Tulinganishe biashara na ajira hapa

Nimeshangaa sana kuona watu wanabeza mtaji wa 500k-1ml kuleta faida ya 300k-500k kwa mwezi.
Maana yake ni kwamba unalaza kuanzia 10k hadi 17k kwa siku.

Labda walielewa hiyo faida ya 500k unaipata kwa siku.
Wanaobisha hawajawai kufanya biashara
 
Muda mwingi anautumia kufanya mazoezi na kucheza mpira tofauti na mask ambae muda mwingi anawaza kutanua biashara na makampuni yake
Hahahaha kwani huo mpira ancheza KILA SAA mazoezi anafanya KILA SAA na HUYO musk NAYE kwani muda WOTE anawaza BIASHARA TU SI Kuna muda anatoka KWENDA kula Bata ALAF musk anapenda starehe HUYO JAMAA ACHA TU mkuu mara ufukweni mara wapi. Hitimisho akili binafsi na MUNGU kwishaaaaaa


Kwishaaaaa


Bro Alex on la beats yoow...... Jah iz really
 
Kitu unachokipa muda zaidi ndio kinachokupa matokeo kama na hapa hujaelewa basi
 
Yes iyo ni nje ya matumizi japo kwa kujibana sana

Hivi tukichukulia mshahara wa take home 500k hapo ni ndani au nje ya matumizi
Take home ni pesa anayobakiwa nayo mwajiriwa ukishatoa tax, pssf,NHIF, na michango mingine kulingana na kada yake.
mweny take home ya 500k it means basic salary inaweza kuwa 650-700k

Hiyo 500k ndo hela yake ya matumizi, saving & kila tu...
 
Take home ni pesa anayobakiwa nayo mwajiriwa ukishatoa tax, pssf,NHIF, na michango mingine kulingana na kada yake.
mweny take home ya 500k it means basic salary inaweza kuwa 650-700k

Hiyo 500k ndo hela yake ya matumizi, saving & kila tu...
Biashara ni ngumu kukimbizana na Kodi ya frem na TRA lakini naweza kusema ukipambana Ina unafuu

Mimi nikisema nimepata 500k kwa mwezi hapo nimetoa kila kitu kula na matumizi mengine japo wakati mwingine upepo unabadirika ila sijawahi shuka 300k kwa mwezi sasa sijui hiyo nitaitaaje saving au take home
 
Hiyo manake ni net profit, faida yako unayobakiwa nayo ukitoa kodi na expenses zote.

So hiyo unawez save au ukaendelea kuweka kweny mzunguko wa bishara whatever but ni faida kamili
 
Hiyo manake ni net profit, faida yako unayobakiwa nayo ukitoa kodi na expenses zote.

So hiyo unawez save au ukaendelea kuweka kweny mzunguko wa bishara whatever but ni faida kamili
Ni kweli, japo sijawahi kuwa na uwezo wa kusave faida ninayoipata hii nikiweza nitakuwa tajiri soon
 
Usisave weka yote kweny mzunguko wa biashara yako kukuza faida, ukisave utapoteza time tu.
Kuna miezi niliamua niwe nafanya kama unavyosema ndani ya miezi sita nilikuwa na rundo la hela(kwa level yangu) nikafikiria nifungue kitengo kingine lakini nikifikiria mfanyakazi nitakae muweka nikaona nitapoteza tu na nikijaza duka mauzo almost ni yaleyale kwanini nisiende nunua tofali na kuita mafundi hahahaha hadi sasa pesa nimezipanda ardhini
 
Biashara ni bora kwa biashara yenye faida chini kidogo au sawa na mshahara. Ila kuacha kazi ya mshahara wa mil 5 halafu ufanye biashara ya faida ya laki tano kwa mwezi huo ni ukichaa. Ndani ya miaka 10 mwenye mshahara atakuwa mbali sana kuanzia saving ,kujenga n.k na NSSF itasoma 120M ambayo ikichukuliwa utajenga lodge mbili huku wa biashara ndani ya huo muda ndio kwanza atakuwa anaingiza M3 kwa mwezi na kuona biashara yake imekua sana.

Sio kila biashara ni bora kuliko ajira.Ni maoni ya mimi muajiriwa kutoka halmashauri ya Kakonko.
 
Kazi gani iyo wanalipwa mshahara Million 5
 
Watanzania wanaolipwa mshahara wa milion 5 kwa mwezi ni asilimia ngapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…