Tukutane hapa kwa walioshindwa ku-root simu zao

Tukutane hapa kwa walioshindwa ku-root simu zao

Japo bado naipenda hii simu yangu
 

Attachments

  • Scr000037.jpg
    Scr000037.jpg
    15.5 KB · Views: 83
Uzi murua sana, ngoja nifuatilie hatua kwa hatua!
Heri yako wewe! Wapo watu, wanaanza kuusoma uzi huu kati kati, na kuanza kuuliza maswali, ambayo huko nyuma yamejibiwa zaidi ya mara kumi! Mi mwenyewe, uzi huu nimeuona Januari mwaka huu, 2018. Nausoma hatua kwa hatua, na maswali yangu, yanapata jibu kila ninapokuwa ninasonga mbele!
Watu waache uvivu. Wajuzi wetu wanachoka kujibu swali hilo hilo walilojibu zaidi ya mara tano huko nyuma!
 
Kuroot redmi 4a maana nimejaribu kingroot nimeshindwa nitumie app gani?
 
Msaada jinsi ya kuroot itel S11 ,maana nimejaribu nimeshindwa
Fuat maelekezo yafuatayo........ Download app ya kingroot kutoka google kwa kutumia browser mfano chrome, ukisha install usiifungue fanya hivi ...........nenda setting then about phone then builid number click hapo haraka harak mpka wakwambie "you are now developers" ........kisha rudi nyuma utakut chin ya accessibilit utakita option inaitw "developer option" fungua then iwashe kisha weka tik kweny usb debugging then rud fungua app ya kingroot start rooting
 
Kuroot simu maana yake ni
kumuezesha au kumpa
mamlaka yote mtuamiaji wa
simu ya android kuongeza,
kupunguza au kurekebisha
mfumo mzima wa android software. Pengine hapo
utakuwa unajiuliza mbona mimi
naweza kutoa au kuongeza apps
au kubadilisha settings za simu
yangu bila hata kuroot simu? Jibu ni kwamba uki root simu
yako ya android utaweza
kufanya mambo mengi sana
kwenye simu yako na kuifanya
simu yako iwe kama wewe
unavyo taka. Mfano, unapo nunua simu yako dukani ikiwa
mpya kabisa na baada ya
kuiwasha utagundua tayari kuna
apps zimekwa kwenye simu na
unapo jaribu kuzitoa huwa
hazitoki. Kwa mfano, simu za samsung huwa zina apps kama (chatOn, S voice, S Planner) na nyinginezo ambazo unakuta
tayari zimeshawekwa kwenye
simu na mdaa mwingine
hauzitaji na ungependa uzitoe
lakini hazitoki. Sasa hapo ndipo
faida moja ya root inapokuja. Ukiwa ume root simu, basi
utaweza kutoa app yoyote mdaa
wowote bila kujali kama
ilikuwepo pale uliponunua simu
yako Faida nyingine ya kuroot ni
kuongeza ufanisi wa simu yako
ya android. Mfano mzuri tazama
picha chini. Picha ya kushoto ni
My files (file manager) ambayo
ipo kwenye simu aina zote za Samsung Galaxy S4. Picha ya
kulia ni file manager ambayo
natumia mimi kwenye samsung
galaxy s4. Sasa utajiuliza
mbona file manager yangu ni
tofauti na ile iliyopo kwenye simu za samsung galaxy s4?
Swali lingine linakuja kwamba
file manager iliyopo upande wa
kulia inatumika kwenye
Samsung Galaxy S6 na S6 edge
pamoja na Note 5. Sasa utajiuliza inawezekana vipi mimi
kutumia file manager iliyopo
kwenye S6 kwenye S4 yangu?
Jibu ni kwamba uki root simu
mambo kama hayo
yanawezekana bila shida. Faida nyingine ni kuipa ulinzi
imara simu yako. Hapa nina
maanisha hata kama simu yako
imeingia baadhi ya apps
ambazo zinahatarisha ulinzi wa
simu yako basi kwa kupitia root utaweza kuziondoa mara moja.
Kwa kweli faida za kuroot simu
zipo nyingi sana. Una weza
search google kuendelea
kuzijua. Sasa tuongelee kidogo baadhi
ya hasara unaweza kuzipata
baada ya kuroot simu yako ya
android. Moja ya hasara kubwa
ni kupoteza warranty. Kumbuka
unaponunua simu dukani hupewa warranty kwamba
endapo simu yako italeta shida
basi utaweza rudisha na
kutengenezewa bure au kupewa
simu nyingine. Endapo uta root
simu yako basi tayari utakuwa umepoteza warrant ya simu
yako. Hasara nyingine unayoweza
kupata baada ya kuroot simu ni
kuaribu simu yako. Zipo simu
nyingi ambazo uki root vibaya
hushindwa kuwaka na
kusababisha hasara kubwa
Nimeelewa sasa
 
Mkuu ungemjibu tu tupate faida, sio wote tunajua
Maandalizi: (i) Charge Simu yako, angalao ijae
kwa 50% (ii) Wezesha ‘’Developer Options”
kwenye simu yako. Menu hii
imefichwa kwa watumiaji wa
kawaida. Sisi tunataka kutumia simu
zetu kwa 100%. Sasa kuifichua nenda
Settings>About phone>Build number. Baadhi ya simu (LG na HTC) nenda
Settings>About phone>Software
information>Build number. Ukishafika
kwenye Build number gusa hapo mara
saba (tap 7 times)…mpaka uambiwe
“You are now a Developer” (iii) Sasa nenda Settings>Developer
options>USB debugging. Weka tiki
hapo (kama haipo) (iv) Nenda
settings>Security>Unknown Sources.
Weka tiki hapo (Kama haipo). Hapo maandalizi yatakua ni tayari.
Sasa download KingRoot 4.0 (or
above) kwa kui search kwenye Google
kisha Install kwenye simu yako. Baada
ya ku install gusa ‘Open’. Baada ya
hapo KingRoot itafunguka na itaitambua simu yako automatically—
Model ya Simu na Toleo lake. (Mf.
Model: H6 Android 4.4.2). Kama simu
yako haijawahi kuwa rooted utaona
‘Root access is unavailable’. Chini
gusa ‘START ROOT’. Hapo KingRoot itakua inakomboa simu yako kutoka
kwenye kifungo cha maisha…kuwa na
subira zoezi hilo litachukua muda
kidogo (sio Zaidi ya dak 6)…mpaka
utakapoona ‘ROOT SUCCSSFULLT’
DONE!!!!! YOU ARE NOW A SUPERUSER…!!!!! -- Ili kuhakikisha kama simu yako
imeshakuwa rooted, nenda PlayStore
kisha download Root Checker. Ukishai
Install na kuifungua gusa ‘VERIFY
ROOT’. Ukiona ‘’Congratulations! Root
access is properly installed on this Device” HAPO KILA KITU TAYARI!!!!! FAIDA ZA KU ROOT SIMU: 1. Utaweza ku update toleo la mfumo
wa simu yako (Kuflash). Mfano kama
unatomia Android 4.4.2 (KitKat)
unaweza kui update kwenda Android
5.0 (Lollipop) Simu ya Android haiwezi
kuflashiwa bila kuwa rooted! 2. Hua inatokea simu kuibiwa. Wewe
unaesoma Makala hii usiibe simu ya
Android siku hizi (ukiokota mtafute
mwenye nayo). Nitafute nikupe story!!
Sasa zipo program nyingi za ku track
simu yako wakati imeibiwa lakini nyingi huondoka kwenye System ya
simu yako baada ya kufanyiwa
‘Factory reset’ au kuflashiwa. Kama
ume root simu yako, zipo Program za
kuitafuta simu yako ambazo hata
mtuhumiwa aiflash au aireset….BADO ITAKUWEPO TU! Mfano wa Program
hizo ni Cerberus. 3. Utakua na uwezo wa kuweka
Program nyingi na nzuri za kuifanya
simu yako iwe fasta na kuboresha
muonekano (performance and
appearance). Pia kuna program za
kutunzia chaji, Kuzuia matangazo kutoka Google (mf. AdAway), n.k….
ambazo hazitafanya kazi bila root MUHIMU;
Rooting inaweza kuharibu kabisa simu
yako na kuifanya isiwake tena!! (Mimi
hapa sitahusika kwa lolote). Usiogope,
hii huwatokea wale wanaokurupuka
na kutofuata maelekezo. Mimi binafsi nishairoot simu yangu na za Marafiki
zangu zisizopungua 20 bila madhara
yoyote kutokea. Fanya utafiti kwanza
ni program gani sahihi ku root simu
yako, omba ushauri,….. Pia Rooting inaharibu Warranty ya
simu yako. Kama ulipewa Warranty
uliponunua simu yako na ukaikuta na
tatizo, ukiirudisha haitakubalika.
Aidha, inawezekana pia ku’unroot’ MWISHO;
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom