Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua haki za msingi za wananchi, huku ikiruhusu haki hizo kuwekwa mipaka kwa mujibu wa sheria pale inapohitajika kwa usalama wa taifa, amani na utaratibu wa umma. Lakini kuna kanuni moja ambayo haiwezi kubadilika:
Sheria lazima itumike kwa usawa.
Kama maandamano yanazuiwa kwa mujibu wa sheria, basi yeyote anayechukua sheria mkononi—bila mamlaka ya kisheria—anapaswa kuwajibishwa pia.
Kwa mujibu wa nadharia ya 𝐌𝐚𝐱 𝐖𝐞𝐛𝐞𝐫, Dola ndiyo yenye mamlaka halali ya kutumia nguvu. Sio vikundi vya mitaani. Sio makundi ya WhatsApp. Sio watu wanaojitangaza kuwa walinzi wa amani. Nguvu halali hutolewa na sheria kupitia taasisi kama Polisi.
Hapa ndipo napata wasiwasi.
Ikiwa kuna watu wanatangaza hadharani kuwa watashughulikia waandamanaji, lakini hawaonekani kuwajibishwa iwapo wanakiuka sheria, wananchi wanaweza kuanza kuhoji kama sheria inatumika kwa usawa. Hata kama mamlaka zina sababu zao, taswira ya usawa wa sheria ni muhimu kwa imani ya umma.
Katika Political Science tunaita hii selective enforcement—hali ambayo watu huona sheria inatekelezwa kwa nguvu zaidi kwa baadhi kuliko kwa wengine. Hata perception pekee inaweza kuathiri uhalali wa taasisi za dola.
𝐓𝐡𝐨𝐦𝐚𝐬 𝐇𝐨𝐛𝐛𝐞𝐬 alisema wananchi wanakubali mamlaka ya dola kwa sababu dola ina wajibu wa kulinda usalama kwa njia ya sheria. Dola inapokuwa taasisi pekee inayotekeleza sheria, wananchi hujenga imani. Lakini pale makundi yasiyo rasmi yanapoonekana kufanya kazi zinazofanana na vyombo vya dola, maswali ya kisiasa hujitokeza.
Amani ya kweli haijengwi kwa hofu. Inajengwa pale ambapo kila Mtanzania anaamini kuwa sheria itamlinda na itamhukumu kwa kipimo kilekile, bila kujali ni nani, anatoka chama gani, au ana maoni gani.
𝐒𝐡𝐞𝐫𝐢𝐚 𝐢𝐤𝐢𝐚𝐧𝐳𝐚 𝐤𝐮𝐨𝐧𝐞𝐤𝐚𝐧𝐚 𝐤𝐮𝐰𝐚 𝐢𝐧𝐚 𝐬𝐮𝐫𝐚 𝐦𝐛𝐢𝐥𝐢, 𝐭𝐚𝐭𝐢𝐳𝐨 𝐬𝐢 𝐦𝐚𝐚𝐧𝐝𝐚𝐦𝐚𝐧𝐨. 𝐓𝐚𝐭𝐢𝐳𝐨 𝐥𝐢𝐧𝐚𝐤𝐮𝐰𝐚 𝐢𝐦𝐚𝐧𝐢 𝐲𝐚 𝐰𝐚𝐧𝐚𝐧𝐜𝐡𝐢 𝐤𝐰𝐚 𝐝𝐨𝐥𝐚 𝐲𝐞𝐧𝐲𝐞𝐰𝐞. 𝐍𝐚 𝐡𝐢𝐬𝐭𝐨𝐫𝐢𝐚 𝐢𝐧𝐚𝐨𝐧𝐲𝐞𝐬𝐡𝐚 𝐤𝐮𝐰𝐚 𝐭𝐚𝐚𝐬𝐢𝐬𝐢 𝐡𝐮𝐩𝐨𝐭𝐞𝐳𝐚 𝐧𝐠𝐮𝐯𝐮 𝐩𝐚𝐥𝐞 𝐳𝐢𝐧𝐚𝐩𝐨𝐩𝐨𝐭𝐞𝐳𝐚 𝐮𝐚𝐦𝐢𝐧𝐢𝐟𝐮 𝐰𝐚 𝐰𝐚𝐧𝐚𝐧𝐜𝐡𝐢.