Uchaguzi 2020 Tume iliwapotosha wagombea Urais nao wakapotoka?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
1. Mapingamizi yaliyowekwa na Lissu ni matokeo ya tafsiri mbaya ya sheria iliyofanywa na Tume, tume inaongozwa na Jaji na wasomi wa Sheria. Je, wanafanya Nini huko ofisini? Unapotoa misleading instructions kwa wagombea Urais si jambo dogo hata kidogo, si makosa ya kibinadamu haya bali ni makosa ya kitaaluma na maadili kwa umma unaokulipa mshahara.

Kama wagombea wa Urais walipaswa kuwasilisha fom zao tume ya Uchaguzi kwa uhakiki na wao wakazipeleka majimboni kinyume na sheria inavyotaka naamini hawa hawana sifa za kuwa wagombea na wakigombea ugombea wao unaweza kupingwa mahakamani na wakaenguliwa.

Kwa wagombea, hawakutakiwa kusikiliza tume na makabrasha yyao tu bali walipaswa kusimamia Sheria. Naamini Tundu Lisu aliliona ili kwa sababu kuanzia mwanzo alijua anawindwa kuenguliwa, akafuata sheria na ndio maana fomu zake zilipokelewa.

Kama fomu za Tundu lisu zilipokelewa na kuonekana ni halili kwa uteuzi je, fomu za akina Lipumba zimepataje uhalali.
 
Wangemkata Lissu nlikuwa nimeshajiandaa kuandamana. Ningeanzia kule juu kabisa kwenye jukwaa la siasa mpaka nipite Chit Chat, nipite MMU, mpaka chini kabisa kule kwenye complaints appreciation and advice
 
Acha kupotosha wewe.

Wakati Lissu akiwa pale kukaguliwa alikuwa analalama kila sekunde kisa kacheleweshwa. Mulipoelimishwa mnaanza tena kupindua meza.

Uhuru wa kuongea huo afu kesho mnasema mnaminywa.
 
Ufinyu wa maono na utambuzi wa mazingira halisia.
Kwanza idadi ya wagombea ni kubwa.
Pili Idadi ya form ni kubwa.
Tatu muda wa kuzipitia kwa usahihi ni mdogo.
Option ya tume iko sahihi.
Uwingi wa wagombea na ukubwa wa form siyo kigezo cha kupindisha sheria. Hii inaonyesha jinsi tume isivyo huru ku handle mambo.
 
Kupinga matokeo ya urais mahakamani hiyo haipo kisheria... Lakini kwa Hili la kufuta mapingamizi mahakama ya Katiba inahusika....
 
Wangemkata Lissu nlikuwa nimeshajiandaa kuandamana. Ningeanzia kule juu kabisa kwenye jukwaa la siasa mpaka nipite Chit Chat, nipite MMU, mpaka chini kabisa kule kwenye complaints appreciation and advice
H ha ha ha haaaa! Asante kwa kuniongezea siku...H ah ha aaaaa! I like this.
 
Kamugisha, haya mapungufu aliyoyaona Lisu angalikuwa ameyafanya yey, basi wangelimuengua! They mislead the contestants na kwa vile hawawezi kumkata Magu, wamefunika kombe mwanaharamu apite!
Lisu kaachwa afanye kila vurugu ilimradi isiwe ya kutia hasara au mauwaji, hata kivunja sheria naaachwa tu ili aoate muda wa kujitangaza kisha aadhibiwe kwenye sanduku.
Sasa kuachwa kwake kisiwe kisingizi cha kujua sheria,
 
Cdm waoga sana wa sanduku la kura, mnataka ushindi wa mezani kwenye uraisi?! Waambieni mabeberu wenu chuma bado kipo sana
Chuga gani kinashiriki kuuza nyumba za umma kwa hawana zake? BEBERU ni nani
 
Lisu kaachwa afanye kila vurugu ilimradi isiwe ya kutia hasara au mauwaji, hata kivunja sheria naaachwa tu ili aoate muda wa kujitangaza kisha aadhibiwe kwenye sanduku.
Sasa kuachwa kwake kisiwe kisingizi cha kujua sheria,
Una elimu gani?
 
Back
Top Bottom