Ku root simu

Simeone

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
672
626
Jinsi ya ku �root� simu yako ya Android.
Utangulizi:
Simu zetu za Android zimekua sehemu ya Maisha
yetu ya kila siku. Tunazitumia katika
Mawasiliano, Kuhifadhi kumbukumbu za muhimu,
burudani, biashara, nk. Haya yote hufanywa na
Program ambazo huwekwa kwenye mfumo wa
simu (Operating System). Programu hizo hubeba
maaginzo maalum (Set of instructions) ambazo
humwezesha mtumiaji kufanyia mambo
mbalimbali kutegemea program hio. Mfano wa
program muhimu kwenye simu ni kama vile Opera
Mini (humwezesha mtumiaji kufungua kurasa
mbalimbali za Intaneti), Calculator, nk.
Program hizo huwekwa sio tu kwenye simu, bali
hata vifaa vingine kama vile Computer. Mtumiaji
wa Simu au Computer ndie anaeamua program
ya kuweka kutegemeana na matumizi yake.
Katika miongo michache iliopita zimetengenezwa
program nyingi mpya na zenye maboresho
makubwa na ya kisasa. Ubunifu uliopo katika
program mbalimbali unaleta ukuaji katika Nyanja
mbalimbali katika maisha yetu ya kila siku.
Program hizi pia zimeleta urahisi na ufanisi.
Mfano Calculator, Saa, Vitabu Vitakatifu (Biblia na
Kuran), Kamusi, Camera, nk.. vyote
vimetengenezewa PROGRAM na kuwa rahisi
kuvitumia katika simu muda wowote, mahali
popote.
SASA TUJE KWENYE MADA;
Android ni Mfumo wa simu (Operating System)
ambao unaboreshwa siku hadi siku. Mfumo huu
una majina tofauti kutegeana na toleo lake. Haya
ni Matoleo (Versions) mbalimbali ya Android
kuanzia ya kwanza mpaka ya mwisho;
1. Cupcake (1.5)
2. Donut (1.6)
3. Éclair (2.0 � 2.1)
4. Froyo (2.2 � 2.2.3)
5. Gingerread (2.3 � 2.3.7)
6. Honeycomb (3.0 � 3.2.6)
7. Ice Cream Sandwich (4.0 � 4.0.4)
8. Jelly Bean (4.1 � 4.3.1)
9. KitKat (4.4 � 4.4.4)
10. Lollipop (5.0 � 5.1.1)
Matoleo haya huboreshwa kadri yanavyozidi
kutolewa. Kujua toleo la simu yako nenda
Settings � About phone � Android Version.
Ukikuta Jelly Bean, KitKat au Lollipop hongeara!
kwani unatumia matoleo ya mwisho
yalioboreshwa!!
Mfumo huu wa Android unafaa kufanyiwa settings
mbalimbali na kuwekewa Program mbalimbali ili
kumfanya mtumiaji aifurahie simu yake kwa
asilimia 100, lakini shida huja kwamba sio kila
PROGRAM inayowekwa katika mfumo huu wa
Android inakubali kufanya kazi!! Wapo
watengenezaji wengi wa program (Software
Designers) ulimwenguni. Sasa watengenezaji wa
mfumo huu wa Android wamezuia Program
ambazo hazijatoka kwao zisifanye kazi kwenye
mfumo huo kwa sababu za kimaslahi.
HAPA SASA TUTAPATA KUELEWA MAANA YA KU
�ROOT� kua ni kuifanya simu ikubali Program
zilizozuiwa na watengenezaji wa Android (Android
Developers). Ukishai �root� simu yako sasa
utakua na uwezo wa kuweka program zinazohitaji
�root permission� kwenye simu yako.
JINSI YA KU �ROOT� SIMU YAKO.
Kuna aina za simu ni rahisi sana ku root, lakini
nyingine zinahitaji utafiti wa kina na muda wa
kutosha. Zipo program nyingi sana zinazoweza
kutusaidia zoezi hili. Mojawapo ya Program
ambazo zinajulikana sana kwa ku root simu ni
kama vile KingRoot, Vroot, Kingoapp Root,
SRSRoot, Framaroot, Root Master, z4root,
Universal root, Easy root, nk.. Baadhi ya Program
hizi zitahitaji Computer, nyingine hazihitaji.
Katika Makala hii tutaelekeza kwa kutumia
Program iitwayi KingRoot ambayo inakubali
kufanikisha zoezi hili kwenye asilimia kubwa ya
simu za Android. Program hii haihitaji Computer.
Kuipata nenda Google kisha I isearch na kui
download. Kwa msaada uliza��
Maandalizi:
(i) Charge Simu yako, angalao ijae kwa 50%
(ii) Wezesha ��Developer Options� kwenye
simu yako. Menu hii imefichwa kwa watumiaji wa
kawaida. Sisi tunataka kutumia simu zetu kwa
100%. Sasa kuifichua nenda Settings>About
phone>Build number. Baadhi ya simu (LG na
HTC) nenda Settings>About phone>Software
information>Build number. Ukishafika kwenye
Build number gusa hapo mara saba (tap 7
times)�mpaka uambiwe �You are now a
Developer�
(iii) Sasa nenda Settings>Developer options>USB
debugging. Weka tiki hapo (kama haipo)
(iv) Nenda settings>Security>Unknown Sources.
Weka tiki hapo (Kama haipo).
Hapo maandalizi yatakua ni tayari. Sasa
download KingRoot 4.0 (in MB 6.34) kwa kui
search kwenye Google kisha Install kwenye simu
yako. Baada ya ku install gusa �Open�. Baada
ya hapo KingRoot itafunguka na itaitambua simu
yako automatically�Model ya Simu na Toleo
lake. (Mf. Model: H6 Android 4.4.2). Kama simu
yako haijawahi kuwa rooted utaona �Root
access is unavailable�. Chini gusa �START
ROOT�. Hapo KingRoot itakua inakomboa simu
yako kutoka kwenye kifungo cha maisha�kuwa
na subira zoezi hilo litachukua muda kidogo (sio
Zaidi ya dak 6)�mpaka utakapoona �ROOT
SUCCSSFULLT� DONE!!!!! YOU ARE NOW A
SUPERUSER�!!!!!
--
Ili kuhakikisha kama simu yako imeshakuwa
rooted, nenda PlayStore kisha download Root
Checker. Ukishai Install na kuifungua gusa
�VERIFY ROOT�. Ukiona ��Congratulations!
Root access is properly installed on this Device�
HAPO KILA KITU TAYARI!!!!!
FAIDA ZA KU ROOT SIMU:
1. Utaweza ku update toleo la mfumo wa simu
yako (Kuflash). Mfano kama unatomia Android
4.4.2 (KitKat) unaweza kui update kwenda
Android 5.0 (Lollipop) Simu ya Android haiwezi
kuflashiwa bila kuwa rooted!
2. Hua inatokea simu kuibiwa. Wewe unaesoma
Makala hii usiibe simu ya Android siku hizi
(ukiokota mtafute mwenye nayo). Nitafute nikupe
story!! Sasa zipo program nyingi za ku track simu
yako wakati imeibiwa lakini nyingi huondoka
kwenye System ya simu yako baada ya
kufanyiwa �Factory reset� au kuflashiwa. Kama
ume root simu yako, zipo Program za kuitafuta
simu yako ambazo hata mtuhumiwa aiflash au
aireset�.BADO ITAKUWEPO TU! Mfano wa
Program hizo ni Cerberus.
3. Utakua na uwezo wa kuweka Program nyingi
na nzuri za kuifanya simu yako iwe fasta na
kuboresha muonekano (performance and
appearance). Pia kuna program za kutunzia chaji,
Kuzuia matangazo kutoka Google (mf. AdAway),
n.k�. ambazo hazitafanya kazi bila root
ZINGATIA:
Rooting inaweza kuharibu kabisa kuharibu simu
yako na kuifanya isiwake tena!! (Mimi hapa
sitahusika kwa lolote) Usiogope, hii huwatokea
wale wanaokurupuka na kutofuata maelekezo.
Mimi binafsi nishairoot simu yangu na za Marafiki
zangu zisizopungua 20 bila madhara yoyote
kutokea. Fanya utafiti kwanza ni program gani
sahihi ku root simu yako, omba ushauri,�..
Pia Rooting inaharibu Warranty ya simu yako.
Kama ulipewa Warranty uliponunua simu yako na
ukaikuta na tatizo, ukiirudisha haitakubalika.
Aidha, inawezekana pia ku�unroot�
HITIMISHO:
Kwa yeyote ambae ni mdadisi na mtafiti,
anaependa kusaidiwa na Technologia, kuna
ulazima wa kuroot simu yake. Baada ya Makala
hii, wale woote ambao tutaenda sambamba
tutaanza kupitia Programs nyingi ambazo
zinahitaji �Root Permission�. Mie natumia
Tecno H6, baada ya kui root nimeifanyia Settings
nyingi sana na ninaitumia katika mambo mengi
sana!! ROOTING imeniwezesha hata kubadilisha
muonekano wa maandishi system nzima!!
 
Nina simu tecno camon CX naomba link ya app ya kuroot nilishajaribu king root mara kadhaa akashindikana,nilishawahi kuroot tecno C5.
 
Angalizo

Kuroot simu ni hatari yawezekana ikazima mazima isiwake tena kabisa
 
Na hakuna umuhimu wa kuroot kwa sababu hataapp ulizowekewa hujazitumia bado
 
Back
Top Bottom