Tulinganishe biashara na ajira hapa

Tulinganishe biashara na ajira hapa

WAKUU nisaidieni basi huwa nawaza HIVI mishahara huwa Ina gundu ? Samahani ka NME wakwaza IKO HIVI👉 Ronaldo analipwa mahela mengi unaambiwa ni MAbilioni SIJUI kwa SAA mara dakika alafu unakuja kushangaaa Miaka YOTE HIYO haja fikia hata bilioni moja ya Dola ya kigogo musk KWENYE zaidi ya MAbilioni ya Dola mia tatu na KITU aliyo nayo JAMAA MPAKA naishiwa nguvu.

Kwishaaaaaa

Bro Alex on la beats yoow..... God is gud
Mishahara haina gundu ila muda wa kuiendeleza izae zaidi kama mfanyabiashara ndio kasheshe

Mimi naweza pata faida ya laki moja kwa mwezi ila uwezo wa kuindeleza hiyo laki moja ije izae laki mbili kwa kutumia biashara ninayofanya ni rahisi kuliko aliyeajiriwa na kupokea mshahara wa laki moja
 
Asantee, inategemea mkuu kwenye kupiga
Bado niwageni siwapi mzigo wa bei ghali. Huku nje ya ajira nachofurahia ni uhuru wa kipato. Kuna siku utapata sana km wakiuza mali zote, na kuna siku napita na mmoja kuzunguka nae kuona km anajua kushawishi wateja ili watoe order nzuri akipita tena
Nimekupata mkuu tuzidi kupambana
 
Mishahara haina gundu ila muda wa kuiendeleza izae zaidi kama mfanyabiashara ndio kasheshe

Mimi naweza pata faida ya laki moja kwa mwezi ila uwezo wa kuindeleza hiyo laki moja ije izae laki mbili kwa kutumia biashara ninayofanya ni rahisi kuliko aliyeajiriwa na kupokea mshahara wa laki moja
Daah HAPO SIJUI hata inakuwaje lakini hata Ronaldo ana BIASHARA zake ILA waaapi

Kwishaaaaaaa

Bro Alex on la beats yoow......... Jah iz really
 
Daah HAPO SIJUI hata inakuwaje lakini hata Ronaldo ana BIASHARA zake ILA waaapi

Kwishaaaaaaa

Bro Alex on la beats yoow......... Jah iz really
Muda mwingi anautumia kufanya mazoezi na kucheza mpira tofauti na mask ambae muda mwingi anawaza kutanua biashara na makampuni yake
 
Kwanza Ajira ni bora na pia biashara ni bora .

Kwa uelewa wangu IPO hivi unapokuwa unesoma na umepata Ajira doesn't matter how much you earn Ila unabidi kufikiria kuwa na biashara yako.

Kwakuwa ukifa
Ukiumwa ugonjwa endelevu
Ukifukuzwa Kazi
Ukistaafu

Yakitokea yote haya Familia yako haitoweza kurithi ujuzi wako , wala Elimu yako Ila familia inaweza kuendeleza baishara zako tena vizuri.

Kwahiyo Kazi ni bora Ila endapo ukiutambua ukweli kuwa you can't make rich in someone's office.

Ikiwa utafikiria hivyo unaweza ukaanza na Kazi then ikafata baishara au ukaanza na biashara na ikafata Kazi yote yanawezekana .

Nahitimisha kwa kusema biashara ni bora ikiwa una facilities zote za muhimu just do business
 
Mishahara haina gundu ila muda wa kuiendeleza izae zaidi kama mfanyabiashara ndio kasheshe

Mimi naweza pata faida ya laki moja kwa mwezi ila uwezo wa kuindeleza hiyo laki moja ije izae laki mbili kwa kutumia biashara ninayofanya ni rahisi kuliko aliyeajiriwa na kupokea mshahara wa laki moja
anashangaa nini RONALDO si mwajiriwa tu akipokea mishahara si anafanyia matumizi tena sometimes expensive kulinda brand yake unafikiri pesa zitakaa,ye haoni athletes wengi wanavyokuwa makapuku baada ya kustaafu?issue sio unaingiza tsh ngapi,je unaitumiaje iyo pesa?unaweza kuwa na salary ya 10m kwa mwezi bila bajeti na mipango ni sawa na mtu asiye na kazi unaweza ata usijenge na usiwe na maendeleo yoyote
 
Tanzania watumishi wa umma ni 500,000 tu

Wengine waliobaki ni secta binafsi kujiajiri...

Sasa Wanaosema ajira ni zaidi ya baishara wapitie hizo Takwimu.

Hiyo kariakoo hayo majengo yanamilikiwa Kwa asilimia kubwa na wafanyabiashara... Sasa niambieni ni wapi Tanzania hii Kuna majengo kama hayo yanamilikiwa na walioajiriwa
 
Hii naifanyia kazi nishasitisha ujenzi kidogo nione kama nitasogea kidogo
sio kusitisha. ACHA. hivyo unavyositisha kwa muda unandelea na biashara na baada ya kuingiza pesa kidogo unazitoa na kuendeleza ujenzi kidogo UNADHOOFISHA BIASHARA. utashindwa kuifanya biashara ikue... itadumaa kila siku utakuwa hapo hapo... acha biashara ikue. Fikiria biashara kuzalisha biashara nyingine. muda wa kujenga ukifika utajenga bila kuathiri biashara na bila kusitisha sitisha...... understand????
 
Inabidi kukubaliana nae maana kupata faida kubwa sawa na mtaji ni = na Impossible
Hakunielewa kitu kimoja, hapo nimeandika mtaji wa 500k-1mil

Means nikiwa na mtaji wa 500k uwezekano wa kufunga faida ya 300k mwisho wa mwezi upo

Pia nikiwa na mtaji wa 1m uwezekano wa kufunga 500k kwa mwezi upo

Ila kwa mitazamo ya waajiriwa niijuavyo kashapiga kama nikiwa na 500k napata faida ya 300k kwahiyo nikiwa na 5milion naweza pata faida mara nne ya faida ya awali kitu bila kujua kuwa wateja wangu ni walewale hata kama yanaongezeka mauzo ila ni kwa asilimia ndogo Sana

Naweza kusema kuna miezi mingine naweza kuwa na mtaji mkubwa ila mauzo yakawa madogo na nisipate faida hata nusu ya mtaji isifike hapa watanielewa wafanya biashara tu hususani wa mtaji tajwa hapo juu na kazi zinazofanana
 
Kitu pekee ambacho mwajiriwa ana kosa ni "leverage power'

Formula ya faida ina kitu cha ziada ambacho hakipo kwenye formula ya mshahara.

Scenario 1
Mshahara =X/t(unalipwa Tsh x kwa mwezi)
njia pekee ya kupata hela nyingi ni kufanyakazi miezi mingi zaidi.

Scenario 2
Faida=QX/t(unapata faida kulingana na units ulizouza kwa muda flani)
Kuna njia mbili za kupata hela nyingi kwa mfanyabiashara,
ya kwanza ni kufanya biashara kwa muda mwingi zaidi(masaa,siku...ukiamua hata weekend,now nina wazo la kuanzisha biashara inayo operate 24 hrs kitu ambacho mwajiriwa hawezi)
Na njia ya pili,ni kwa kuongeza idadi ya bidhaa au huduma(Q) au kufungua matawi mengi zaidi kitu ambacho mwajiriwa hawezi.

Hitimisho
Ajira ni safe zaidi kuliko biashara,hivyo kuchagua njia ipi upite itategemea risk tolerance yako,but all of all, running for business and entrepreneurship,it worth a shot!
 
sio kusitisha. ACHA. hivyo unavyositisha kwa muda unandelea na biashara na baada ya kuingiza pesa kidogo unazitoa na kuendeleza ujenzi kidogo UNADHOOFISHA BIASHARA. utashindwa kuifanya biashara ikue... itadumaa kila siku utakuwa hapo hapo... acha biashara ikue. Fikiria biashara kuzalisha biashara nyingine. muda wa kujenga ukifika utajenga bila kuathiri biashara na bila kusitisha sitisha...... understand????
Nalipa pango kubwa sana kwa mwaka ni pesa nyingi kwa level yangu ya biashara bora nisimamishe kibanda cha room mbili nihamishe familia huko nipange room moja nikijipanga kujenga nyumba kubwa

Ila nashukuru kwa ushauri
 
Back
Top Bottom