Tukumbushane Album bora za wasanii wa Bongofleva

screpa

JF-Expert Member
Sep 10, 2015
10,792
15,693
Muziki wa Bongofleva tangu uanze miaka ya 90 mwishoni umefanikiwa kuibua majina mengi makubwa, lakini tofauti na ilivyo sasa kipindi huu muziki unaanza ilikuwa ili utoboe ni lazima uwe na album. Utamaduni huu wa kutoa album ulipoteza umaarufu kuanzia kwenye miaka ya 2009 hivi ambapo wasanii wamekuwa wakilalamika mauzo kuwa hafifu kutokana na kuibuka wazee wa kudurufu kazi hizo na kuziuza kwa bei chee mtaani, pia mitandao ya kijamii imeathiri kwa kiasi kikubwa mauzo ya album. Baada ya kusema hayo machache tukumbushane wasanii waliofanikiwa kutoa album na majina ya album hizo, wasanii waliowahi kutoa album zikafanya vizuri ni kama Mr II 'Sugu', Profesa Jay Dudubaya, Lady Jaydee, Solo Thang, Gangwe Mobb Jay Moe , Juma Nature, Afande Sele, Crazy GK, TID, Dully Sykes, AY, Mwana FA, Caz T, Soggy Doggy Anter, Mangwea, Mr Ebbo, Banana Zoro, Bwana Misosi, Daz Nundaz,Wagosi Wakaya, Mike T Mnyalu, Bizman, Feruz, Daz Baba, Stara Thomas, Ray C, Noorah, Mr Paul, Parklane, MB DOGGY, Mandojo na Domokaya, Mr Nice, Fid Q, Matonya, Mr Blue, Mh. Temba, Madee, Alikiba, Diamond, n.k

*Album za wasanii wa mwanzoni kama Sugu nilikuwa nazisikiliza kwa mabraza, nikitembelea kwa mabro unakutana na album kama 'Ndani ya Bongo', 'Nje ya Bongo', 'Deiwaka', n.k na kwa Mara ya kwanza nikavutiwa kuupenda huu muziki wa 'kufokafoka', nakumbuka kipindi hicho nilikuwa mtoto wa primary.

**MACHOZI JASHO NA DAMU' ya Profesa Jay, hii Album nakumbuka nilimpiga sound Maza hadi akaninunulia. Ni bonge moja la Album, moja kati ya album bora kupata kutokea kwenye bongofleva yenye nyimbo kama Ndiyo Mzee, Bongo Dar es salaam, Niamini, Jina Langu, Tathmini, n.k

***ULIMWENGU NDIO MAMA' ya Jay Moe, hii nakumbuka nilikuwa form1 Sengerema Sec (boarding), kwa Mara ya kwanza nilitoa hela yangu mfukoni (pocket money) na kuinunua. Kwangu mimi hii ni Album bora kabisa kupata kutokea kwenye Bongo Hiphop, hakuna wimbo wa kuforward mule, utakutana na ngoma kama 'Bishoo', 'Kama Unataka dem', 'Majukumu', 'Maisha ya Boarding', 'Mvua na Jua' na nyingine nyingi. Ukitaka kumjua JayMo huyu ndio alikuwa JayMo wa kweli alikuwa anaandika hasa, sio huyu wa sasa wa 'Pesa ya Madafu', 'Tunakula Bata', huyu wa sasa simuelewi kabisaa, ila ndio hivyo siwezi mlaumu sana maana ni lazima aswitch aendane na hiki kizazi cha 'Instagram'.

****A.K.A MIMI ya Mangwea, huwezi taja album 5 bora za wakati wote kwenye list yako ukaiacha hii album utakuwa na matatizo. Ni moja ya album niliyotoa hela yangu mfukoni na kuinunua, ina nyimbo kali sana kama 'Mikasi', 'Ghetto langu', 'A.K.A Mimi', 'Mademu wangu', n.k

*****CINDERELA' ya Alikiba, Nilikuwa sipendi kabisa hawa watu wanaitwa 'wabana pua', ila kwa mara ya kwanza nikavutiwa, nikanunua album ya huyu jamaa, na ndio ikawa mwisho wangu wa kununua album, ilikuwa moja ya album nzuri sana, ina nyimbo nyingi na zote zinasikilizika, nyimbo kama 'Cinderella','Nalia', 'Njiwa', 'Nakshinakshi', 'makmuga', na nyingine nyingi nilizipenda sana though sahivi mimi ni team Diamond . Album nyingine kali kwa hawa wasanii wa kuimba ni ya Banana Zoro 'MAMA', kama hujawahi kusikiliza itafute hutajuta ina madude makali mno though ilikuwa underrated, haikuwa maarufu kama SAUTI YA DHAHABU ya TID, sikuinunua ila kuna mshkaji wangu alikuwa nayo.

******.

NB: Sio kwamba album zote ambazo sijazinunua hazikuwa Kali, ni vile tu tatizo na kifedha lilinilazimu kuwa selective sana, ni Profesa Jay pakeyake ambaye nna album zake zote, wengine nilikuwa nachagua sana, na album nyingine nilikuwa nasikiliza kwa washkaji mfano album ya Ugali ya Nature ilisambaa sana kitaa, so sikuona haja ya kuinunua. Kiukweli nimemiss zama zile za album zilikuwa na raha yake. Sio sahivi wimbo mbovu, video kali, kiki kwa wingi. Kwa upande wako ni Album ipi umewahi kununua? Ni ipi album yako kali zaidi kwenye bongofleva?
 
Ooh! Hiyo Deiwaka nimekumbuka mbali sana sidhani atakama shule nilikua nimeanza ila mabraza wakubwa ulikua huwezi kuwakosa nayo hiyo album...

Kuna album ya Solo ilikia inaitwa Homa ya Dunia yayo ilikua nzuri japo huwa haiongelewi saaaana..
 
Homa ya dunia ni kali sana, ni moja ya album niliyokuwa natamani kuinunua ila kipindi inatoka sikuwa na hela. Ina pini kama Mambo ya pwani, Homa ya Dunia, Simu Yangu, Ndani ya Party ft Mack 2 B nk. Hawa vijana wa 'Wateule' walikuwa wananikosha sana
 
Album ya daz baba nakumbuka ilikuwa poa sana ilikuwa haina kupeleka mbele ngoma zote zilikuwa poa.
Yap, napenda sana ile ngoma inaitwa Elimu Dunia, huyu jamaa alikuwa mkali kushinda hata Feruzi sema Feruzi alipata bahati zaidi ya kutoboa baada ya kutoka na Starehe. Hata ukilinganisha Album ya Elimu Dunia vs Starehe ya Feruzi kwa upande wangu ya Daz Baba ilikuwa noma zaidi
 
Mkuu embu nipe list ya members wa kundi la Wateule maana hili kundi kuwa linanichanganya sana...
 
Hivi Sista P na Zay B waliwahi kutoa album? Au ndo walikuwa 'one/two hit wonder'?
 
Album ya daz baba nakumbuka ilikuwa poa sana ilikuwa haina kupeleka mbele ngoma zote zilikuwa poa.
Yap, napenda sana ile ngoma inaitwa Elimu Dunia, huyu jamaa alikuwa mkali kushinda hata Feruzi sema Feruzi alipata bahati zaidi ya kutoboa baada ya kutoka na Starehe. Hata ukilinganisha Album ya Elimu Dunia vs Starehe ya Feruzi kwa upande wangu ya Daz Baba ilikuwa noma zaidi
Elimu Dunia ni ngoma kali muda wote yani ukisikiliza lazima ikuhamishe hisia, ndani ya ngona kashirikishwa Afande alifanya vizuri sana alafu mwishoni unasikua sauti ya Feruz analalamika sana yani hatari
 
Mkuu embu nipe list ya members wa kundi la Wateule maana hili kundi kuwa linanichanganya sana...
SoloThang, JayMoe, Mchiz Mox, Jafarai, Mack 2 B(kama sikosei). Inasemekana hili kundi lilipatikana baada ya kushinda mashindano fulani ya rap na kuitwa WATEULE'. Ila sema naona JayMo na SoloThang waliamua kuwa Solo, huku Mchiz Mox na Jafarai wakitoka na ngoma ya Watu Kibao na kutumia jina la kundi Wateule'. Baadae Jafarai naye akatoka kama solo na ngoma ya 'Niko bize' ambayo ilibamba kinoma, na baadaye Mchizi Mox akaja na 'Mambo Vipi' ambayo nayo ilichafua hali ya hewa mtaani.Waliwahi kutoa ngoma ya pamoja siikumbuki jina
 
Basi ndii maana kundi linachanganya sana kutokana na kwamba wakitoa ngoma ya kundi mara nyingi hawatimii yani ngoma hii wapo flani na flani alafu ndoma nyingene unakuta wapo wengine tena... Ngoma kama msela sidhani kama Mox yupo
 
Hawajawahi kuwa na ushirikiano mzuri
 
Album ya rafiki by Mr. Nice,,,,,ilikua ni shida sio Bongo sio Kenya, ilikua ni mwendo wa kuku kapanda baiskel bata kavaa raizon!!!
Yap ilibamba ile mbaya though kwangu mimi ilikuwa takataka, sijui watu waliipendea nini
 
Hawajawahi kuwa na ushirikiano mzuri
Wateule walikua vizuri sana ila huwa nashangazwa na uwezo wa Jafarai mana huwa nikimsikiliza naona ana vitu vyepesi sana ukilinganisha na wenzake lakini wakitoa ngoma ya pamoja naona wanaenda sawa tu....
 
Jafarai alikuwa mzuri mwanzoni, isikilize vizuri Niko Bize alivyopangilia mashairi. Ila tangu alivyoanza kutoka na Shyrose sijui alipatwa na nini, aligeuka kuwa mwepesi mno kama ulivyosema, hadi Leo hii akitunga mashairi utaishia kucheka tu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom