Tulionusurika kufa maji tukutane hapa

Tulionusurika kufa maji tukutane hapa

IKIRIRI

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2018
Posts
2,734
Reaction score
3,027
Miaka ya 2004 Niko kidato cha2 tulikuwa na kawaida ya kwenda beach kuogelea kila wiki.
Sasa wiki1 nakumbuka nilikuwa na wanangu4 wazoefu sana mda ule Mimi nilikua muoga sana wa maji.
Kumbe tulivyoingia kuogelea maji yalikuwa yanajaa,nimekuja kugundua too late,mbaya zaidi wale wataalamu wa kuogelea walikuwa mbali na Mimi,hata ningeita wasingesikia kamwe.

Jamani jamani kifo cha maji hatari sana yaliyonikuta Mungu anajua,sijui hata nilijiokoaje nadhani mda ulikuwa bado sina hamu tena na maji.

Ushauri: km hujui kuogelea jiweke mbali na maji.
 
nimenusurika kufa na maji twice ni dhairi siku zangu zilikuwa bado hazijafika, sifa za kijinga zilitaka kuniua.
 
Kuna siku naogolea coco kumbe Sasa jioni maji Yana kuja na yanarudi yakanipeleka mbali bila kujua nakuja kushtuka Niko mbali Seema uzuri palikuwa na watu wengi ilibidi nimshike braza mwenye tairi..WANAWAKE wanapelekwa mbali halafu wanabakwa utafanyaje jamaa anataka kukuacha anakwambia mpe kidogo akuokoe??
 
Duuh huu Uzi umenikumbusha mbali Sana

Ilikuwa mwaka 2011 nikiwa form six huko mwanga Kilimanjaro ,alikuja dada mzungu jirani na shule basi nikaja kumshobokea na viinglish vyangu vya broken.

Mtoto akaja kukolea akawa anakuja school asiponiona analia basi masela wananisaka Kila chimbo kwamba mzungu wako analia huko.

Basi siku moja kaja na wazungu wenzake Kama watatu wakasema tukaogelee, nikawabeba washkaji zangu Kama kumi ivi..

Kufika bwawa lenyewe la umwagiliaji limejengwa kwa sakafu,basi watu wakapunguza nguo wakaanza kuruka kwenye maji ,kiukweli mi sijui kuogelea nkabaki mwenyewe nje nawashangaa Mara wakaanza come on men sio parefu
Nkaona itakuwa aibu niende na watasha alafu wajue sijui kupiga mbizi Mara nkapunguza nguo nkasogea nyuma umbali wa Kama mita kumi nkakimbia nkajitosa kwenye bwawa bwaaaaa
Watu ohhh oyeeee hiooo ....Mara naibuka nazama ,naibuka nazama nikaona ndo mwisho tayari sasa

Ikafika hatua sasa nikiibuka kidogo nanyoosha mikono kuomba msaada tatizo sasa wenzangu wakajua ni manjojo daah nlikunywa maji machafu Kama Lita tano ivi nahisi

Basi akaja malaika wa mungu ,jamaa mmoja akatambua nimezidiwa akaja akaniokoa daaah

Niliumwa U.T.I Kama mwezi mzima ivi
"Ukitaka kujua maji sio uhai we Zama tu utapata mrejesho"

Kwa sasa ata maji ya beseni tu nayaogopa ..
 
Hii imewahi kunikuta..Nilikuwa sijui vizuri kuogelea..Uogeleaji wangu ilikuwa siangalii ninapokwenda..Kichwa kipo ndani ya maji macho nimefumba..Nikaanza kwenda wrong direction naelekea kwenye kina kirefu bila kujijua..

Imefika stage nataka nisimame miguu haifiki chini then naanza kuzama..Nilidata..Nikianza kupiga mbizi kwa kasi huku sijui naelekea wapi..Hapo nishapanic..Mungu alikuwa upande wangu,nilikuwa naelekea kwenye kina kifupi..

Baada ya kuchoka kabisa na kuona siwezi tena kuendelea nikaamua nisimamame..Nikagusa chini..Maji yapo kifuani..Nilitembea hadi nje nikabeba nguo zangu na kusepa bila kuaga washkaji...

Hii siku siji kuisahau kamwe..
 
Mimi naziheshimu sana swimming pool za kwenye mahoteli makubwa, nilikuwa nafikiri ni fupi, sasa siku moja nikasema ngoja na mimi niogelee kwenye swimming pool, aisee nilikunywa maji mpaka nikajamba na kauharo kidogo na kamkojo kidogo kakatoka, siku ile ndiyo nilijua maji ya swimming pool sio masafi kama yanavyoonekana
 
pole sana mkuu
 
Duuh huu Uzi umenikumbusha mbali Sana..
Ilikuwa mwaka 2011 nikiwa form six huko mwanga Kilimanjaro ,alikuja dada mzungu jirani na shule basi nikaja kumshobokea na viinglish vyangu vya broken.mtoto akaja kukolea akawa anakuja school asiponiona analia basi masela wananisaka Kila chimbo kwamba mzungu wako analia huko.
Basi siku moja kaja na wazungu wenzake Kama watatu wakasema tukaogelee, nikawabeba washkaji zangu Kama kumi ivi..
Kufika bwawa lenyewe la umwagiliaji limejengwa kwa sakafu,basi watu wakapunguza nguo wakaanza kuruka kwenye maji ,kiukweli mi sijui kuogelea nkabaki mwenyewe nje nawashangaa Mara wakaanza come on men sio parefu
Nkaona itakuwa aibu niende na watasha alafu wajue sijui kupiga mbizi Mara nkapunguza nguo nkasogea nyuma umbali wa Kama mita kumi nkakimbia nkajitosa kwenye bwawa bwaaaaa
Watu ohhh oyeeee hiooo ....Mara naibuka nazama ,naibuka nazama nikaona ndo mwisho tayari sasa
Ikafika hatua sasa nikiibuka kidogo nanyoosha mikono kuomba msaada tatizo sasa wenzangu wakajua ni manjojo daah nlikunywa maji machafu Kama Lita tano ivi nahisi
Basi akaja malaika wa mungu ,jamaa mmoja akatambua nimezidiwa akaja akaniokoa daaah
Niliumwa U.T.I Kama mwezi mzima ivi
"Ukitaka kujua maji sio uhai we Zama tu utapata mrejesho"
Kwa sasa ata maji ya beseni tu nayaogopa ..
hawa wazungu wametuzidi kwa kila kitu mkuu,mm nlipata mshaji mmoja alikua anafanya research hapa bongo nikampa support yakutosha,basi alipomaliza nikampeleka mwanza ,kesho yake tukaingia ufkweni nikaka benchi na makonyagi yangu namcheki jamaa anavyocheza na maji,nkaona hiyo michezo nachezaga mtoni acha na mimi nicheze ziwani kuingia tuu wimbi hilo!,likanipeleka kusikojulikana ,nkaanza kuhangaika naona kama ndoto kumbe laivu,likaja wimbi lingine likanrudisha nkaponea ,konyagi ilikwisha nguo karibia nziache natetemeka hapo nkajua pombe sio chai,hadi leo kuoga ni chapu nakutoka sina mbwembwe na maji mimi.
 
Ilikua pande za bahari beach kwa kando hivi.
niko na marafiki zangu wanapata msuba mi nikaona isiwe mambo ngoja nikapige mbizi.
Basi nikawa naogelea maji ya level yangu baada ya muda hivi nikawa narushrusha miguu na mikono nikawa naelea elea nikajiona yes nishajua kuogelea. Nikawa nafanya hivyo nikichoka nakanyaga chini. Sasa nilielea kwa muda mrefu kidogo kumbe maji yalishanipeleka kwenye kina kirefu. niliposema nishushe miguu nikanyage chini ndio balaa lilipoanza. Miguu haifiki chini na nishakunywa vikombe kadhaa. Nikaanza kutapatapa piga maji kama sina akili nzuri nilitoka niko hoi washkaji wanafurahi eti duh unayakata maji. kumbe mwenzao nimeponea tundu ya sindano.
 
hawa wazungu wametuzidi kwa kila kitu mkuu,mm nlipata mshaji mmoja alikua anafanya research hapa bongo nikampa support yakutosha,basi alipomaliza nikampeleka mwanza ,kesho yake tukaingia ufkweni nikaka benchi na makonyagi yangu namcheki jamaa anavyocheza na maji,nkaona hiyo michezo nachezaga mtoni acha na mimi nicheze ziwani kuingia tuu wimbi hilo!,likanipeleka kusikojulikana ,nkaanza kuhangaika naona kama ndoto kumbe laivu,likaja wimbi lingine likanrudisha nkaponea ,konyagi ilikwisha nguo karibia nziache natetemeka hapo nkajua pombe sio chai,hadi leo kuoga ni chapu nakutoka sina mbwembwe na maji mimi.
tatizo hatupendagi kusema hatuwezi kuogelea, na maji hayajaribiwi lazima yakuumbue tu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom