nadhan ni mhimu sana ukaangalia nini kimesababisha abadilike au wewe ubadilike..........
jiulize, je mlivyoanza uhusiano wenu na baadae ndoa alikuaje na wewe ulikuaje, saizi yupoje na wewe upoje, anakutazamaje na wewe unamtazamaje..........
ukishapata majibu ya maswali hayo, njoo ujiulize je ndoa yenu imefika a point of no return?..........
kama jibu ni NO, jipige pige umwombe outing moja, mwende sehemu tulivu, huko ukamwambie ukweli vile unavoitazama ndoa yenu, ilikotoka na inakoelekea.........
usim'bebeshe yeye zigo la lawama, huko points zikawe ni way out kutoka hapo mlipo, zaidi sn hata akikulaumu 'jitwike' hizo lawama zake so long as anatoa way out kutoka hapo!..........
nina uhakika akiona umeshuka, lkn aibu itamshika na atatafuta namna ya kukuridhisha..........
kwa maelezo yako aliyoya-quote
demi sidhan kama ndoa yako ipo hatarini kihivyo, ila nadhan umeolewa na mwanamme mwenye wivu au hajiamini!