Rais Samia; Achana na hoja ya Haki Sawa inakupotezea Ushawishi ndani ya jamii

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,864
RAIS SAMIA, ACHANA NA HOJA YA HAKI SAWA. INAKUPOTEZEA USHAWISHI NDANI YA JAMII.

Na, Robert Heriel.

Kwa maoni na mtazamo wangu ambao kimsingi nauamini, ninaona mbele zaidi miaka kadhaa ijayo. Naomba Mhe. Rais uachane na hoja ya Haki Sawa bhaina ya Mwanamke na Mwanaume.

Hakunaga haki Sawa baina ya mwanamke na Mwanaume.
Nature ipo hivyo na ndivyo ilivyoamua. Kwa kawaida watu wote wanaolazimisha usawa wa haki Kwa vitu tofauti hupambana na Nature/Asili. Hupambana na Dunia ambaye ndiye Mama wa wote tuliopo Duniani, achilia mbali Mungu Baba muumba wa Dunia na vyote vilivyomo.

Mama Samia, nakusihi achana na hoja hiyo ikiwezekana usiizungumzie tena uwapo kwenye majukwaa. Ni afadhali Wasaidizi wako wa chini ndio uwape jukumu Hilo la kulizungumzia Jambo hilo, lakini wewe Kama Rais achana nalo Hilo. Linakupotezea Ushawishi mkubwa katika Mazingira halisi na yakawaida.

Hakunaga haki Sawa Kwa vitu ambavyo havipo Sawa. Hakunaga usawa Kwa vitu vyenye wajibu na majukumu tofauti.
Wanawake Wana haki zao, na wanaume wanahaki zao kulingana na jinsia.
Watoto wanahaki zao na watu wazima wanahaki zao kulingana na hirimu, rika na umri.

Kidini, katika dini kubwa zote na hapa naomba nizitaje, Dini ya kiislamu Kwa madhehebu yake yote, hakuna haki Sawa baina ya mwanamke na Mwanaume. Mwanaume anapewa nafasi zaidi kuliko mwanamke
Dini ya Kikristo Kwa madhehebu yake mengi, Hakuna hayo mambo ya Haki Sawa.
Dini zote za kiutamaduni za Afrika, hakuna haki Sawa baina ya mwanamke na Mwanaume.

Labda Wapagani ndio huweza kuwa na usawa katika mambo yasiyo Sawa.

Nataka kusema nini Mhe. Rais?

Hili suala la Haki Sawa achana nalo kabisa, na Kama lipo moyoni mwako na unalipenda, nakushauri tafuta watu wakulisemea wawe vipaza sauti vyako wewe jifiche na uendelee na hoja zingine.

Wanawake wenyewe wanajijua hawapo Sawa na Wanaume alafu unawaambia wapo Sawa Kwa kweli haikai vizuri. Sisi ambao tuko mtaani, vijiweni au hata watu wako wanaweza kukupa mrejesho katika hili, mtaani hakunaga hayo mambo ya Haki Sawa.

Na usijesema ni Sisi wanaume ndio tunawakandamiza bali hata wanawake wenyewe wengi wao hawautaki huo mfumo wa haki Sawa baina ya mwanamke na Mwanaume.

Mfumo dume ndio mfume sahihi na unaopendwa na Nature Duniani kote, hata Kwa hao wazungu mfumo dume upo licha ya wao kupambana Karne Kwa Karne kuuondoa.

Mhe. Samia, hoja ya Haki Sawa inakuondolea ushawishi ndani ya jamii mpaka Kwa wanawake wengi.

Nitakupa Mfano,
Kuna Mama mmoja anaitwa Joyce Kiria nafikiri niwa WANAWAKE LIVE.
Huyu Mama tangu nimjue anapigania zaidi haki za wanawake, Kwa sehemu kubwa anafanya vizuri kutetea haki za wanawake, ingawaje kuna sehemu anapuyanga lakini hiyo sio hoja ya leo.

Dada Joyce hana uungwaji Mkono mkubwa, Hana ushawishi mkubwa ndani ya jamii licha ya kufahamika zaidi ya miaka kumi sasa.
Sababu kubwa inayopelekea asiwe na ushawishi licha ya kufurukuta ni kutaka kusawazisha Gap baina ya mwanamke na Mwanaume. Anapambana na Nature Jambo ambalo ni hakika atashindwa na ameshashindwa.

Lakini ukiangalia wanawake wenzake ambao haya miaka kumi huenda hawana, yaani wajuzi juzi, kina Dada Irene Mbowe, kina Pastor Rose Shaboka hawa wanaushawishi mkubwa Sana na wanapendwa na kufuatiliwa ndani ya jamii Kwa sababu wanatetea haki za wanawake lakini sio kutaka HAKI SAWA.

Mhe. Rais nataka ujue kwenye nchi yetu mambo yapo Sawa kabisa, changamoto zilizopo ni ndogo Sana. Mpaka unakuwa Rais ni majibu kuwa nchi hii wanawake mnanafasi kubwa ndani ya nchi lakini hampo Sawa Kama wanaume.
Ukweli ni kuwa hamtakuja muwe Sawa na Wanaume dunia ingalipo.

Taifa la Marekani ambalo linajitia ndio Baba WA demokrasia na haki za binadamu mpaka hivi leo tangu lipate uhuru miaka ya karne ya 18 mpaka hivi leo Karne zaidi ya mbili unusu halijatawaliwa na Mwanamke. Hivyo Kwa nchi yetu changa wewe kuwa Rais na ukiwa Kama mwanamke ni Jambo la kushukuru Mungu na kuiona nchi hii inawajali na kuwathamini WANAWAKE.

Kama nchi ingekuwa haiwajali wanawake ni wazi Leo hii usingekuwa Rais, wala baadhi ya viongozi wakubwa wakike wasingekuwa kwenye nafasi hiyo.

Sikatai changamoto zipo lakini hiyo ni Nature kwani hata wanaume wenyewe nao wanapata changamoto hizo hizo.

Mhe. Rais, kitu ambacho nahisi/Kwa hisia zangu, wanawake wengi hawakijui ni kuwa changamoto mnazopitia wanawake kwenye harakati za maisha ndizo hizo hizo wanazopitia Wanaume.

Sema wanawake wanapenda mambo rahisi, wanapenda kupendelewa, wanapenda kupewa hata Kwa wasichokitolea jasho, Jambo ambalo ni ngumu.

Mhe. Rais, utaungana na Mimi kuna kazi za wanaume na zipo kazi za wanawake, Hilo halihitaji ubishi. Lakini haimaanishi Kazi ikiwa yakiume haiwezi kufanywa na Mwanamke, halikadhalika na kazi ikiwa ya kike haiwezi kufanywa na Mwanaume.

Ndio maana hata vitabu vya dini vinaeleza kuwa, Mwanaume atakula Kwa jasho, na Mwanamke atazaa Kwa uchungu.

Kuongoza au kutawala ni KAZI ya kiume. Lakini haimaanishi wanawake hawawezi kuifanya, wanaweza, lakini kutokana na Nature na maumbile ya wanawake walivyo hawataki kuvuja jasho, hawataki kuhenyeka ndio maana Mungu akaona kazi hiyo wanaume ndio waifanye.

Sasa Kwa vile dunia inageuka wanawake nao wanataka kufanya kazi za kiume, Kazi za kuvunja jasho lakini hawataki kuvuja jasho hapo ndio tatizo linapotokea.

Ndugu Mhe. Rais Samia Suluhu.
Hapa Duniani hakuna mwanaume yeyote aliyepata Urais au uongozi wowote wa juu pasipo kuhenyeka, pasipo kutoa jasho, pasipo kupelekwa Msobe Msobe. Hayo ni mambo ya kawaida kwenye maisha ya kuvuja jasho, kazi za kiume.

Hata katika mambo ya kawaida, iwe utafutaji wa maisha, wanaume tunavuja jasho, tunahenyeka, ndio maana kuna muimbaji aliwahi Imba "Wanaume tumeumbwa Mateso kuhangaika"
Hii ni tofauti na nyie.

Wanawake mnapenda upendeleo hata Kwa kuvunja kanuni ya Asili. Yaani ufanye kazi ya kiume alafu hutaki kuvuja jasho, ukihenyeshwa kidogo mnasema mnanyanyaswa, mnakandamizwa, sijui mnatukanwa na kudhalilishwa,
Ukijiingiza kwenye kazi za kiume hayo ni mambo yakawaida Sana. Huko ndilo kuvuja jasho.

Wanawake wanafikiri kuwa wanaume wakienda kuomba kazi basi tunapata kirahisi Kwa sababu ya uanaume wetu. Wakati mambo ya kuzinguliwa, kutukanwa na kunyanyaswa kwetu ni ishu ya kawaida mno, Kwa sababu kwetu wanaume tunapenda kurahisisha mambo.

Kuhusu kuombwa Rushwa hata wanaume tunaombwa Rushwa. Iwe ya Pesa au ya ngono.
Kuna rafiki yangu yeye ni mchezaji mpira, miaka kadhaa iliyopita alipata bingo la kuchezea timu Fulani kubwa hapa Bongo, baada ya hatua zote za kusajiliwa kukaribia kukamilika, yule aliyemuunganisha akampeleka Kwa boss mmoja hivi,
Hiyo Boss akamuomba Uroda Mshikaji, yaani mwanaume anaombwa kulalwa na Mwanaume mwenzake.

Mshikaji sharti hilo likamshinda na kazi akakosa. Yupo mpaka Leo anaranda Randa na Timu za mchangani huko Morogoro.
Jamaa halalamiki

Lakini Kwa wanawake wanavyopenda kulalamika hii kwao ingekuwa big deal.

Mhe. Rais, nataka nikuambie kuwa, unaposema haki Sawa naomba uwaambie pia nao wajiandae Kuvuja jasho. Wasidhani mambo ni mteremko kisa wao ni wanawake.

Hakuna upendeleo hapa, jasho lazima mvuje ikiwa tuu mtajiingiza kwenye kazi za Kiume.

Lazima mnyanyaswe, mkandamizwe, ikiwezekana mteseke Kwa sababu mmetaka mambo yasiyo wahusu.

Heshima mliyo nayo wanawake ni kubwa na inawatosha, lakini Kwa vile mnataka heshima zaidi na yamwanaume ambayo kimsingi sio asili yenu basi hamna budi kuvuja jasho, kuteswa na kunyanyaswa.

Kwa mfano,
Wanawake wanataka haki ya kufanya kazi na kumiliki Mali Kama wanaume,
Tumewapa hiyo nafasi, mnafanya kazi, lakini ajabu ni kuwa mkiambiwa mchangie pato la Familia mnasema hela ya mwanamke niya mwanamke, ya mwanaume ndio ya familia, huo ni upumbavu, tena kwa mwanaume Kama Mimi nakuzaba makofi. Sasa unaenda kufanya kazi ili iweje.

Hutaki kuchangia pato la familia kaa nyumbani lea familia nakuletea pesa, ukijitia kihere here kunisaidia kuvuja jasho/kutaka kufanya kazi ya kuzalisha kipato basi utagewa na majukumu ya kipato ulichozalisha Kwa sehemu.


Mwisho;
Wanawake tunawapenda, na ndio maana tunafanya kila liwezekanalo ili mfurahi.
Mkijiingiza kwenye kazi za kiume jueni kuvuja jasho hakuepukiki Jambo ambalo ninyi hamlitaki.

Mhe. Samia. Achana na hoja ya Haki Sawa haitakujenga wala kuijenga jamii kivyovyote vile.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Mawasilisho ya hoja yapo vizuri sana,naomba kukuunga mkono japo hata kuelewa huyo ulie mpoint na watu walio kama yeye na pengine hata dunia kwa ujumla.

Ile kusema adui wa mwanamke ni mwanamke mwenyewe naikubali sasa kwa vile huku mtaani wakina mama wanavyomnanga mh utadhani sio mwanamke mwenzao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jana niliona aibu kweli kweli... kutamka mbegu hadharani niliona aibu kubwa..
Halafu mwanamke hajazidiwa Mbegu tu na mwanamme...

Kwa iyo sisi wanawake wametuzidi mayai...!!??

Aisee kusimama kuzungumzia maumbile kila siku ni kuonyesha bado kuna kutokjiamini mahali...

Halafu pia muda huisha pambania nchi,gender achana nazo.

Ukweli ni kwamba Mwanamke anayehangaikia sana usawa huishia kuwa Radical kwenye hayo mambo na kuwachukia wanaume..
Huwezi kupambana na asili wakati na wewe ni zao la hiyo asili..

Hata zikiwa awamu mbili Muda huisha. Mzee wa msoga mvumulivu sana.
Ndo maana kila siku anacheka tu...
Anajua kualign na Time.
 
Jana niliona aibu kweli kweli... kutamka mbegu hadharani niliona aibu kubwa..
Halafu mwanamke hajazidiwa Mbegu tu na mwanamme...

Kwa iyo sisi wanawake wametuzidi mayai...!!??

Aisee kusimama kuzungumzia maumbile kila siku ni kuonyesha bado kuna kutokjiamini mahali...

Halafu pia muda huisha pambania nchi,gender achana nazo.

Ukweli ni kwamba Mwanamke anayehangaikia sana usawa huishia kuwa Radical kwenye hayo mambo na kuwachukia wanaume..
Huwezi kupambana na asili wakati na wewe ni zao la hiyo asili..

Hata zikiwa awamu mbili Muda huisha. Mzee wa msoga mvumulivu sana.
Ndo maana kila siku anacheka tu...
Anajua kualign na Time.


Wanawake wengi hufikiri tunawadharau lakini wanashindwa kujua kwenye ishu za kazi za Kuvuja jasho wapo watakaokidharau ambao huwa wengi zaidi kuliko wanaokuheshimu.

Hiyo IPO Kwa wote hata Kwa Sisi wanaume.

Sema wanawake hawajui nafikiri Hilo.

Wanawake hawajui kurahisisha mambo madogo,
 
Mawasilisho ya hoja yapo vizuri sana,naomba kukuunga mkono japo hata kuelewa huyo ulie mpoint na watu walio kama yeye na pengine hata dunia kwa ujumla.

Ile kusema adui wa mwanamke ni mwanamke mwenyewe naikubali sasa kwa vile huku mtaani wakina mama wanavyomnanga mh utadhani sio mwanamke mwenzao.

Sent using Jamii Forums mobile app


Na anapozidi kutamka haki Sawa ndio anazidi kuchochea Moto.

Unafikiri haki Sawa mchezo.

Atafute mtu wa kulizungumzia Jambo Hilo, Kama ndio agenda yake, alafu yeye aendelee na hoja zingine za kitaifa
 
Sasa kama hana hoja za maana na za kimaendeleo afanyeje?Hiyo ndiyo hoja pekee aliyonayo.Hilo ndilo chaka lake la kuficha madhaifu ya uongozi wake.

Unamlazimisha aongee cha maana ambacho hana?Unamlazimisha aongee cha maana wakati kichwani ni debe tupu?

Cha maana ni sisi sasa kufanya yetu kwa kuwa mamlaka hutoka kwetu na uwezo wa kumweka pembeni tunao.
 
Mwanamke yeyote mwenye malezi bora ya kiafrika anajua nafasi ya baba/mwanaume na mama/mwanamke na abadan hawezi kutaka wawesawa...
Hata aliyelelewa vizuri kidini anaelewa mwanaume na mwanamke hawawezi kuwasawa kabisa.
Siasa za kijinga zinatufanya tuuache ukweli ili kutafuta sifa za kisiasa nahivyo kuvuna kura kwa kugawa watu.
Mwanaume ni mwanaume hakuna wakuligeuza hilo naye alipewa dunia aitawale kisha akapewa msaidizi.
msaidizi wa ndani hawezi kugeuka Kuwa mkuu wa nyumba.
 
Bi mkubwa nakukumbusha just in case ulisahau mwaka fulani ulialikwa na wanawake kama.mgeni rasmi katika siku ya wanawake duniani enzi hizo ukiwa Makamu wa Rais.

Siku hiyo uliwaambia wanawake kwamba wewe pamoja na kuwa Makamu wa Rais ila ukifika nyumbani unakuwa mke na unapiga magoti kwa mumeo na kumuandalia chakula, leo umesahau ile kauli ya kwamba wanawake hawapo sawa na wanaume? Dini yako ya kiislam imekulea hivyo? Havi mashababi na maulamaa saivi wanakutazama tu.

Sipati picha Talibani wanatutazamaje sa hii.
 
Hoja ya kijinsia ya kutetea wanawake inapendeza ikiongelewa na mwanaume, ikiongelewa na kusisitizwa na kulazimishwa na mwanamke inaonekana Kama ni ubabe. Huyu Mama angewafunda wanawake wenzake kuheshimu wanaume angeona jinsi wanaume wanavyowatetea wanawake na kwa style hii ataanzisha vita baridi baina ya wanawake na wanaume.
 
Back
Top Bottom