Tukumbushane Nyimbo za Bongo Flava Zilizotamba enzi za 2000-2008

"hivi ni vituko uswahili,uswahilini kuna vitukoo"
mchizi gani yule aliimba hii kitu?
Suma g ama nani?
 
hapa ndo napopapenda. back in days kuna machz kama joint mobb, wateule, big dogg poz, big loud family. n2p, solid ground, free dogz camp, manzese cru, zig zag fam, Nes.noiz etc hawa jamaa dnt knw wako wapi? always naupenda wimbo wa mtulize wa mabaga fresh na necha kipindi kile necha na walumendago family. dah! michano ya zahran na complex i cnt stand lovn them. kuna mchz wa hbc anaitwa terry fanani hv yuko wapi?
 
Dah! Nakumbuka Kibanda cha simu ya Soggy Doggy,Kama unataka demu ya J-mo,Mabinti ya Mwana Fa,Raha tu ya AY,Tanga kunani ya Wagosi na Mi mmasai ya Mr. Ebbo. Zipo kibao!!
Dah! Nakumbuka Solothang wakati anasumbua na wimbo wake wa 'mambo ya pwani'.
 
Nikizipata mbona itakuwa noma! nikizipata mbona wanga wenigi wata koma! Hivi aliimba nani?
 
vina utata wa solo thang,tunasonga kwa mwendo wa farasi au kinyonga tunasonga wa hashim dogo mwendawazim na kikosi,maisha ya boarding jmoe ft dully,ingekua vipi jmoe ft FA
 
Jamani tuongee ukweli.kulikuwa na ngoma kali sana zenye ujumbe kuliko sasa.
1.nyalu land-mike T
2.wauguzi-wagosi
3.ingekuwa vipi-FA
4.haturap-FA
5.posta -........,
6.mtazamo
7.sister sister-GK
8.vumilia etc
 
Jamani tuongee ukweli.kulikuwa na ngoma kali sana zenye ujumbe kuliko sasa.
1.nyalu land-mike T
2.wauguzi-wagosi
3.ingekuwa vipi-FA
4.haturap-FA
5.posta -........,
6.mtazamo
7.sister sister-GK
8.vumilia etc

posta-sonell
mtazamo-afande
vumilia-uvc
 
Nilimpenda solo kwenye mtazamo wa afande sele, au ule wimbo wake wa simu yangu na soggy doggy.
Solo noumaaaaaaaaa! msikilize kwenye ile nyimbo na feruzi unaoitwa boss kama sikosei! alishuka verse hatari hasa alipo pause ki hip hop pale aliposema "anhaaa chana karatasi" ni maneno marahisi lakini namna alivyounganisha maneno lazima umkubali.
 
Ni Buzz Double Seven, Six Nine Zero,
Piga namba hii popote uliza Solo,
Ila kama ni kimeo usipige kwani Mgogoro,
Hata kama niko Dar, nitajibu niko Moro,

Wananiita Solothang a.k.a "Not Reachable"
Hapo simu nishazima natafutwa na vinabo
Wakiiba hii moja tu nanunua double!!
 
Ni Buzz Double Seven, Six Nine Zero,
Piga namba hii popote uliza Solo,
Ila kama ni kimeo usipige kwani Mgogoro,
Hata kama niko Dar, nitajibu niko Moro,

Wananiita Solothang a.k.a "Not Reachable"
Hapo simu nishazima natafutwa na vinabo
Wakiiba hii moja tu nanunua double!!


Mkuu kuna namba umeruka hapo...
Double seven, six, nine zero = 77690

Anasema ni Buzz two, Double seven, six, nine, zero......ambayo ni 277690
 
simu yangu ni soo
Kuishika mtu sikubali
Hata niwe na demu wangu
Simu yangu ntaiweka mbali
Na schelewi kuizima
Nkaiwasha nkiachana nae
Najuwa ikiwa hewani
Nitagombana nae
Simu yangu inakuwa Dafatari
La kuhifadhia mistari
Una create folder kama msg za siri
wapendao kubip
Hapa mtaliwa dola
Pembeni natumia beeper
Chunga ntakutia hasara
Sinunui simu Dukani
Simu zangu zote mazabe
Yenye ndogo thamani
ili machizi wasiibe
Wameiba 6210
Sasa niko na Blue 1
Wamentoa Finland
Sasa niko Japan
Buzz 272519
Sms zinakwenda
Wakati pesa zimekwisha
Lakini sometimes
Inanipa wendawazimu
Dola tano tano
Zinapoisha mi sina hamu...

Jay Moe ni habari nyingine kwa kweli...
Live longer kamanda...
 
yo nataka demu lakini tuanzie makumbusho
Awe mfano wa Fifi madada zangu waitwe wifi
Sio Nkinde, sio Leilah mtaa wao wa miyeyusho

Dah Juma ni yuleyule...
Tangu enzi ileeee mpaka leo ukimuendea hovyo anakukalisha...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom