kwa wanaharakati wa haki za binadamu kutoka Uganda na Kenya, ambao walifukuzwa nchini tarehe 19 Mei 2025 bila kupewa nafasi ya kukata rufaa au kusikilizwa na mahakama."

ACPHR imeitaka Tanzania kutambua wajibu wake katika Mkataba wa Afrika na mikataba mingine ya kikanda na kimataifa ya haki za binadamu ambayo imeiridhia.

Imeitaka kuheshimiwa kwa viwango vya haki za binadamu vya kikanda na kimataifa kwa ujumla, na hasa kuhusiana na uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi Oktoba 2025;

"Kufanya uchunguzi wa kina kuhusu taarifa za ukiukwaji wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na kupotezwa kwa watu kwa nguvu, mateso, ukamataji kiholela, na ukandamizaji wa maandamano na mikusanyiko mingine ya umma;

"Kuhakikisha uhuru wa kujieleza na upatikanaji wa taarifa katika kipindi cha uchaguzi, ikiwa ni pamoja na kutoa huduma ya intaneti bila vikwazo wala kukatizwa;

"Kuweka mazingira rafiki yanayowezesha kufanyika kwa uchaguzi wa amani, huru, wa haki na wa uwazi, ili kuruhusu wananchi kutumia haki yao ya kupiga kura katika mazingira yasiyo na vitisho, vurugu, au kikwazo chochote;

"Kuhakikisha ulinzi wa watetezi wa haki za binadamu na wanaharakati nchini Tanzania, na kuchunguza taarifa zote za ukiukwaji wa haki dhidi yao;

"Kufanya uchunguzi kuhusu taarifa za kuwekwa kizuizini na kunyanyaswa kwa wanaharakati wa haki za binadamu kutoka Uganda na Kenya, kwa lengo la kuwabaini na kuwafikisha mahakamani wahusika wa ukiukwaji huo na kuhakikisha fidia kwa waathirika kwa wakati muafaka.

"Kutekeleza mabadiliko ya kikatiba na kisheria yaliyotolewa na Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, ikiwa ni pamoja na kuruhusu wagombea binafsi kushiriki katika uchaguzi, na kuhakikisha mahakama za kitaifa zina mamlaka ya kushughulikia migogoro ya uchaguzi."
 
Hiyo taasisi iliundwa na Tanzania kama mwanzilishi wa AU, yaani tuchonge kinyago wenyewe halafu tukikiangalia kitutishe ? Iwe bhojo
 
AZIMIO KUHUSU HALI YA HAKI ZA BINADAMU KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
ACHPR/Res.640 (LXXXIV) 2025

Tume ya Afrika kuhusu Haki za Binadamu na Watu (Tume ya Afrika), iliyokutana katika Kikao chake cha 84 cha Kawaida, kilichofanyika kwa njia ya mtandao kuanzia tarehe 21 hadi 30 Julai 2025:

Ikikumbuka mamlaka yake ya kukuza na kulinda haki za binadamu na watu barani Afrika kwa mujibu wa Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu (Mkataba wa Afrika);

Ikizingatia Maazimio yake ya awali kuhusu Uchaguzi barani Afrika yakiwemo: ACHPR/Res.23 (XIX) 96; ACHPR/Res.133 (XXXXIIII) 08; ACHPR/Res.164 (XLVII) 2010; ACHPR/Res.174 (XLVIII) 2010; ACHPR/Res.232 (EXT.OS/XIII) 2013; ACHPR/Res.239 (EXT.OS/XIV) 2013; ACHPR/Res.272 (LV) 2014; ACHPR/Res.293 (EXT.OS/XVII) 2015; na ACHPR/Res.331 (EXT.OS/XIX) 2016;

Ikikumbuka Azimio la ACHPR.Res.580(LXXVIII)2024 kuhusu Kufungiwa kwa Intaneti na Uchaguzi Barani Afrika, linalozitaka Nchi Wanachama kuchukua hatua za kisheria na nyinginezo kuhakikisha upatikanaji wa intaneti ulio wazi na salama kabla, wakati na baada ya uchaguzi, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa watoa huduma za mawasiliano na intaneti wanatoa huduma bila vikwazo na bila kukatizwa;

Ikikumbuka wajibu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Tanzania) chini ya Mkataba wa Afrika na mikataba mingine ya kikanda na kimataifa kuhusu haki za binadamu ambayo imeiridhia;

Ikielezea wasiwasi mkubwa kuhusu taarifa za ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanyika katika muktadha wa uchaguzi unaotarajiwa kufanyika nchini Tanzania mwaka 2025;

Ikielezea masikitiko kutokana na taarifa za ukandamizaji wa vurugu dhidi ya mikutano ya hadhara na maandamano, yakiwemo ya tarehe 09 Aprili 2025 kufuatia kukamatwa kwa Bwana Tundu Lissu, na tarehe 24 Aprili 2025 katika Mahakama ya Mwanzo ya Kisitu ambapo viongozi wa upinzani na wafuasi walizuiwa kuhudhuria kesi ya Bwana Lissu;

Ikielezea wasiwasi zaidi kuhusu madai ya watu kutoweka kwa nguvu, mateso, na kukamatwa kiholela ambayo yamelaaniwa na wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, Bunge la Ulaya, miongoni mwa wengine;

Ikilaani vikali taarifa kuhusu kufukuzwa nchini kwa aliyekuwa Waziri wa Sheria na Jaji Mkuu wa zamani wa Kenya pamoja na timu yake tarehe 18 Mei 2025, na pia kukamatwa kiholela na kuteswa kwa wanaharakati wa haki za binadamu kutoka Uganda na Kenya, ambao baadaye walifukuzwa nchini tarehe 19 Mei 2025 bila sababu wala kupewa nafasi ya kusikilizwa na mahakama;

Ikielezea wasiwasi zaidi kuhusu vikwazo vya upatikanaji wa taarifa, uhuru wa vyombo vya habari, na uhuru wa kujieleza nchini Tanzania, yakiwemo kufungiwa kwa mtandao wa kijamii X (zamani Twitter) tarehe 04 Juni 2025, pamoja na kuwekewa vikwazo kwa majukwaa mengine kama YouTube, Clubhouse na Telegram, ambapo huduma hizo hazipatikani bila kutumia mitandao ya VPN;

Tume inatoa wito kwa Serikali ya Tanzania kuchukua hatua zifuatazo:

1. Kuhakikisha inaheshimu viwango vya haki za binadamu vya kikanda na kimataifa kwa ujumla, hasa katika kipindi cha kuelekea uchaguzi wa Oktoba 2025;

2. Kufanya uchunguzi kuhusu madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu, yakiwemo kutoweka kwa nguvu, mateso, kukamatwa kiholela, na ukandamizaji wa mikutano ya hadhara na maandamano;

3. Kuhakikisha uhuru wa kujieleza na upatikanaji wa taarifa katika kipindi cha uchaguzi, ikiwa ni pamoja na kutoa huduma ya intaneti isiyo na vizuizi au kukatizwa;

4. Kuweka mazingira wezeshi ya kuhakikisha uchaguzi huru, wa haki, wa amani na ulio wazi, ili kuwawezesha wananchi kutumia haki yao ya kupiga kura katika mazingira yasiyo ya hofu, vurugu au vikwazo vingine;

5. Kuhakikisha ulinzi wa watetezi wa haki za binadamu na wanaharakati nchini Tanzania, na kuchunguza taarifa zote za ukiukwaji wa haki dhidi yao;

6. Kufanya uchunguzi wa kina kuhusu madai ya kukamatwa na kuteswa kwa wanaharakati wa haki za binadamu kutoka Uganda na Kenya, kwa lengo la kuwabaini na kuwafikisha wahusika mbele ya sheria na kutoa fidia kwa waathirika kwa wakati;

7. Kutekeleza marekebisho ya kikatiba na kisheria kama yalivyoamriwa na Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, yakiwemo kuhakikisha kuwa wagombea binafsi wanaruhusiwa kushiriki katika uchaguzi, na kuwa mahakama za ndani zina mamlaka ya kuamua migogoro ya uchaguzi.
 
Ya ulaya walisema inataka kuleta ushoga nchini, haya sasa, hawa hapa waafrika wenzenu,mtasema wanataka kuleta nini? Ccm ni genge la majambazi, huwezi kulikabili kwa mdomo tu, jumuia za kimataifa zichukue hatua kali,( kama zina jeuri hiyo)
 
View: https://www.facebook.com/share/v/19rMZRkX9x/
 
Kisiwa cha Amani kimegeuka kuwa kisiwa cha wachawi, Mungu saidia watu wako, lakini hapa lilikuwa darasa la nchi mbalimbali duniani sijui saivi tunaonekanaje vile.
 
Back
Top Bottom