Tulipoongea walitusema sie wapigaji, leo wanafanya tulioyasema

Tulipoongea walitusema sie wapigaji, leo wanafanya tulioyasema

Huyu wa Zanzibar ingawa kaiba ushindi wa mwenzake ila anaonekana ni mtu mwenye exposure na angalau anajua dunia inavyofanya kazi. Huyu wa kwetu huku ni balaa.
Wa huku kule Zenji nasikia jinale wamwita "Ng'ombe" Shehe wangu
 
Ujinga wa miaka mitano mnaanza kuhangika sasa
Ndo shida ya kulazimisha mtu ambaye ajajiandaa kuwa Raisi awe Raisi na kukiuka matakwa ya wananchi.
Haya mambo ndo yalitakiwa yafanywe siku zote ili maisha ya wananchi yaboreke na tuwe na uchumi imara. Ila kwa sababu hawana akili na wanalazimisha kutawala ndo mana wako hivi
 
Tatizo ya serikali yetu inadhan Kila hela inayotoka nje imekuja kusaidia upinzani! Hususani cdm.
 
Labda nikuulize, tutajuaje huyo mtu hajapata pesa kwenye madawa?

Je, unataka watu waingize na kutoa pesa nchini watakavyo?

Unatakaje labda?
Kiasi kiwe materaial enough to attract investigation. Pesa ndogo ndogo waachane nazo.
 
Kiasi kiwe materaial enough to attract investigation. Pesa ndogo ndogo waachane nazo.

Mkuu, hakuna mtu anayefuatilia pesa ndogo ndogo let alone kuwa na resources za kufanya hiyo kazi.

Watu kila siku wanatuma pesa bongo na kuingia/kutoka na hela bila kuulizwa lolote.

Mleta uzi na wengine kadhaa wanataka mtu asiulizwe lolote regardless of kiasi jambo ambalo halipo sio TZ tu bali nchi zote.

Mleta uzi katolea mfano wa link ya mtu anaondoka na 200k USD na dhahabu kilo8 airport wanasema eti asiulizwe aondoke tu simply sababu ni zake. Hili haliwezekani hata Mwinyi aseme vp.

Hawa hawa watakuja kulalamika dhahabu inaibiwa huku hawataki ukaguzi airports.
 
Hata mimi uwa sioni mantiki wka mtu anayeingiza pesa nchini kumsumbua, bora usumbue anayetoa. Leo kutokana na sheria ngumu za BOT paypal haipokea pesa Tanzania ukitaka fungua online shop kwa Ebay, au Shopify njia ya kulipwa watu wengi wanayoiamini ni paypal na paypal Tanzania haipokei pesa.

Imagine kenya wanapokea pesa mpaka kutoka Upwork kwa Mpesa Safaricom, Skrill ina withdraw kwa Mpesa, paypal pia lakini sisi hizi sheria unajiuliza mtu anapokea pesa analeta pesa ya kigeni sasa sheria zote za nini?
Watu wana akili ndogo sana, kisa chote cha mashariti magumu ya kuingiza pesa ni kukabiliana na vyama vya upinzani. Wasije kupata misaada mikubwa wakafanya mambo yao ya siasa kwa ukwasi, watashamiri na kujidai na sisi hatutaki. Tunataka tuwaone wakiwa ombaomba walambe miguu ya mtukufu.
 
Jamani ifike wakati sasa tuache kuilaumu CCM kizembe.

Granted. CCM ina makosa nengi sana. Siitetei.

Naomba nieleweke kwamba mimi si mtetezi wa CCM wala Magufuli. Ni mtetezi wa haki na mantiki, ni mtetezi wa uchambuzi wa kina usio na uvivu wa kufikiri.

CCM ina makosa mengi.Mengi sana. Magufuli namsema kila siku hapa.

Lakini, hivi CCM ina nguvu gani kiasi cha kulazimisha mambo nchi nzima?

Hao watu waliofanikisha wizi wa kura nchi nzima wote ni CCM?

Na baada ya wizi wa kura kujulikana wazi, wasiokuwa CCM nchi nzima wamefanya nini?

Tumeona hao wanawake wa CHADEMA waaliodai uchaguzi haukuwa wa haki na huru, wamekubali kuapishwa kupata vyeo vya ubunge. Mpaka wameadhibiwa kwa aibu.

Je, kweli tatizo letu ni CCM tu?

Hawa wataalamu watumishi wa umma, wasio na nyadhifa za kisiasa au hata uanachama wa vyama vya siasa, wanaoburuzwa kwa amri kutoka juu, tushasikia hata mmoja kaamua kujiuzulu kazi yake kwa kufuata maadili ya kazi na kukataa maamuzi ya kulazimishwa kisiasa?

Mimi naona hapa kuna jambo la utamaduni limepita siasa, tuache kujidanganya kulaumu CCM tu kila siku.
CCM ni lazima ilaumiwe kwa sababu imefukarisha watu na kufanya ujinga na umasikini utamalaki. baada ya umasikini kutamalaki hata waziri akiachishwa kazi leo, kesho watoto na familia yote ni shida tupu. Hapo ndio tatizo lilipo, hakuna mtu atakayethubutu kujiuzulu kwa sababu ya kukataa upumbavu wakati anajua kesho yake itakuwa ni taabu tupu
 
Really, katika mamilioni yote ya Watanzania?

Hapo ndipo utakapojua CCM ni tatizo, lakini tatizo si CCM tu.

Watanzania ni kama kuku aliyefungwa kamba kwa miaka mingi sana.

Hata baada ya kamba kufunguliwa, kuku huyu bado mwoga na anabaki pale pale alipozoea kufungiwa. Hajui kuwa anaweza kwenda mbali, au anaogopa kwenda mbali.

Kuna matatizo ya kiutamaduni. Kuna matatizo ya woga.

Mzee Butiku alishawahi kusema hili.

Naitafuta hii video siipati labda waliishaifuta kwa amri kutoka juu, naona kuna jamaa waliiweka Twitter na Facebook.

Maendeleo ya watanzania tunaitaji damu mpya kabisaa...ila kwa ccm hakuna hasa kipindi hichi watu wapoteza ajira sana..makampuni mengi yamefunga. Nikiangalia pale quality centre pameanza kuwa gofuu

Sent from my TECNO CX Air using JamiiForums mobile app
 
Huu ndo ushamba wenyewe
Tunajadili kitu kingine
Unakuja na CHADEMA!!!
Ukidhani mshamba ni wewe peke yako? Washamba tupo wengi na kwa taarifa yako ndio wapiga kura sasa! Acha porojo za kujifanya ujuaji, kitu gani unachochadili kidichohusu kushika madaraka?

Uoga tu unakufanya kupepesa pepesa! Hakuna chochote pasipo wanasiasa, Hakuna chochote pasipo vyama vya siasa.
 
Kipimo bado hakijajaa.Siku kikijaa ni balaa.

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
"Those who make peaceful resolution impossible will make violent revolution inevitable" - John Fitzgerald Kennedy.

"It is impossible to predict the time and progress of revolution. It is governed by its own more or less mysterious laws" -Vladimir Illyich Ulyanov "Lenin".
 
Uliona wapi sera za ujamaa zilipofanikiwa duniani?. Mtu masikini huwa apewi lesseni ya udereva kwa matajiri smart
 
Hii serikali ya Ccm miaka mitano ya kwanza imefanya vyema Sana Ila Kama ilivyo kawaida Lila sehemu kuna mapungufu
Hii nchi hakika tutafika huko wananchi mnapo pataka Ila sio Leo Wala kesho
Tupambane tu
 
Tuliwahi kusema humu kwa sera za CCM hii na namna yao ya ufanyaji kazi kamwe Tanzania haitofikia kuwa nchi yenye maendeleo ya kweli ya wananchi na nchi kwa ujumla.

Duniani kote, nchi zilizopiga hatua za kimaendeleo ya haraka ya kiuchumi na ambazo zinachukuliwa kama nchi zenye uchumi mkubwa duniani (Malyasia, Singapore na Thailand) hata siku moja hazikuwai kuwa na sera za kutaifisha hela za watu wanazoingiza nchini kwao.

Nchi hizi hata siku moja hazikuwai kuweka sheria za kibank za kuwabana watu kufanya miamala hasa mikubwa ya kifedha jambo lililopelekea watu wengi kupeleka fedha kwenye nchi hizi na hatimaye fedha hizi zikaleta mapinduzi makubwa kwenye maisha ya wanadamu na uchumi kwa ujumla.

Hapa Tanzania watu wanaojiita kuwa wazalendo, kuanzia mwaka 2015 walianzisha taratibu za kukamata fedha za watu na kuzitaifisha na pia kuweka sheria kali za kudhibiti miamala ya kifedha na matokeo yake tukayaona ndani ya miaka mitano ambapo hela ikawa adimu na watu wengi kupoteza ajira na kukosa fursa za kukopa kwa masharti nafuu kwenye mabenki.

Miradi tunayohangaika nayo Tanzania kama ya treni, miundombinu na masoko ya uhakika yenye hadhi vyote vingeweza kufanywa kwa fedha zinazoingizwa nchini na watu hawa kwa utaratibu mzuri.

Tulipoongea kukemea uporwaji ule wa fedha za wananchi watafutaji watu walituita majina mabovu kuwa nyie wapigaji na wezi Ila baada ya madhara yake kuonekana, leo hii huko Zanzibar wamekuja na hili👇

View attachment 1637873
Kupitia hii Kauli, ningeoenda kujua tu. Hivi Zenji Wana Bank kuu yao?
Kama tunashare hii ya Dar. Sasa anawahakikishuaje Hawa watakao kuja na fedha kutoka nje, hazitahojiwa. . . ?
 
Maendeleo ya watanzania tunaitaji damu mpya kabisaa...ila kwa ccm hakuna hasa kipindi hichi watu wapoteza ajira sana..makampuni mengi yamefunga. Nikiangalia pale quality centre pameanza kuwa gofuu

Sent from my TECNO CX Air using JamiiForums mobile app
Nenda quality Centre, nenda Mkuki Tower , hakuna maduka. Watu wamefunga biashara hadi inatisha
 
Uliona wapi sera za ujamaa zilipofanikiwa duniani?. Mtu masikini huwa apewi lesseni ya udereva kwa matajiri smart
Wao kutaifisha mali ndo wanaona ufahali kumbe wanajenga picha mbaya sana kwa wawekezaji na kufanya wakimbie kwa speed ya umeme
 
Wao kutaifisha mali ndo wanaona ufahali kumbe wanajenga picha mbaya sana kwa wawekezaji na kufanya wakimbie kwa speed ya umeme
Wajamaa na makomunist wote hawana confidence ya kuongoza matajiri na wasomi thus ni lzm wawashughulikie kwa kuwasomesha namba ili waweze kuwatawala.
 
Tuliwahi kusema humu kwa sera za CCM hii na namna yao ya ufanyaji kazi kamwe Tanzania haitofikia kuwa nchi yenye maendeleo ya kweli ya wananchi na nchi kwa ujumla.

Duniani kote, nchi zilizopiga hatua za kimaendeleo ya haraka ya kiuchumi na ambazo zinachukuliwa kama nchi zenye uchumi mkubwa duniani (Malyasia, Singapore na Thailand) hata siku moja hazikuwai kuwa na sera za kutaifisha hela za watu wanazoingiza nchini kwao.

Nchi hizi hata siku moja hazikuwai kuweka sheria za kibank za kuwabana watu kufanya miamala hasa mikubwa ya kifedha jambo lililopelekea watu wengi kupeleka fedha kwenye nchi hizi na hatimaye fedha hizi zikaleta mapinduzi makubwa kwenye maisha ya wanadamu na uchumi kwa ujumla.

Hapa Tanzania watu wanaojiita kuwa wazalendo, kuanzia mwaka 2015 walianzisha taratibu za kukamata fedha za watu na kuzitaifisha na pia kuweka sheria kali za kudhibiti miamala ya kifedha na matokeo yake tukayaona ndani ya miaka mitano ambapo hela ikawa adimu na watu wengi kupoteza ajira na kukosa fursa za kukopa kwa masharti nafuu kwenye mabenki.

Miradi tunayohangaika nayo Tanzania kama ya treni, miundombinu na masoko ya uhakika yenye hadhi vyote vingeweza kufanywa kwa fedha zinazoingizwa nchini na watu hawa kwa utaratibu mzuri.

Tulipoongea kukemea uporwaji ule wa fedha za wananchi watafutaji watu walituita majina mabovu kuwa nyie wapigaji na wezi Ila baada ya madhara yake kuonekana, leo hii huko Zanzibar wamekuja na hili[emoji116]

View attachment 1637873
Nchi ipo mikoononi mwa limbukeni
 
Back
Top Bottom