Mbilimbili
Senior Member
- Mar 17, 2012
- 172
- 19
Habari za Pasaka wandugu, mimi ni kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 24. Nilitokea kuwa na uhusiano wa kimapenzi na binti mmoja tuliyesoma naye shule ya Msingi mwaka 2001, kwa bahati nzuri kwake na mbaya kwangu yeye alijaliwa kupata mtoto alipomaliza kidato cha nne. Kitu ambacho hakikunifurahisha, sababu tulikuwa marafiki wa kawaida tokea awali. Baada ya mtoto wake kuwa mkubwa, tulijikuta kuwa wapenzi. Na Pasaka ya mwaka jana nakiri kwamba ndio mara ya kwanza, kumvua nguo. Nilijutia uamuzi wangu ila nilikaza roho na tukaendelea kula raha za maisha, ila tokea jana sim yangu hapokei wala txt zangu hanijibu. Nikimpigia mdogo wake ananiambia dada yake hajisikii kuongea na mimi, sijui nilichomkosea wala hataki kunieleza.