Bila kutibu ugonjwa huo uliokwisha ingia vichwani mwa watanzania karibu wote, hata tukiletewa rais malaika Gabriel/Jibril, hatutakwenda popote. Ni lazima tuanza kupambana na hiyo changamoto ya tabia zetu kwanza ndipo tuangalie mbele.Duuh! umeanzisha mjadala mzuri. Lakini leo wikendi nina mahangaiko kidogo. Nitarudi kuchangia, inshallah!
King'asti; uliozungumza liko kwenye hiiyo tabia ya kutokuwa responsible na kukosa accountability; ni miongoni mwa tabia mbaya tulizo nazo ambazo ndiyo ninazotaka tutafute mbinu za kuachana nazo. rais kuacha kushugulikia matatizo ya muhimu ni kuwa irresposnsible, na vile vile inatokana na kuamani kuwa madaraka aliyo nayo ni haki yake (entitled) na wala hakuna wa kumwajibisha. Watu kusahahu na kushindwa kuzungumzia mambo ya muhimu kwa sababu ya kuchekewa ba rais ni kuwa irresponsible kwa kusindwa kumwajibisha rais anapokuwa hakufanya majukumu yake ipsavayo. Kuna vicious circle kubwa sana katika tabia zetu.Mwali, nani anamuwajibisha nani sasa? Ikiwa mfumo mzima ni wa kizembezembe tu kuanzia juu kushuka chini? Huyo boss wangu tu hana nafasi ya kuniwajibisha manake hata yeye binafsi haji ofisini on time, anatembelewa na hawara kazini, lunch anaenda 3 hours?
Gaijin, chukulia mfano wa mtoa maamuzi kwenda mkutano Davos akiacha mgomo wa madaktari. Kurudi mkutanoni he is the hero kwa sababu kawaita madaktari, kachekacheka nao na wakaahirisha mgomo kwa muda!
Mfumo mzima unafanya kazi zisiende. Hata mwenye ethics zake za kazi anaharibiwa na mfumo uliopo. Say issue imejulikana for several months na inawekwa mezani kwako siku mbili kabla ya deadline. Unahitaji collaboration kutoka kwa watu mbalimbali. In the end lazma ulipue ili usilale nacho kidagaa!
Mwali, huoni kuwa unarudia swali hilo hilo ninaloongelea? Kuwa hatuna tabia ya kujituma mpaka ama tulazimishwe kwa namna moja ama nyingine: ama kwa vitishomvya kufukuzwa kazi au kwa incetive ya kupata rushwa. Hilo ni gogor lile lile. Na kweli wengine wetu tunaweza kwenda kulalamika kwa wakuu wa vitengo, lakini je una uhakika gani kuwa mkuu wa kitengo huyo atakusikiliza ilhali wote tuna hulka hiyo hiyo? Unaweza ukamkuta naye yuko kwenye simu akiongelea upuuzi wa namna hiyo hiyo.Mi nadhani kila kitu kinatokana na impunity and lack of accountability. Tungekua tunachukua hatua nadhani watu wangejirekebisha. Asiefunzwa na wazazi atafunzwa na dunia, ikibidi atafunzwa na mahakama.
Huo utakuwa ni utaratibu mzuri, lakini ni nani atakayemkamata waziri na kumpeleka mahakamni iwapo tuna system ya watu wanaoogopa kuwawajibisha subordinates wao labda kutokana na ukweli kuwa anayeishi kwenye nyumba ya vioo huwa hapendi kurisha mawe.Tukizungumzia kuzama kwa meli (mfano) mtu mmoja anaweza kujiuzulu na jambo likaishia hapo, watu wanaridhika kua amewajibika. huo sio uwajibikaji. anae mfata ataendelea na system ile ile. Ikiwa kutakua na utafiti, na wale wote watakao onekana wana makosa ya action, omission or negligence wakafutwa kazi, wakapelekwa mahakamani na kufungwa, kulazimishwa kulipa faini, jina zao na picha zao kutangazwa ili tuwazomee, na serikali ikalipa familia ya majeruhi wote, utaona na system itabadilika, kila mtu atajitahidi kuhakikisha jangaa lile halitokei tena.
Ni kweli hiyo ndiyo hukla yetu, je ni kwa nini tumejikuta hapa? na ni njia gani tunayoweza kufanya ili tung'oke kutoka kwenye dimbwi hili?
Mkuu Kichuguu
(a) Hatujali kabisa ethics za kazi; nadhani hili linaeleweka sana.
Kuhusu hili mimi nadhani ujira mdogo wanaolipwa Wafanyakazi kwa kiasi kikubwa unachangia sana katika tatizo hili. Unakuta mshahara wa mtu unamtosheleza kwa siku labda 10 tu katika mwezi na siku nyingine 20 akili inamzunguka hajui ataishije ili kuweza kukidhi mahitaji yake muhimu kama yuko single au yale ya familia yake.
na hii ndio manaa inaonekana kama vile wafanyakazi wa serilaki wana mgomo baridi. Mshahara mdogo, watu wana ripoti kazini then wanapotea na mambo yao. Serikali inawakopa wafanyakazi, na wafanyakazi hawatekelezi wajibu wao.
Tunahitaji ku overall civil servants. Ongeza mishahara kwa wafanyakazi, sheria za kazi zisimamiwe na tuache mambo ya hivyo hovyo
na ndio manaa inaonekana kama vile wafanyakazi wa serikali wana mgomo baridi. Mshahara mdogo, wana ripoti kazini then wanapotea na mambo yao. Serikali inawakopa wafanyakazi, na wafanyakazi hawatekelezi wajibu wao.
Tunahitaji ku overall civil servants. Ongeza mishahara kwa wafanyakazi, sheria za kazi zisimamiwe na tuache mambo ya hivyo hovyo
Ndivyo tulivyo.
Baada ya vita ndio hasa mambo yalipoanza kuharibika kwa ile sera ya "Tufunge mkanda". Tuliahidiwa kuwa hali hiyo itakuwa ya muda wa miezi 18 tu. Masikini Watanzania siye tukaamini. Miezi 18 ikapita, miaka 18...28 hadi sasa ni miaka 34. Bado tunaambiwa "kuweni wavumilivu, hali ngumu ya uchumi si Tanzania tu, tupeni muda, tumeanza kuyashughulikia, mikakati kabambe imeanza, uchambuzi yakinifu utafanyika....." Wakati sisi tulianza na kufunga mikanda hadi tumeishia kuzuwia suruali kwa kamba ya mgomba , viongozi wetu mikanda yao imemaliza tundu wanatoboa nyengine; ufanisi utakuja wapi?Kwa watu walioshi miaka ya sitini na ile ya sabini wakati bado kuna siasa za Ujamaa na Kujitegemea, mtakubaliana nami kuwa mambo hayo hayakuwamo miongoni mwa jamii yetu. Yalianza kukua kidogo kidogo mwanzoni mwa miaka ya themanini baada ya vita, na yakaua kwa kasi sana kuanzia mwishoni mwa miaka hiyo ya themanini, ambapo miaka ya leo hii tumefikia mahali ambapo ni alarming sana.
MAMMAMIA.............
Nadhani cha kufanya ni kufumua mfumo huu mzima uliooza na kuanza upya. Tupate viongozi wazalendo, sio watawala na wanyapara tulionao sasa. ......................
na hii ndio manaa inaonekana kama vile wafanyakazi wa serilaki wana mgomo baridi. Mshahara mdogo, watu wana ripoti kazini then wanapotea na mambo yao. Serikali inawakopa wafanyakazi, na wafanyakazi hawatekelezi wajibu wao.
Tunahitaji ku overall civil servants. Ongeza mishahara kwa wafanyakazi, sheria za kazi zisimamiwe na tuache mambo ya hivyo hovyo
Je unajua kuwa kuna watumishi wa serikali wenye mishahara mikubwa sana lakini utendaji wao umejaa rushwa tu?