Tumaini University Makumira na Uhuni Wanaoufanya

Tumaini University Makumira na Uhuni Wanaoufanya

wew sio bure hzo data kama hujazipika bas naww nimmoja wao
 
Wabongo tuna shida kubwa mno hasa ya kutokuwa responsible na matatizo binafsi.

Tumeegama sana upande wa lawama! We seem to be the most excellent creatures in blaming for whatever challenges we face in our course of living.

Mtu mlalamishi always namchukulia irresponsible. Do whats right & Stop blaming others!
 
pole mkuu itakua wamekula kichwa.
kabisa, si kwa majungu haya aisee. Huyu jamaa hana tofauti na sungura aliyeshindwa kuzifikia ndizi kwa vile ziko juu akaamua kusema "sizitaki mbichi hizi".
 
Kwendraaaaaaa zako wewe ni nani?umefanya upupu ukatimuliwa unakuja kulalama huku?
 
Kuna theory mbili hapa

Mosi: ni uzalendo umekufanya ukaandika haya (I hardly believe in this theory)

Pili: Umeachika na chuo ukaamua kuleta umbea wa chumbani (Most probable)

Anewei, taarifa imeshiba mno kiasi cha kuwapa stroke wahusika wa pande zote (i.e. Wezi, Walioibiwa pamoja na taasisi husika)
 
ntawaunga mkono wote wanaokwepa kodi za kijinga kijinga


nawapongeza makumira
 
Taarifa kama hizi si za kupuuza wahusika na sisi tunatakiwa kuziangalia kwa umakini. Alowances tunazo ambiwa hazikatwi kodi hii inawahusu zaidi TRA, lakini ukweli wengi wetu hatutaki tukatwe kodi kwenye viji allowance tunavyo pata. After all wafanya kazi ndio hulipa kodi kubwa sana Tanzania. Na hii hali sidhani kama iko huko Makumira tu katika taasisi za umma na binafsi Tanzania. Je kutolipa kodi allowance ni kosa kisheria. Tuelimishane. Kwa muda mrefu Tumaini Makumira ilikuwa TUMAINI IRINGA hadi Iringa ilipo panda hadhi lakini mleta mada haonyeshi tofauti.

Mifuko ya Akiba ya Jamii hili swala ni haki ya wafanyakazi kupata stahiki zao. Jukumu la chuo kulipa na pia ni jukumu la mfuko kuhakikishwa malipo yamefanyika. Hili tatizo liko vyuo vingi ingawapo sasa hivi kwa serikali linapungua lakini bado yako madai ya malipo kwa wafanya kazi kadha.

Dai la wahadhiri kutokutosha wa kulaumiwa hapa kama ni kweli ni TCU kwani ni kazi yao kusimamia vyuo. Madai ya mleta uzi hayasemi viwango vya TCU vikoje hivyo anatumia hisia zaidi kutuaminisha kwamba kuna tatizo. Mfano anasema kuna maprofessor 3 je kwenye list yake ya wahadhiri mbona hao hawaonekani pale juu. Kustafu kwa mtu sio lazima kumfanye ashindwe kazi, huko vyuo vya umma mbona wastaafu ni wengi na wanapiga kazi kwa mikataba?Ukisema mtu anafundisha koozi sita-ni kwa mwaka au kwa semester, koozi zenyewe ni kubwa kiasi gani. Mleta uzi atuambie hizo masters program ni by course work au research, je chuo kinatumia part time walimu au vipi. Taarifa hii haina data ya kutosha kumuwezesha msomaji atoe hukumu. KIUFUPI KUNA SUMU ZAIDI na si taarifa ya kutafuta dawa kama tatizo kweli lipo.

Tupe ufafanuzi mkuu tuelewe kipi kinaendelea au ni kweli kama wachangiaji wengi wanavyosema eti una bifu na chuo?
 
Tumaini ya Iringa, ambayo baadaye ilikuja kuwa University of Iringa (UoI), ni copy and paste ya hiyo yab Makumira,
 
Chuo kizuri sana hicho Mzee baba,vyuo vikuu vingine vya private hali ni mbaya zaidi.
Cha msingi kubaliana na yaliyokukuta,Usifikiri huo unaa ulio uelezea pamoja na vielelezo vyote ndio umewakomoa.Hiyo ni taasisi,wataelekezwa cha kufanya ili mambo yaende sawa,ila wewe utaendelea kuteseka na kupigika
 
Kwa nini usipeleke taarifa yako vyombo husika kama unadhani itasaidia?

Bila shaka una chuki zako sasa unapambana kukichafua Chuo kama sehemu ya kisasi. Kwa nini usifuate njia zingine zakisheria kutafuta unachokitafuta badala ya kuweka JF utumbo huo?

we kweli bongolala, kila mtanzania ni mlinzi wa nchi yake, badala usikitike watanzania wenzako wanavyonyanyaswa kwa kudhulumiwa na serikali inavyoibiwa kodi huna aibu kuandika hivi. kaa kimya km huna cha kuchangia
 
Chuo kizuri sana hicho Mzee baba,vyuo vikuu vingine vya private hali ni mbaya zaidi.
Cha msingi kubaliana na yaliyokukuta,Usifikiri huo unaa ulio uelezea pamoja na vielelezo vyote ndio umewakomoa.Hiyo ni taasisi,wataelekezwa cha kufanya ili mambo yaende sawa,ila wewe utaendelea kuteseka na kupigika

niteseke na nini, kwa taarifa yako tu niko vizuri kuliko unayodhani, ila najaribu kupaza sauti ndugu zangu wasaidiwe. Usijifanya mwamuzi. kwa ufupi tu ujue hizi taarifa zipo kwenye vyombo vya serikali subiri we ndio utateseka muda si mrefu
 
IDADI YA WAHADHIRI NA RANK ZAO

Senior Lecturers - 09
Lecturers - 12
Assistant Lecturers - 46
Ni jambo linalostua chuo kikuu kinachojinasibu kutoa PhD kinaendeshwa kwa 70% na wahadhiri wasaidizi ambao wana-hold elimu ya kiwango cha Masters, hawa ndio wanaofundisha programa za Masters. Mtu mwenye Masters anafundisha Masters program halafu mnatuambia TCU walipitia pale, waliangalia nini, Wizara iwafuatilie maafisa waliotumwa pale pengine wameshikishwa Rupia. Kile chuo kina Associate Professors watatu (03), tena wengine ni wastaafu, kina PhD holders 06 tu, Law wawili, Education wawili na wengine ni wa Theology. Unakuta Mhadhiri moja anafundisha course 6 na ole wako ukatae uaoneshwa mlango tena bila kulipwa chohote. Waziri wa Elimu mama Prof Joyce Ndalichako njoo utembele hiki chuo u-prove hizi claims elimu inauawa. Muda ujao nita-attach Timetable ya semester iliyomalozika hivi punde muone walimu wanavyofundisha masomo mengi tena mengine siyo fani zao.


  1. KODI YA SERIKALI ILIYOIBIWA TANGIA 1997-2018
Katika chuo Kikuu cha Tumaini Makumira Mishahara hulipwa mara 2 kwa mwezi, mwisho wa mwezi wanalipa basic salary tu. Allowances zote hulipwa katikati ya mwezi yaani kuanzia tar 15-17 ya kila mwezi. Allowances zinahusisha House allowance (200,000 – 300,000 kutegemeana na rank ya MFANYAKAZI), Transport Allowance (60,000 – 100,000), Special Faculty allowance (Tshs 550,000), na Responsibility allowance kwa wale wenye nazo ( wenye vyeo chuoni). MALIPO HAYA HUFANYWA MARA 2 KWA MWEZI kwa malengo makuu mawili:
  • Kukwepa kodi za Serikali – maana malipo yote yanayofanywa katikati ya mwezi hayakatwi kodi
  • Kudhulumu wahadhiri na wafanyakazi wengine mawasilisho yao kwenye mifuko ya hifadhi za jamii (NSSF na LAPF ndiyo mifuko unayoruhusiwa kujiunga ukiajiriwa Tumaini University Makumira )

  • Jedwali lililoambatanishwa linaonesha idadi ya wahadhiri, rank zao, miaka waliyoajiriwa na kiasi cha allowance wanacholipwa kila mwezi ambazo hazijakatwa kodi za serikali na Jumla ya fedha zote ambazo hazijakatwa kodi.
Baada ya ukokotoaji ktk jedwali ambalo nimei-attach utaona kwamba kiasi cha Tshs 6,959,400,000 (Almost 7 Billion) ndiyo kiasi cha hela ambayo haikulipiwa kodi za Serikali tangia Chuo hiki kianzishwe mwaka 1997. Kiasi hali halisi yaweza kuwa zaidi ya haya makadirio, kilichobaki ni kwa vyombo husika vya Serikali kufutilia taarifa hizi.

B: KIASI CHA HELA AMBAYO HAIKUWASILISHWA MIFUKO YA HIFADHI ZA JAMII (NSSF & LAPF)
  • Jedwali lililoambatanishwa linaonesha kiasi cha pesa ambayo chuo kimekwepa kuwasilisha ktk mifuko ya hifadhi za jamii. Ukokotoji (calulation) hufanyika kwenye basic pay tu inayokatwa na kuwasilishwa kila mwisho wa mwezi. Ukokotoaji hauhusishi allowances zinazolipwa katikati ya kila mwezi hivyo kuwadhulumu wahadhiri na wafanyakazi wengine pesheni zao mwisho wa siku. Si hivyo tu pesa hizi zilizokwepwa zingetumiwa na mifuko hii ktk shughuli mbalimbali za uwekezaji na kuinua uchumi wa nchi. Kwa kufanya hivi chuo hiki kimehujumu uchumi wa nchi yetu.
  • Jedwali lililoambatanishwa linaonesha allowance kwa mwezi, asilimia inayokatwa na mfuko, miaka(wastani), miezi ktk mwaka na idadi ya wahadhiri ktk rank zao
Katika Jedwali lililoambatanishwa utaona kwa wastani kila Senior Lecturer ameibiwa na chuo kiasi cha Tshs 43,200,000/= mpaka sasa, kila Lecturer chuo kimemwibia kiasi cha Tshs 28,800,000/= na kila Assistant Lecturer ameibiwa na chuo kiasi cha Tshs 18,360,000/= kwa wastan mpaka sasa. Pesa ambzo hazijawasilishwa ktk mifuko ya hifadhi z jamii ni Jumla ya Tshs 1,570,320,000/=. Hii kiasi ni makadirio tu maana data zingine hazikuwa rahisi kuzipata km zilivyo (yaani exact figures). Kiasi halisi ni zaidi ya haya makadirio. Kazi imebaki upande wa mifuko husika kuzifuatilia taarifa hizi kwa undani zaidi.
Ndugu pitia tena TCU guidelines ujiridhishe na uhalali wa hiki chuo, kwa nature ya uendeshaji wa vyuo vikuu ni gharama kubwa sana. Ukitaka kulijua hilo, qngalai investment inayofanywa kwenye vyuo vikuu vya umma. Udsm kwa mfano gharama ya kuwaweka hao maprofesa na senior lecturers unaowaona pamoja na mambo mengine inaigharimu serikali sio chini 120b kwa mwaka. Ndo uniambie, makumira wanaweza kufanya hivyo? Pesa hiyo ikitafutwa wanafunzi watasoma pale? Nafikiri tuwapongeze angalau kwa idadi hii nzuri ya wanataaluma na wanajitahidi sana. Tuna vyuo vikuu vya setikali havina profesa hata mmoja, mfano ni DUCE, MUCE, MWALIMU NYERERE na vingine vingi. Hayo mambo ya kodi, kodi ianakatwa kwenye basic na kama wanafanya hivyo hawana wanachodaiwa. Inavyoonekana wewe hukutaka wafanyakazi wapate motisha zingine, kitu ambacho kinaruhusiwa kisheria. Umekuja kwa hasira sana mkuu, jitafakari upya
 
niteseke na nini, kwa taarifa yako tu niko vizuri kuliko unayodhani, ila najaribu kupaza sauti ndugu zangu wasaidiwe. Usijifanya mwamuzi. kwa ufupi tu ujue hizi taarifa zipo kwenye vyombo vya serikali subiri we ndio utateseka muda si mrefu
Wacha urongo, hata maandishi yako yanaonyesha kilicho nyuma ya mgongo wako. Aibu hii, umefanya utafiti wa uendeshaji wa vyuo vikuu binafsi tz?
 
Back
Top Bottom