Tuliotelekezwa na baba zetu tukutane hapa

Baba jayaron

JF-Expert Member
Jun 29, 2015
4,279
5,843
Habari,

Kuanzia leo nataka tukutane wale wote mliokua pasipo uwapo na uwajibikaji wa baba mpaka kufikia mlipo, ilihali wao ni wazima na wangeweza kuwajibika.

Tushauriane;
1. Tuwafanye nini?
2. Nini kifanyike kwetu isitokee?

Nawasilisha hoja kama mhanga ila sasa nina familia yangu i love them to death.

Karibu.
 
Ni muhanga tena mkubwa.

Biblia inasema 7x70, hivyo tuwasamehe na tuwaone kama baba zetu japo hawana watlichotufanyia chochote.

2. Kisasi si juu yetu ni juu Bwana acha Bwana apogane nao.hukohuko waliko watakutana na mgalilaya.

Ushauri: Kwa nyie wanaume, tafadhali chondechonde, msiwatenge watoto mnaowazaa hata km mliozaa nao hamwataki kabisa.

Wanaume, inauma kulea mtoto bila baba. Mnawaathiri watoto, kimungu kimaisha, kimapenzi. Mnawafanya wanawake kukosa ujasir na maneno ya kuwaeleza waliowazaa. Mnamfanya mtoto awe na maswali mengi kuhusu huyo mama yake na ww pia baba.

Mwe, nimeumia sana na mada hii. Ila tuwasamehe km nasi Mungu anavyotusamehe makosa na dhambi zetu.
 
Siwezi sema amenitelekeza ila sijawahi kuwa sehemu ya maisha yake.Amenisomesha na namshukuru kwa hilo.It pains baba yako hujawahi kukaa nae hata siku moja,labda sababu ni familia aliyonayo...Anway nimesamehe and ni move on,Allah amjaalie umri mrefu na amwepushe na maradhi.
 
Nami kama alinikataa namsamehe Tu sina jinsi!hope angenichukua now angekuwa anajivunia kuwa na binti mzuri mwenye maadili na adabu pia kichwa kama mimi..Angekuwa anawaza kupokea mahari now but hatujawahi hata kuonana tangu am still foetus tumboni mwa mama yangu mpaka sasa! popote ulipo nakusaka na nkikupata utaniambia ukweli wote nijue moja!
 
Mie hakuwahi kuwa nami 2001 nikiwa form 1 nilimwandikia barua anipatie hela ya matumizi sio Ada akapotezea. ..lakini namshukuru Mungu nimesoma hadi university na kazi yangu nzuri tu...nampa big up mama kwa kunipigania....Lakin mimi pia nimezaa na msichana ambaye kwa bahati mbaya hatukuoona lakini namsupport mtoto kwa kila kitu .....niwaombe tu wanaume tusiwakatae watoto wetu na kuwaachia mzigo akin a mama
 
The good thing sijawahi kutumia jina lake toka chekechea mpk chuo kikuu, hapa my mom alicheza kama pele. Simchukii ila I've never been proud of him....i saw him twice in my lifè time......Sijawahi kutumia chake sijui labda wakati nazaliwa.....sijawahi kumuuliza mama what happened na sitowahi ila always naaminigi he had nvr loved me coz hata kama wao watakua walizinguana it had nothing to do with me.....Narudia tena simchukii niieleweka hapo, ila nimejihaidi tu moyoni I wanna make and be a good dad so that my children shall be proud of me......In fact nitaanzisha ukoo wangu jamani mniombee, mi nitakua first generation coz wanangu watatumia surname yangu ya sasa ambayo hai-relate kabisa na babu yao........
 
Sikuwahi kupewa matunzo na baba yangu...Mara ya mwisho nilimuona nikiwa darasa la 5 I was 10 yrs old,.....

Malipo yapo hapahapa duniani

Nikiwa na 25 yrs baba aliumwa sana na alipofoka macho, watoto wake alipwategemea wote walikuwa nje ya nchi...

Nilimsamehe na nilimuhudumia hadi anaenda kaburini...

Asante kwa mama angu aliyenikuza na kunifundisha kutolipa kisasi..
 
The good thing sijawahi kutumia jina lake toka chekechea mpk chuo kikuu, hapa my mom alicheza kama pele. Simchukii ila I've never been proud of him....i saw him twice in my lifè time......Sijawahi kutumia chake sijui labda wakati nazaliwa.....sijawahi kumuuliza mama what happened na sitowahi ila always naaminigi he had nvr loved me coz hata kama wao watakua walizinguana it had nothing to do with me.....Narudia tena simchukii niieleweka hapo, ila nimejihaidi tu moyoni I wanna make and be a good dad so that my children shall be proud of me......In fact nitaanzisha ukoo wangu jamani mniombee, mi nitakua first generation coz wanangu watatumia surname yangu ya sasa ambayo hai-relate kabisa na babu yao........
Jmn Mungu akusaidie uwe baba mwema. I also changed ma name nikiwa std seven but sina kinyongo naye. I thank God for all strong single mums who raised us jmn.
 
Hakujali kama alileta kiumbe kama mimi duniani kwanini nijisumbue kumpenda?. Sijawahi kuwa na mapenzi na baba yangu. Labda baadae nitapata ila miaka yangu hii zaidi ya 25 bado hana nafasi. Namshukuru Mama angu na ndugu upande wa mama.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom