Dah,ingawa mimi sio zamani saana,lakini kiukweli umenikumbusha mabali sana...Miaka ya 90 kila mtaa taarab,anaolewa mtu leo baada ya miezi mitatu unasikia taarab kwao anaolewa tena... enzi hizo bendi ya mashujaa inavuma sana.Ndio baadaya maswezi yakaingia na kushika kasi mjini,unaambiwa ukiingia kucheza tu lazima uondoke nao! Nakumbuka ugomvi baina ya Tabora boys na Milambo boys...Nakumbuka wakati huo Wanafunzi wa Uyui wanaonekana mabishoo kuliko shule zote...Wakati huo mimi nasoma Mirambo TPDF ambayo baadaye ilikuja kuwa Unyanyembe..
Enzi zangu ni kipindi cha akina Yahya Akilimali wakati huo kulikuwa na kombe la Mgulunde..dogo alikuwa aknapiga vyenga huyo,wacha kabisa...Timu kali zilikuwa Tabora Boys na Milambo Boyz.Nakumbuka Chuo cha Reli ambacho baadaye kilikuja kufa..
Wakati huo ikisemekana kuwa Tabora ilikuwa miongoni mwa mikoa yenye warembo wakali(lkn sio miss tz!),unakuta mtoto mkali,lakinin fuatilia anapotokea sasa,ndio utashangaa...Wakati huo washua wanatokea Cheyo na National,hapo kabla ya Ally H. Mwinyi na Ipuli.Mitaa kama mwanza road,mabatini,bomba mzinga,matakini,chemchem,minazi mikinda,mbugani,nk. ilikuwa inafahamika kama mitaa ya watu wa hali ya chini!
Wakati ule daladala za nini,wakati kila mtu anamiliki baskeli?! Mnakumkumbuka TX(kwa sasa ni marehemu) pale stend kuu ya zamani?Kuli alikuwa mkorofi huyo,wacha kabisa.
Dah,Tabora... ingawa nipo mbali lakini nakumis sana,ipo siku nitarudi tu nyumbani..I love You Tabora.
Mkuu umenikumbusha mbali sana...mwehu maarufu enzi zile alikuwa anaitwa malingumu mzee mmoja kichaa alikuwa soko kuu, mimi nilizaliwa ng'ambo mtaa maarufu unaitwa kwihara street, baba yangu alikuwa ana shamba kijiji cha usenge karibu na jumba la makumbusho(livingstone)...pale kwihara kulikuwa na waarabu kina zahoro nasikia aliuza ile ardhi kwa chuo cha st augustine au tumaini university......ujio wa papa binafsi ulinigusa sana nilikuwa mdogo ila kwa kweli papa John Paul II alikuwa charismatic...na kwa kweli huko alipo ni mtakatifu...jet yake ilitua uwanja wa tabora wa vumbi, tukiwa nyumbani mida ya saa tisa hivi tulishangaa ndege nyeupe ina mlio mkali(jet) ikitua....majambazi niliokuwa na wakumbuka mimi ni kina mohamed romba...pale ng'ambo kulikuwa na mpakistan mmoja na familia yake alikuwa anaitwa Nuru din alikuwa na wasichana mabinti wareeembo...hakika maisha ni safari yenye uchungu sana kwa sisi tuliopitia mambo magumu....kanisa katoliki ilikuwa ni nguzo muhimu ...namkumbuka marehemu padre John Mageda, ndiye alinibatiza......akikuwa anajua sana kuimba zile sala za ekaristi takatifu...bwaaana awe naaaanyiiiiiii, inuuueeeeeniiii mioyooooooooooo! tumeinuuua kwa bwanaaaaa! mimi nilisoma Uyui sekondari
Mimi sio mwenyeji wa Tabora ila hiyo Bustani ya wanyama naikumbuka,kulikua na Simba walimwita jina la Mlungush, mpaka leo sijui hata nini maana ya hilo jinaFamilia ya Dr Kobelo wengi walifariki,akiwepo Dr mwenyewe,mkewe na yule mtoto wao aliyekuwa ana akili sana baadae akawa chizi ,Yule alikuwa anatembea kama amekata centre bolt ya bega la kushoto alikuwa anaitwa Steve. Thobias baadae ya kufungwa alirudi uraiani na mara ya mwisho nilisikia anapiga tempo pale Orion Tabora Hotel, sasa sijui kama bado yupo hapo maana mwaka jana mmiliki wahoteli hiyo Bw POLLE a.k.a Kanyenyela alifariki dunia pia.
Mnaikumbuka ile bustani ya wanyama kule national? Nasikia ilishafungwa siku hizi. Nilikwenda Mboka mwaka juzi sikubaliani na nyie kuwa mji haubadiriki kimaendeleo maana nimeshuhudia majumba ya kufuru Mitaa ya mihogoni kule kama unakwenda kiwanda cha tumbaku Miemba na maeneo ya Ipuli na Cheyo. Kweli maendeleo siyo ya haraka lakini tunajikongoja taratibu.
Mlungushi...umenikumbusha mbali sana...alikua akiunguruma kila asubuh..national yote mnamsikiaMimi sio mwenyeji wa Tabora ila hiyo Bustani ya wanyama naikumbuka,kulikua na Simba walimwita jina la Mlungush, mpaka leo sijui hata nini maana ya hilo jina
Pia kulikua na basi linaitwa Mtoto wa nyumbani lilikuwa ninafanya safari za Tabora - Shinyanga,Basi lingine ni Azaiz transport.Mlungushi...umenikumbusha mbali sana...alikua akiunguruma kila asubuh..national yote mnamsikia
Hahahaaaa!! Nimecheka sana aisee!! Wanchoma kumoyo ndio hivyo vilikua vikiitwa "Mokas?" Mtu anaweka kichuma chini ya soli ili akitembea kitoe sauti "Kwa! Kwa! Kwa!" Hahahaaaaaaaa!!Mimo nakumbuka polisi walivyopIga marufuku viatu vilivyochongoka kuviita "WANCHOMA"
Wanchoma kumoyo ni kiatu kilichochongoka mbele....not necessarily kiwe na kichuma chini wakati wa kutembea kinapiga kelele. Mokasini ni kiatu aina ya kokoko lakini ni kiatu cha kiume.Hahahaaaa!! Nimecheka sana aisee!! Wanchoma kumoyo ndio hivyo vilikua vikiitwa "Mokas?" Mtu anaweka kichuma chini ya soli ili akitembea kitoe sauti "Kwa! Kwa! Kwa!" Hahahaaaaaaaa!!
Mzee Mgumia Waziri wa Maliasili enzi za Mwinyi,Akiitwa Aboubakari Mgumia,akawa Mbunge wa Tabora Mjini 1990-1995 nikiwa Tabora.Dada yake Mwalimu Mgumia alikuwa Mwalimu wangu.Walikuwa na nyumba ng'ambo karibu na soko kuu la Ng'ambo!!Ukoo mkubwa sana huu TaboraDah.. Wish sehem zote nizifaham, nikisikia stori hizi nakumbuka mbali sana, isevya rest in peace bibi na babu.. Stori nyingi humu huwa naziskia kwa mama n wakubwa zangu wakizungumzia.. I wish n mimi ningekuwa nachangia.. Rest in peace dad mzee mgumia, nikipata stor za tabora nakukumbuka mzee wangu..
Dah.. Broo uko wapi!? Umechelewa kidogo tu nilikuwa huko kwa wiki km 3 hv au 4, nahisi tungeonana.. Nmezunguka maeneo mengi sana, kiukweli furaha yangu haielezek, japo watoto wengi wa huko historia hawaijui.. Unamchukua bodaboda akuzungushe maeneo maswali mengi ukimuuliza anakwambia hajui au yee mgeni..Mzee Mgumia Waziri wa Maliasili enzi za Mwinyi,Akiitwa Aboubakari Mgumia,akawa Mbunge wa Tabora Mjini 1990-1995 nikiwa Tabora.Dada yake Mwalimu Mgumia alikuwa Mwalimu wangu.Walikuwa na nyumba ng'ambo karibu na soko kuu la Ng'ambo!!Ukoo mkubwa sana huu Tabora
Hahahhaa hii thread nouma!! inanikumbusha life la Tabora wakuu, maeneo ya Ng'ambo kwenye pilau usiku usiku!! Tukutuku kuchota maji, kwa Sonda kucheki UEFA, hahaha nilikuwapo miaka 10 hadi 12 iliyopita wakuu pale Tabora Boys.
Mwanaisungu ilishagakufa mkuu....
Kuna siku moja, enzi hizo tukipewa masurufu (mikate na juice) wakati wa likizo likaja behewa toka tupu toka mwanza kwa ajili ya wanafunzi wa tabora waliokuwa wanakwenda dom, moro, singida, dar n.k. Kukawa na purukushani kidogo nani mlengwa wa behewa hilo kati ya milambo, girls, boys au ttc. Jamaa mmoja wa milambo akachukua mkate akaenda akafuta maneno ubavuni mwa behewa na kuandika 'A lecole sencodre de milambo'. Basi watu weweeeee
Sasa hivi ni mkubwa sana.kwenye vichaa hapo umemsahau makamba jeki bana!........jamaa mmoja alikua kibarua maarufu tunamuita fulu saba......anapeleka pwani huyoooo!!!!nakumbuka nikiwa 'kinda' tu mwanajeshi mmoja aliuawa majaruba ya isevya kutokea stesheni pale.......basi 'wajeda' wakaenda zika mtu wao kimya kimya halafu wakaingia mtaani sasa.......weee....wiki nzima msako,waliokuwa watuhumiwa wa hata udokozi miaka ile walikufa vibaya kwa singe na vipigo vya washkaji,vilio vikatawala mji mzima na amani ya hata kulala mlango wazi ikarejea!
FIFI alikuwa anatuhumiwa kuwaambukiza ukimwi dada zetu kwa makusudi,one day alionekana mitaa ya kwetu na dada mmoja wa pale pale mtaani kwetu anaitwa Tatu Mazegembe........alikuwa na makalio makubwa huyooo wacha.........basi wacha tumtoe nduki na mawe huku tunamwambia yule dada 'unaenda kufa wewe!!!'......aaaaa mboka matata wee.....mji wangu wa utotoni uliokataa kukua!
Mkuu rudi nyumbani kumenogaDah,ingawa mimi sio zamani saana,lakini kiukweli umenikumbusha mabali sana...Miaka ya 90 kila mtaa taarab,anaolewa mtu leo baada ya miezi mitatu unasikia taarab kwao anaolewa tena... enzi hizo bendi ya mashujaa inavuma sana.Ndio baadaya maswezi yakaingia na kushika kasi mjini,unaambiwa ukiingia kucheza tu lazima uondoke nao! Nakumbuka ugomvi baina ya Tabora boys na Milambo boys...Nakumbuka wakati huo Wanafunzi wa Uyui wanaonekana mabishoo kuliko shule zote...Wakati huo mimi nasoma Mirambo TPDF ambayo baadaye ilikuja kuwa Unyanyembe..
Enzi zangu ni kipindi cha akina Yahya Akilimali wakati huo kulikuwa na kombe la Mgulunde..dogo alikuwa aknapiga vyenga huyo,wacha kabisa...Timu kali zilikuwa Tabora Boys na Milambo Boyz.Nakumbuka Chuo cha Reli ambacho baadaye kilikuja kufa..
Wakati huo ikisemekana kuwa Tabora ilikuwa miongoni mwa mikoa yenye warembo wakali(lkn sio miss tz!),unakuta mtoto mkali,lakinin fuatilia anapotokea sasa,ndio utashangaa...Wakati huo washua wanatokea Cheyo na National,hapo kabla ya Ally H. Mwinyi na Ipuli.Mitaa kama mwanza road,mabatini,bomba mzinga,matakini,chemchem,minazi mikinda,mbugani,nk. ilikuwa inafahamika kama mitaa ya watu wa hali ya chini!
Wakati ule daladala za nini,wakati kila mtu anamiliki baskeli?! Mnakumkumbuka TX(kwa sasa ni marehemu) pale stend kuu ya zamani?Kuli alikuwa mkorofi huyo,wacha kabisa.
Dah,Tabora... ingawa nipo mbali lakini nakumis sana,ipo siku nitarudi tu nyumbani..I love You Tabora.
Yomba dada, mwakapela kukaya inywi bhasulaI love u tabora, wakulugo.
Ye-ye-ye...mwanakadimu!