Job Ndugai: Wananchi waache kulalamika badala yake wafanye kazi kwa bidii na kujiletea maendeleo

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Ndugaii.JPG
Mbunge wa Kongwa na Spika wa zamani wa Bunge, Job Ndugai amewataka wananchi kufanya kazi kwa bidii na kujiletea maendeleo badala ya kutumia muda mwingi kulalamika.

Akizungumza wakati wa mkutano wa baraza la madiwani kujadili bajeti ya Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (Tarura), Wilaya ya Kongwa, Ndugai amewaasa madiwani kuhamasisha wananchi kuitumia vyema miundombinu iliyojengwa na serikali zikiwemo barabara kwa ajili ya kujiletea maendeleo.

Amesema kuwa jukumu la kwanza la serikali ni kulinda usalama wa wananchi hivyo ni wajibu wa wananchi kufanya kazi kwa bidii na kujiletea maendeleo badala ya kutumia muda mwingi kulalamika. Wakati huo huo, alitoa wito kwa wananchi kushiriki kikamilifu kwenye kampeni endelevu ya utunzaji wa mazingira kwa kuhifadhi ardhi, kupanda miti na kutunza miundombinu.

Chanzo: Habari Leo
 
Ndugai alikosea alipoomba radhi kwa kuongea ukweli kuhusu deni la taifa,

Alopaswa asimamie alichosema ambacho ndio ukweli, na kuna siku tutakumbuka kauli yake.

Alipotishwa kidogo kaomba radhi kwa haki yake ya kutoa maoni, na hawakumsamehe wakamzonga hadi kautema uspika wa bunge
 
Ndugai alikosea alipoomba radhi kwa kuongea ukweli kuhusu deni la taifa,

Alopaswa asimamie alichosema ambacho ndio ukweli, na kuna siku tutakumbuka kauli yake.

Alipotishwa kidogo kaomba radhi kwa haki yake ya kutoa maoni, na hawakumsamehe wakamzonga hadi kautema uspika wa bunge,

Sent from my Infinix X658E using JamiiForums mobile app
Ukikua utaelewa kwanini alijiuzu bado utoto unakusumbua
 
viloba via uzeeni vibaya mbone yeye alikuwa analalami mpaka akapigwa chini atuwache tulalamike kwa raha zetu
 
Za jioni Wakuu.

Jobu Ndugai Spika aliyeweka rekodi ya kujiuzulu amewataka Wananchi kuacha kulaumu na Kulalamikia Watawala na Vyama vya Siasa badala yake wafanye kazi Ili kujikwamua kwenye umaskini na kujiletea Maendelea.

Ameongeza kwamba Wasitegemee Vyama vya Siasa kuwaletea Maendelea.

Tiririka hapa

 
Addiction is real.
and so are Bigoted and Racist Individuals addicted to 'Supremacy'

Huwa wanafurahi kutumia kauli za Watu wakubwa Nchini kuchagiza ajenda zao za Kitumwa. Hata pale wasipowapenda hao Viongozi kama 'Jobu'

Kitaeleweka
(Hayo juu yaliandikwa kabla ya nyuzi kuunganishwa)


Utaelelewa.
 
Back
Top Bottom