Hckcode8
JF-Expert Member
- Apr 25, 2016
- 370
- 245
Jinsi ya ku ‘root’ simu yako ya Android.
Utangulizi:
Simu zetu za Android zimekua sehemu ya
Maisha yetu ya kila siku. Tunazitumia katika
Mawasiliano, Kuhifadhi kumbukumbu za
muhimu, burudani, biashara, nk. Haya yote hufanywa na Program ambazo huwekwa
kwenye mfumo wa simu (Operating System).
Programu hizo hubeba maaginzo maalum (Set
of instructions) ambazo humwezesha mtumiaji
kufanyia mambo mbalimbali kutegemea program
hio. Mfano wa program muhimu kwenye simu ni kama vile Opera Mini (humwezesha mtumiaji
kufungua kurasa mbalimbali za Intaneti),
Calculator, nk.
Program hizo huwekwa sio tu kwenye simu, bali
hata vifaa vingine kama vile Computer.
Mtumiaji wa Simu au Computer ndie anaeamua program ya kuweka kutegemeana na matumizi
yake. Katika miongo michache iliopita
zimetengenezwa program nyingi mpya na
zenye maboresho makubwa na ya kisasa.
Ubunifu uliopo katika program mbalimbali
unaleta ukuaji katika Nyanja mbalimbali katika maisha yetu ya kila siku. Program hizi pia
zimeleta urahisi na ufanisi. Mfano Calculator,
Saa, Vitabu Vitakatifu (Biblia na Kuran), Kamusi,
Camera, nk.. vyote vimetengenezewa
PROGRAM na kuwa rahisi kuvitumia katika simu
muda wowote, mahali popote. SASA TUJE KWENYE MADA;
Android ni Mfumo wa simu (Operating System)
ambao unaboreshwa siku hadi siku. Mfumo huu
una majina tofauti kutegeana na toleo lake.
Haya ni Matoleo (Versions) mbalimbali ya
Android kuanzia ya kwanza mpaka ya mwisho; 1. Cupcake (1.5)
2. Donut (1.6)
3. Éclair (2.0 – 2.1)
4. Froyo (2.2 – 2.2.3)
5. Gingerread (2.3 – 2.3.7)
6. Honeycomb (3.0 – 3.2.6) 7. Ice Cream Sandwich (4.0 – 4.0.4)
8. Jelly Bean (4.1 – 4.3.1)
9. KitKat (4.4 – 4.4.4)
10. Lollipop (5.0 – 5.1.1)
Matoleo haya huboreshwa kadri yanavyozidi
kutolewa. Kujua toleo la simu yako nenda Settings – About phone – Android Version.
Ukikuta Jelly Bean, KitKat au Lollipop hongeara!
kwani unatumia matoleo ya mwisho
yalioboreshwa!!
Mfumo huu wa Android unafaa kufanyiwa
settings mbalimbali na kuwekewa Program mbalimbali ili kumfanya mtumiaji aifurahie simu
yake kwa asilimia 100, lakini shida huja kwamba
sio kila PROGRAM inayowekwa katika mfumo
huu wa Android inakubali kufanya kazi!! Wapo
watengenezaji wengi wa program (Software
Designers) ulimwenguni. Sasa watengenezaji wa mfumo huu wa Android wamezuia Program
ambazo hazijatoka kwao zisifanye kazi kwenye
mfumo huo kwa sababu za kimaslahi.
HAPA SASA TUTAPATA KUELEWA MAANA YA
KU ‘ROOT’ kua ni kuifanya simu ikubali Program
zilizozuiwa na watengenezaji wa Android (Android Developers). Ukishai ‘root’ simu yako
sasa utakua na uwezo wa kuweka program
zinazohitaji ‘root permission’ kwenye simu yako.
JINSI YA KU ‘ROOT’ SIMU YAKO.
Kuna aina za simu ni rahisi sana ku root, lakini
nyingine zinahitaji utafiti wa kina na muda wa kutosha. Zipo program nyingi sana zinazoweza
kutusaidia zoezi hili. Mojawapo ya Program
ambazo zinajulikana sana kwa ku root simu ni
kama vile KingRoot, Vroot, Kingoapp Root,
SRSRoot, Framaroot, Root Master, z4root,
Universal root, Easy root, nk.. Baadhi ya Program hizi zitahitaji Computer, nyingine
hazihitaji.
Katika Makala hii tutaelekeza kwa kutumia
Program iitwayi KingRoot ambayo inakubali
kufanikisha zoezi hili kwenye asilimia kubwa ya
simu za Android. Program hii haihitaji Computer. Kuipata nenda Google kisha I
isearch na kui download. Kwa msaada uliza……
Maandalizi:
(i) Charge Simu yako, angalao ijae kwa 50%
(ii) Wezesha ‘’Developer Options” kwenye simu
yako. Menu hii imefichwa kwa watumiaji wa kawaida. Sisi tunataka kutumia simu zetu kwa
100%. Sasa kuifichua nenda Settings>About
phone>Build number. Baadhi ya simu (LG na
HTC) nenda Settings>About phone>Software
information>Bui ld number. Ukishafika kwenye Build number gusa hapo mara saba
(tap 7 times)…mpaka uambiwe “You are now a
Developer”
(iii) Sasa nenda Settings>Develo per options>USB debugging. Weka tiki hapo (kama
haipo)
(iv) Nenda settings>Securi ty>Unknown Sources. Weka tiki hapo (Kama haipo).
Hapo maandalizi yatakua ni tayari. Sasa
download KingRoot 4.0 (in MB 6.34) kwa kui
search kwenye Google kisha Install kwenye
simu yako. Baada ya ku install gusa ‘Open’.
Baada ya hapo KingRoot itafunguka na itaitambua simu yako automatically—M odel ya Simu na Toleo lake. (Mf. Model: H6 Android
4.4.2). Kama simu yako haijawahi kuwa rooted
utaona ‘Root access is unavailable’. Chini gusa
‘START ROOT’. Hapo KingRoot itakua
inakomboa simu yako kutoka kwenye kifungo
cha maisha…kuwa na subira zoezi hilo litachukua muda kidogo (sio Zaidi ya dak 6)…
mpaka utakapoona ‘ROOT SUCCSSFULLT’
DONE!!!!! YOU ARE NOW A SUPERUSER…!!!!!
--
Ili kuhakikisha kama simu yako imeshakuwa
rooted, nenda PlayStore kisha download Root Checker. Ukishai Install na kuifungua gusa
‘VERIFY ROOT’. Ukiona ‘’Congratulatio ns! Root access is properly installed on this Device”
HAPO KILA KITU TAYARI!!!!!
FAIDA ZA KU ROOT SIMU:
1. Utaweza ku update toleo la mfumo wa simu
yako (Kuflash). Mfano kama unatomia Android
4.4.2 (KitKat) unaweza kui update kwenda Android 5.0 (Lollipop) Simu ya Android haiwezi
kuflashiwa bila kuwa rooted!
2. Hua inatokea simu kuibiwa. Wewe unaesoma
Makala hii usiibe simu ya Android siku hizi
(ukiokota mtafute mwenye nayo). Nitafute
nikupe story!! Sasa zipo program nyingi za ku track simu yako wakati imeibiwa lakini nyingi
huondoka kwenye System ya simu yako baada
ya kufanyiwa ‘Factory reset’ au kuflashiwa.
Kama ume root simu yako, zipo Program za
kuitafuta simu yako ambazo hata mtuhumiwa
aiflash au aireset….BADO ITAKUWEPO TU! Mfano wa Program hizo ni Cerberus.
3. Utakua na uwezo wa kuweka Program nyingi
na nzuri za kuifanya simu yako iwe fasta na
kuboresha muonekano (performance and
appearance). Pia kuna program za kutunzia
chaji, Kuzuia matangazo kutoka Google (mf. AdAway), n.k…. ambazo hazitafanya kazi bila
root
ZINGATIA:
Rooting inaweza kuharibu kabisa kuharibu simu
yako na kuifanya isiwake tena!! (Mimi hapa
sitahusika kwa lolote) Usiogope, hii huwatokea wale wanaokurupuka na kutofuata maelekezo.
Mimi binafsi nishairoot simu yangu na za
Marafiki zangu zisizopungua 20 bila madhara
yoyote kutokea. Fanya utafiti kwanza ni
program gani sahihi ku root simu yako, omba
ushauri,….. Pia Rooting inaharibu Warranty ya simu yako.
Kama ulipewa Warranty uliponunua simu yako
na ukaikuta na tatizo, ukiirudisha haitakubalika.
Aidha, inawezekana pia ku’unroot’
HITIMISHO:
Kwa yeyote ambae ni mdadisi na mtafiti, anaependa kusaidiwa na Technologia, kuna
ulazima wa kuroot simu yake. Baada ya Makala
hii, wale woote ambao tutaenda sambamba
tutaanza kupitia Programs nyingi ambazo
zinahitaji ‘Root Permission’. Mie natumia Tecno
H6, baada ya kui root nimeifanyia Settings nyingi sana na ninaitumia katika mambo mengi
sana!! ROOTING imeniwezesha hata
kubadilisha muonekano wa maandishi system
nzima!!