Lord Denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 23,491
- 57,970
Tuliwahi kusema humu kwa sera za CCM hii na namna yao ya ufanyaji kazi kamwe Tanzania haitofikia kuwa nchi yenye maendeleo ya kweli ya wananchi na nchi kwa ujumla.
Duniani kote, nchi zilizopiga hatua za kimaendeleo ya haraka ya kiuchumi na ambazo zinachukuliwa kama nchi zenye uchumi mkubwa duniani (Malyasia, Singapore na Thailand) hata siku moja hazikuwai kuwa na sera za kutaifisha hela za watu wanazoingiza nchini kwao.
Nchi hizi hata siku moja hazikuwai kuweka sheria za kibank za kuwabana watu kufanya miamala hasa mikubwa ya kifedha jambo lililopelekea watu wengi kupeleka fedha kwenye nchi hizi na hatimaye fedha hizi zikaleta mapinduzi makubwa kwenye maisha ya wanadamu na uchumi kwa ujumla.
Hapa Tanzania watu wanaojiita kuwa wazalendo, kuanzia mwaka 2015 walianzisha taratibu za kukamata fedha za watu na kuzitaifisha na pia kuweka sheria kali za kudhibiti miamala ya kifedha na matokeo yake tukayaona ndani ya miaka mitano ambapo hela ikawa adimu na watu wengi kupoteza ajira na kukosa fursa za kukopa kwa masharti nafuu kwenye mabenki.
Miradi tunayohangaika nayo Tanzania kama ya treni, miundombinu na masoko ya uhakika yenye hadhi vyote vingeweza kufanywa kwa fedha zinazoingizwa nchini na watu hawa kwa utaratibu mzuri.
Tulipoongea kukemea uporwaji ule wa fedha za wananchi watafutaji watu walituita majina mabovu kuwa nyie wapigaji na wezi Ila baada ya madhara yake kuonekana, leo hii huko Zanzibar wamekuja na hili👇