Tulipoongea walitusema sie wapigaji, leo wanafanya tulioyasema

Tulipoongea walitusema sie wapigaji, leo wanafanya tulioyasema

Kama hutoi maelezo tutajuaje sio za madawa?

Unachukuliwa maelezo sio sababu unashutumiwa bali kuwa cleared. Tatizo mpo defensive muda mnadhani kila kitu mnaonewa.

Mwinyi kawapiga kamba hapo.
Nimekuuliza wapi wanataifisha hela zako zote just because hujadeclare. Nijibu
 
Nimefika US, U.K. na hadi Australia . Kote you declare lakini hata kama hujadeclare hawataifishi.

Swali langu wapi duniani wanataifisha hela zako zote just because hujadeclare??? Nijibu

Jisomee hapo USA unaweza hata kufungwa. Endeleeni kula matango pori mkadhani sasa mnaweza kuleta hela Zenji bila declaration.
 
Jisomee hapo USA unaweza hata kufungwa. Endeleeni kula matango pori mkadhani sasa mnaweza kuleta hela Zenji bila declaration.
Acha kukimbilia kuniambia unaweza hata kufungwa. Nimekwambia nipe mfano wa hela zilizotaifishwa popote duniani just because the owner did not declare at the entry point???

Uliomba mfano mie nikakupa. Sasa na wewe nipe mfano wako hai
 
Inaonekana wewe si mfanyabiashara, na hujui mazingira yanayowakumba wafanyabiashara na wapambanaji esp wanapotoka kupambana nje ya nchi. Sikulaumu.
Mtanzania kaondoka nchini hana kitu, kaenda nchi za watu huko kafanya kazi kwenye mashamba kajibana mpaka kapata dola zake elfu arubaini kaamua sasa ntarudi nyumbani nikajenge nyumba za kupanga halafu anaweka pesa benki anaulizwa alete ushahidi wa alipozipata pesa, ni biashara gani umefanya, risiti ziko wapi n.k

Siku ukienda nje kutafuta maisha bila kujua utafanikiwa au la ukajitosa kwenye machimbo huko ukapata jiwe lako migodini Congo ukauza ukawekewa pesa kwenye account ukarudi nchini kwako na kuulizwa uliuza madini kibali cha kufanya biashara ya madini nje ya nchi kiko wapi hukawa huna kisha ukaambiwa umefanya money laundry ndo utaelewa.

Labda nikuulize, tutajuaje huyo mtu hajapata pesa kwenye madawa?

Je, unataka watu waingize na kutoa pesa nchini watakavyo?

Unatakaje labda?
 
Acha kukimbilia kuniambia unaweza hata kufungwa. Nimekwambia nipe mfano wa hela zilizotaifishwa popote duniani just because the owner did not declare at the entry point???

Uliomba mfano mie nikakupa. Sasa na wewe nipe mfano wako hai

Hilo ni swala la sheria za nchi na nchi zinaamuaje kufanya na mali ambayo haikuwa declared. Point ni kwamba pesa yeyote ile ZNZ, TZ au popote pale itatolewa maelezo.

Leo wanarudi kulekule tulikosema sie. Kweli CCM ni kikundi cha wahuni tu. Hakuna think tank wa kweli mule
Think tank haiwezi kuwa genge la watu waoga na wanafiki kama tunaowaona ikulu ya mfalme j
 
Tuliwahi kusema humu kwa sera za CCM hii na namna yao ya ufanyaji kazi kamwe Tanzania haitofikia kuwa nchi yenye maendeleo ya kweli ya wananchi na nchi kwa ujumla.

Duniani kote, nchi zilizopiga hatua za kimaendeleo ya haraka ya kiuchumi na ambazo zinachukuliwa kama nchi zenye uchumi mkubwa duniani (Malyasia, Singapore na Thailand) hata siku moja hazikuwai kuwa na sera za kutaifisha hela za watu wanazoingiza nchini kwao.

Nchi hizi hata siku moja hazikuwai kuweka sheria za kibank za kuwabana watu kufanya miamala hasa mikubwa ya kifedha jambo lililopelekea watu wengi kupeleka fedha kwenye nchi hizi na hatimaye fedha hizi zikaleta mapinduzi makubwa kwenye maisha ya wanadamu na uchumi kwa ujumla.

Hapa Tanzania watu wanaojiita kuwa wazalendo, kuanzia mwaka 2015 walianzisha taratibu za kukamata fedha za watu na kuzitaifisha na pia kuweka sheria kali za kudhibiti miamala ya kifedha na matokeo yake tukayaona ndani ya miaka mitano ambapo hela ikawa adimu na watu wengi kupoteza ajira na kukosa fursa za kukopa kwa masharti nafuu kwenye mabenki.

Miradi tunayohangaika nayo Tanzania kama ya treni, miundombinu na masoko ya uhakika yenye hadhi vyote vingeweza kufanywa kwa fedha zinazoingizwa nchini na watu hawa kwa utaratibu mzuri.

Tulipoongea kukemea uporwaji ule wa fedha za wananchi watafutaji watu walituita majina mabovu kuwa nyie wapigaji na wezi Ila baada ya madhara yake kuonekana, leo hii huko Zanzibar wamekuja na hili👇

View attachment 1637873
CCM's policy inconsistency. It is terrible.
 
Kwahiyo ulitaka huyu asiulizwe? Aondoke tu maana huyu alikua hata haleti pesa TZ bali anaondoka. Ulitaka apite tu na hizo fedha na dhahabu.

"Mfanyabiashara Noshad Mohamed ameshikiliwa na Jeshi la polisi baada ya kukamatwa katika uwanja wa ndege wa Zanzibar akijaribu kuondoka nchini akiwa na madini ya dhahabu kilo 8 na fedha taslimu za mataifa 15. Amesema mfanya Biashara huyo amekamatwa na pesa za mataifa 15 ikiwemo Dola za kimarekani 233,422 na Euro 57,595 pamoja na fedha mbali mbali za mataifa menngine tofauti."
Kuwa na fedha zako ni jinai?Kuna aliyeibiwa fedha hadi tunapora Mali za watu?Huyo Ndugu ni RAIA wa nchi gani?
 
Kuwa na fedha zako ni jinai?Kuna aliyeibiwa fedha hadi tunapora Mali za watu?Huyo Ndugu ni RAIA wa nchi gani?

Ulitaka aondoke na dhahabu na pesa bila maelezo?

Nini Sasa kazi ya ukaguzi airport kama watu hawakaguliwi?

Niambie nchi Moja ambayo watu wanaingia na kutoka na mali bila ukaguzi?

USA kiwango cha declaration ni kuanzia 10k USD, hiyo ni Marekani, huyu anatoka na over 200k USD na dhahabu bado hutaki atoe maelezo?

Mnapinga kila kitu hata taratibu za kawaida kabisa duniani kote.
 
Nani aje awekeze huko? Mbona taarifa zetu wanazo huku na hata mimi siwezi kumshawishi mtu kwa Sera za awamu ya sifa
 
Maneno tu haya wanapanga wawachuze watu waingie mkenge halafu mwendo mdundo!
 
Kuna jamaa alisema nchi imekabidhiwa washamba na malimbukeni, wala hakukosea. Unaweza kuona wamewatoa watu wangapi kwenye reli walipozuia bureau de change zisifanye kazi wakati wangeweza kuwawekea kanuni .
 
Nani aje awekeze huko? Mbona taarifa zetu wanazo huku na hata mimi siwezi kumshawishi mtu kwa Sera za awamu ya sifa
Hawajui kuwa ni ngumu sana kutengeneza trust hasa ukishaipoteza. Waliambiwa sana wakashupaza shingo
 
Maneno tu haya wanapanga wawachuze watu waingie mkenge halafu mwendo mdundo!
Naona wameona mabeberu wamewakalia kooni kisawasawa sasa hawana option nyingine zaidi ya kutumia akili ili hela ziingie nchini
 
Kuna jamaa alisema nchi imekabidhiwa washamba na malimbukeni, wala hakukosea. Unaweza kuona wamewatoa watu wangapi kwenye reli walipozuia bureau de change zisifanye kazi wakati wangeweza kuwawekea kanuni .
Kati ya vitu ambavyo awamu hii ilinyimwa ni busara na akili kwenye maamuzi
 
Tuliwahi kusema humu kwa sera za CCM hii na namna yao ya ufanyaji kazi kamwe Tanzania haitofikia kuwa nchi yenye maendeleo ya kweli ya wananchi na nchi kwa ujumla.

Duniani kote, nchi zilizopiga hatua za kimaendeleo ya haraka ya kiuchumi na ambazo zinachukuliwa kama nchi zenye uchumi mkubwa duniani (Malyasia, Singapore na Thailand) hata siku moja hazikuwai kuwa na sera za kutaifisha hela za watu wanazoingiza nchini kwao.

Nchi hizi hata siku moja hazikuwai kuweka sheria za kibank za kuwabana watu kufanya miamala hasa mikubwa ya kifedha jambo lililopelekea watu wengi kupeleka fedha kwenye nchi hizi na hatimaye fedha hizi zikaleta mapinduzi makubwa kwenye maisha ya wanadamu na uchumi kwa ujumla.

Hapa Tanzania watu wanaojiita kuwa wazalendo, kuanzia mwaka 2015 walianzisha taratibu za kukamata fedha za watu na kuzitaifisha na pia kuweka sheria kali za kudhibiti miamala ya kifedha na matokeo yake tukayaona ndani ya miaka mitano ambapo hela ikawa adimu na watu wengi kupoteza ajira na kukosa fursa za kukopa kwa masharti nafuu kwenye mabenki.

Miradi tunayohangaika nayo Tanzania kama ya treni, miundombinu na masoko ya uhakika yenye hadhi vyote vingeweza kufanywa kwa fedha zinazoingizwa nchini na watu hawa kwa utaratibu mzuri.

Tulipoongea kukemea uporwaji ule wa fedha za wananchi watafutaji watu walituita majina mabovu kuwa nyie wapigaji na wezi Ila baada ya madhara yake kuonekana, leo hii huko Zanzibar wamekuja na hili👇

View attachment 1637873
Ujinga wa miaka mitano mnaanza kuhangika sasa
 
Back
Top Bottom