Tukumbushane watu wa Tabora-Mboka Manyema

Tukumbushane watu wa Tabora-Mboka Manyema

Hatari sanaaa,kitu mboka mbokaaaaa,me nimeishi pale pia hapo juzi tu 2011-2014.Niliishi bachu jirani na shule ya msingi inaitwa Tauni skuli,pia niliishi isevya then ipuli bonana.Jimama zima lilinipenda daaa liliniteka sn,linanipa papuchi balaa.Hapo watoto wa uhazili na SAUT duu ni ngozi tu
I LOVE MBOKA,NITAENDA TEMBEA KIDOGO.
 
Tabora-Mboka Manyema
Tabora schools,shule za mapinduzi............Warswa and Berlin........Wakuu nakumbuka pale Orchard
 
Ukiwa unaenda kiloleni kupitia chekeni au checkline ya kiloleni na rufita clab kuna mzee alikuwa anaitwa Papaa Wemba alimuuzia msukuma Msikiti wa ijumaaa mzee akatoa pesa za mnadani za ng'ombe siku anaenda juwaonesha watoto wake akakuta watu wanaswali weeee ikawa noma mzee kaambiwa aliyemuuzia ana cheti cha wehu.

Papaa wemba alikuwa na gari lake linapeleka watu Nsororo mkifika njiani anawashusha mcheze mziki ukuweza kukata kiuno unaingia kwenye gari.
Mnakumbuka magari ya kazuge!!kaserekandis!! Niache nilivyo!!
Mnamkumbuka mzee Nyembo wa ipuli R.I.P .

Mboka noma.
 
Dah.. Wish sehem zote nizifaham, nikisikia stori hizi nakumbuka mbali sana, isevya rest in peace bibi na babu.. Stori nyingi humu huwa naziskia kwa mama n wakubwa zangu wakizungumzia.. I wish n mimi ningekuwa nachangia.. Rest in peace dad mzee mgumia, nikipata stor za tabora nakukumbuka mzee wangu..
 
Miaka ya 80's mwanzoni nilipata kuishi Tabora Mjini,baadae nikaja kusoma Tabora Boys miaka ya 90's....leo nimekumbuka maisha ya Tabora,Ujio wa Baba Mtakatifu,enzi za ukuu wa Mkoa Ndugu Gama....Timu ya mpira ya Milambo chini ya akina Job Ayoub "kwasakwasa",Quresh Ufunguo,Dadi Phares,Hamad Mwinyimkuu,Abas Mchemba na Bubu fulani alikuwa na mashuti sana wengine siwakumbuki Matajili wa wakati huo ni matajili wa mbao wakiitwa "Digala",kuna jamaa alikuwa tajili wa mbao mitaa ya Kiyungi karibu na Filter akiitwa Fifi(sijui kama yu hai)...mitaa ya ng'ambo mtaa wa Rehani alikuwepo Mavyombo,Msabaha...!kulikuwa na kina Said Kindamba,Waarabu wa Kwihara na Mrema wa Cheyo!...Miaka hiyo Tabora ilisifika kwa kuwa na Majambazi hatari,wengi wakitokea mitaa ya Ng'ambo..kuna jambazi mmoja walimkata mguu ili aache kuiba akawa anatembea na gongo(nimemsahau jina),Vichaa(wehu) wa kutosha na maarufu kama Athumani Nuna,Super Tall,Aman n.k...Mitaa ya wajanja ilikuwa National na Cheyo!!Misosi kama ugali muhogo,makopa,mawese na ngazi...Vipi nani wa Tabora anipe update za leo?mda sijafika Chemichemi,Gongoni,Bachu,Kanyenye,Kiloleni,Isevya,K'koo,Mwanza Road na Ipuli....Wapi vijana wa enzi hizo wa Mboka Manyema?
Eeeeee bwana wewe,hebu achana na hii story yako ya kahawa miaka nenda rudi,unatujazia kurasa,kumbusha watu mambo ya maendeleo na dini,sio kila kukichwa kuongelea wehu na majmbazi ya zamani Tabora,eboooo.
 
Ukiwa unaenda kiloleni kupitia chekeni au checkline ya kiloleni na rufita clab kuna mzee alikuwa anaitwa Papaa Wemba alimuuzia msukuma Msikiti wa ijumaaa mzee akatoa pesa za mnadani za ng'ombe siku anaenda juwaonesha watoto wake akakuta watu wanaswali weeee ikawa noma mzee kaambiwa aliyemuuzia ana cheti cha wehu.

Papaa wemba alikuwa na gari lake linapeleka watu Nsororo mkifika njiani anawashusha mcheze mziki ukuweza kukata kiuno unaingia kwenye gari.
Mnakumbuka magari ya kazuge!!kaserekandis!! Niache nilivyo!!
Mnamkumbuka mzee Nyembo wa ipuli R.I.P .

Mboka noma.
Baaasi hayo tu,umemaliza?,au kahawa imekwisha?
 
Dah.. Wish sehem zote nizifaham, nikisikia stori hizi nakumbuka mbali sana, isevya rest in peace bibi na babu.. Stori nyingi humu huwa naziskia kwa mama n wakubwa zangu wakizungumzia.. I wish n mimi ningekuwa nachangia.. Rest in peace dad mzee mgumia, nikipata stor za tabora nakukumbuka mzee wangu..
Jamila Mgumia una mfahamu?
 
Kwa sie watu wa sports hatutowasahau Abasi mchemba,Saidi Mwamba,Kasangax,Luaga,Kagoma...hawa wote walitangulia mbele ya haki,,,Tbr ilikua juu na tamu ki soka enzi hizo nikisoma mihayo sec school pamoja na akina Prince Baina ,Ibrahim karenga.Ebby,Wiliam anyosisye,Ben ngozi na wengineo
 
Acha pumba, kama huelewi kitu ujue hakikihusu
Nafikiri wewe akili yako imejaa pumba zilizoungua,ooh mboka kulikuwa na chizi huyu na yule,oooh kulikuwa na muuza mihogo shule ya uyui,oooh kulikuwa na bubu pale sinema ya diamond,ooh kulikuwa na uwanja wa chipukizi,ooh sijui jambazi sugu Kandege,ooh Jetha muhindi alikuwa mwehu,oooh Roshi alikuwa mwehu,oooh Malingumu alikuwa mwehu,sasa wewe uliekimbia umande huna jingine?,kila siku ooh tujikumbushe Mboka,hiyo mboka imedorora kama nyasi zilizokauka,sababu ya majungu,ushirikina,ujambazi na kahawa na kucheza bao baaaaaasi,na yote hiyo imesababishwa na maupuuzi kama hayo,laiti ungekuwa na mawazo ya maendeleo usingekalia upupu unaotuletea marabuku.
 
Jamila Mgumia una mfahamu?
Hapana mkuu, ila nina uhakika atakuwa ni ndugu yangu, kibaya niliondoka tabora mdogo toka 98 sikurud tena hadi mwaka huu, nmefanya kama kupita kwenda urambo katika mazishi ya kaka yangu.. anaweza akawa ananijua, mie sikukaa sana upande wa faza wangu, but i wish niwajue ndugu zangu, naskia tupo wengi kupita maelezo
 
Nilikuwa naishi jirani na bar ya kwa sonda na dr kisengi cjui kisenge.
 
Simbamwene tulikuwa tunaenda kuangua zambalau na embe boribo juu ya makaburi...vp umekuwa mji?ha ha ha ha ha ha umenikumbusha Mwajuma Ringa?ivi kwanini Mboka Manyema vichaa wengi?...dah Hamis Mambwa aliogopwaje?Diamond near by TMP uwanja wa Chipukizi?ukumbi wa Disco hapo Mwanaisungu geti la kuingia Uhazili...video tunangalizia Maua Bar Opposite na Central Police


Dah yaani umenikumbusha mbali sana Maua Bar, Mwanaisungu na Kuna Mwarabu pia alikua anaonesha video kwake nimemsahau jina
 
nakumbuka tukio la mabehewa ya petroli kuwaka moto pale stesheni..kilikuwa kipindi cha vita ya ghuba,basi tukajua marekani na saddam wameanza kukinukisha na huku tayari.....lol!

Wakati mabehewa ya mafuta yanawaka mi nilikua Kigwa makazi ya wakimbizi na moto tuliuona tukajua kimenuka
 
Tabora hotel,Railway station,TMP,Uhaziri college,Cheyo,Rufita club Kiloleni,Filter,Ttc,Railway college,Tabora Boys/Girls,Kazima,Uyui,Mihayo,Milambo Sec Schools...Kiwanda cha nyuzi
 
Back
Top Bottom