Kiukweli Maisha ya Usingo siyo kabisa. Kwa Mtu wa Umri wa 25+ ni maisha ya kuwa wawili kama maumbile yalivyo. Changamoto za Maisha zimepelekea hii hali but Ukweli siyo kabisa. Sikutegemea kama nitakuja kukaa kwenye Hii hali Baada ya kuwa kwenye Ndoa kwa Miaka kumi. Mapenzi yalivurugika Mwaka wa Tisa. After break up, Nimeshindwa kabisa kupenda tena, Naishia single Mwaka sasa najihisi kichaaa. Yaani wanawake wote siwaelewi tena Japo ni wazuri sana wa Tabia na Mwonekano. Akili imedumaa. Nyumba imekuwa kama mapango ya Amboni. Kula ilimradi tuu nimekula. Mkate,mihogo, Katanga nk. Yaani Haya maisha siyo kabisa. Mungu hakutuumba tuwe hivi. Kibaya zaidi unambembeleza EX arudi anakuambia Never!!!! Dah ...... Only God knows