DAR si LAMU
JF-Expert Member
- Mar 31, 2007
- 2,928
- 544
...Kwenye Elimu. Ukimlipa mwalimu vizuri -kwa maana apate mahitaji yake ya msingi, na kujikita zaidi kwenye kuandaa masomo na kufundisha- utakuwa umeokoa fedha nyingi, kuliko inavyofikiriwa. Can you imagine kiasi cha ujinga utakaofutwa, achilia mbali kuwawezesha vijana skills mbali mbali. We have to see the big picture. Lazima tuwekeze kwenye Elimu. And yes, maslahi bora kwa walimu ni muhimu, sana.Tatizo la Tanzania ni kubwa ziadi ya Ubepari maana Walimu na Madaktari wanataka kujithaminisha wao pasipo mnunuzi kuelewa thamani ya huduma zao. Wakati wa Mwinyi alijaribu kutaka kuwalipa walimu mishahara mizuri, kwa kutoza karo shule za msingi. mwaka uliofuata wanafunzi waliojiandikisha kujiunga na shule hizo iliporomoka kufikia chini ya asilimia 50...ikabidi awamu ya pili ya Mkapa arudishe elimu bure kwa shule hizo. Elimu na Afya sio swala la biashara hata siku moja kwa mtu maskini. Ni necessity - mandatory! tukisha kuwa na uwezo, then inaweza kuwa biashara..
...Kwenye Afya. Daktari yupi mwenye njaa -ingawa hawa wetu hawana- atafanya matibabu vizuri. Je, ataipenda kazi yake? hapa mazingira ya kazi ni muhimu sana [Walimu wanahusika na hili pia] katika kuhakikisha huduma bora inapatikana. Hivi, tunapoteza kiasi gani kutibu watu nje ya nchi? Je, uwekezaji kwenye sekta hii -vifaa, maslahi ya madaktari, na vingine- hauwezi kupunguza gharama hizi, na pengine kutuingizia kipato?
...Huu ni mzigo wa serikali yeyote duniani, ipende isipende, kwa kutoza ada au bila kutoza.