Tukumbushane Nyimbo za Bongo Flava Zilizotamba enzi za 2000-2008

Mnataka kuzingumzia Bongo Flava mnawakumbuka KU "Kwanza Unit"..?!!!

hii thread ilikuwa 2007 watoto sikuhizi hebu some hapo chini

Mtanisamehe lakini najua wengi wenu humu JF mlikuwa Joni visomi na najua pia kuwa ambao hawakusoma mlikuwa mabaharia,na of course wengi wenu mnatokea mikoani na Dar mekuja miaka 1- iliyopita... lakini vile vile nilitaka kuwafahamisha kuwa early 80's kulikuwepo hili kundi la KU na sie wengine tulikuwepo siku ile ya jumamosi walipokuja CINE CLUB kurekodi video yao ya MSELA



ku1.jpg

176069136.img.jpg

176069062.img.jpg



Masela hawa wako wapi sasa...!!

Kwa wale tuliokuwa tukifwatilia kwa karibu muziki huu wa kizazi kipya wakati unaanza kuchipua,tutaungana mkono kuwa vijana walitokea mbali kiana na bila shaka katika harakati zao za kuukuza muziki huu walikutana vizingiti vingi na vya kila aina,mfano naweza kumtolea rafiki yangu Robert ambaye ilifikia wakati wazazi wake wakawa wanaingia na Radio zao chumbani ilimradi tu kumnyima bwana mdogo haki zake za msingi tena za kikatiba za kusikiliza muziki aliokuwa akiuf*gilia eti kwa maelezo kuwa muziki huo ni wa kihuni na usiokuwa na maadili hata kidogo.


Hapa kushoto ni KU Crew,katikati ni Terry kutoka HBC na kulia ni Mr II.Enzi hizooooo


Lakini kadri miaka ilivyokuwa ikizidi kusonga na wasanii kuendelea kuwa wabishi na kuachia mipini mipya tena kwa hela ya ngama waliyokuwa wakiidunduliza kwa taaabu kubwa, huku wakiwa hawapati maslahi yoyote ya maana zaidi ya ujiko tu...hatimaye wasanii walianza kuongezeka taratibuu jambo lililokuwa likiwachanganya zaidi wazazi wengi waliohisi vijana wamechanganyikwa.


Left ni Saigon na katikati ni Dola Soul kutoka the Diplomatz,kulia kwao ni Mr Paul...enzi hizoooooo


Yote hayo yalichangiwa na wengi tu kuanzia waandishi,vituo vya radio, mapromoter na kadhalika.....Jambo kubwa la kujiuliza wengi wa waanzilishi wa vita hiyo kubwa ya kuupigania muziki huu hawajulikani walipo.

Na leo hii itakuwa si vibaya hata kidogo tukiweza kuwakumbuka kwa pamoja wachache tu ambao mchango wao hata kama ni mdogo lakini umeweza kuifikisha Bongo Flava hapa tulipo na kuweza kuufanya muziki huu uwe kioo cha muziki wa vijana kwa Afrika Mashariki na Kati.


Hapa kushoto ni Caz T kutoka (BANTU POUND GANGSTER),katikati ni Bonny Harmony kutoka(AFRO REIGN),na kulia ni Rashid Ziada (KR) kutoka GWM ambaye pia ni mwasisi wa kundi la Wanaumeela TMK.


Kati ya tutakao wakumbuka wengine wanaendelea na muziki na wengine hatuko nao duniani kwa sasa, wengine hatujui walipo na wanafanya nini! tunajua wengi wangependa kujua wako wapi maselaaaa?



JE UNAWAKUMBUKA MASELA HAWA ?

Saleh Jabir
Adili a.k.a. Nigga One (R.I.P)
Afro Reign
K. U Crew
Bantu Pound
4 Kreuz Flava
Hard Blasters
Weusi Wagumu Asilia3
Sos B (ameongezwa na tony-serena znz)
Rhymson (KU Crew)
E-Attack
Fresh X
Kool Mooccc
Columba Mwingira - mawingu Band
OJ - Mawingu Band
Sindila
De-Plow-Matz
II Proud
G.W.M.


WATANGAZAJI WA RADIO (RADIO 1)
Master t
Mike mhagama


MAPROMOTER
Kim Magomelo (Kim & the Boyz)


STUDIOS
Container la Master J
Don bosco Studios
Sound Crafters


Je unazikumbuka video hizi za kwanza kwanzaaaaaa ?
1.Oyaa Msela oyaaaaa (Mawingu Band)
2.Usiige mambo ya mjini (Hard Blasters)
3.Kukurukakara zako (Sos B)



KUMBI
Kilimanjaro pool side
FM Club (zamani Lang'ata Social Hall)
Silent Inn club (umeongezwa na Frank Suura)

fuatilia hapa https://www.jamiiforums.com/entertainment/8100-hawa-wako-wapi-sasa-6.html#post114063
 
Kero no 1 underground hi nymbo mpaka leo nkisikia nakubal rap zaman bana,kuna machali kama Fredy jbu (rip) spark dog,father nely (rip) mac stif jcb wa enzi izo hu squad kbl hajalainka watengwa,lord eyez kbl ya unga Ak na mafaza wengne enz za metro mawngu dah arusha ilkuwaga kwel hip hop cty
 
Mnataka kuzingumzia Bongo Flava mnawakumbuka KU "Kwanza Unit"..?!!!

hii thread ilikuwa 2007 watoto sikuhizi hebu some hapo chini


fuatilia hapa https://www.jamiiforums.com/entertainment/8100-hawa-wako-wapi-sasa-6.html#post114063

mkuu vijana wa leo hawawezi elewa hii kwani enzi hizo hata wanaoitwa wakongwe wa game leo walikuwa hawapo...huyo mr 2 sugu alikuwa mbeya sijui iringa huko,nigger j a.k.a prof j hajulikani alikuwa wapi!!!!huwezi zungumzia wakali wa enzi hizo bila kuitaja fukwe ya coco beach na zile beach parties ambapo k.u crew ndo ilikuwa ngome yao!
 
Sijui ilikua nani, nakumbuka tu alikua chipukizi wa mwanza,
ila hio chorus alikua mdada ana sauti bomba ile mbaya...

alikuwa ni suma genius kijana wa mwanza! Leo nimeukumbuka sana ule wimbo wa Daz Nundaz-KAMANDA!
 
Kero no 1 underground hi nymbo mpaka leo nkisikia nakubal rap zaman bana,kuna machali kama Fredy jbu (rip) spark dog,father nely (rip) mac stif jcb wa enzi izo hu squad kbl hajalainka watengwa,lord eyez kbl ya unga Ak na mafaza wengne enz za metro mawngu dah arusha ilkuwaga kwel hip hop cty
Mkuu enzi zile kutoka ilikua kazi usipime!
 
mkuu vijana wa leo hawawezi elewa hii kwani enzi hizo hata wanaoitwa wakongwe wa game leo walikuwa hawapo...huyo mr 2 sugu alikuwa mbeya sijui iringa huko,nigger j a.k.a prof j hajulikani alikuwa wapi!!!!huwezi zungumzia wakali wa enzi hizo bila kuitaja fukwe ya coco beach na zile beach parties ambapo k.u crew ndo ilikuwa ngome yao!
Mkuu hivi kwanza unit kind Di-rob na GK si ndipo walipotokea? Washikaji walikuwa wanachana mbaya duh!
 
mi nilikua naupenda sana ule wa Sos B unaitwa Kukuru kakara zako zitakuponza....pamoja na ule wa Kwanza unit wa Mimi Msafiri......pia kuna ule wa x Plasters na machalii wa arusha unaitwa wachaga piga Chata....dah hapo nakuwa burdaaani.......pia kuna ule wa big dog posse unaitwa kumwambia...
Sos B kapotelea wapi huyu jamaaa? Kana kunamtu anafaham roots za huyu mtu atutupie humu plz!
 
.....Yo, yo ndani ya bongo mambo supa hapana uongo, ingawa sometimes bongo chungu kama sifongo,nafanya makaratee kama machinga mtaa wa kongo,na kimtindo mtindo nakata ngebe kimtima nyongo,hapana matata kitu roho inapenda mtapata,bongo dar es salaam ni mpeto wa kutakata,pitia pitia viwanja vya bongo ustaajabu,napita slip way, blue palm a mambo club,kama hujazoea unaweza ukavunja shingo,mambo isidingo, na watu mkononi nokia ringo,huwezi kujua yupi mtoto wa geti yupi changu,wote wanameremeta kama mamtoni mwanangu,rudi mwananyamala ooh mateja kibao,katiza saa moja moja uone roba za mbao,........!!!
Nigger Jay enzi hizo hana uproffesal teh! Teh! Alikuwa na Terry na willy. Dah! Hard Blasterz Crew was hot!
 
Nyumba ya urithi...''ndugu zangu wamenitenda ooh,kitendo kibaya wamenitendeaaaa,sikujua napokwenda mi,ila mungu bado ananipenda;''...hope mnaukumbuka...ni jamaa anaitwa 'kijiwe'
Mkuu huyo hakua TX-MOSHI KWELI?
 
kambuzi mememe kakolo mwamwamwa kabru kate chabo pwiyaa usiende resi masela tumetaitiwa!saa saba mchana mbuzi anakula jani!plasmod fella kompayalii.......manzewse crew sijui lugha gani walitumiakatika hii verse katika wimbo wao kula kona!!!!!.........................
Manzese crew na ule wimbo wao wa CHINGA teh! teh! Sina uhakika nawachanganya na TBT CREW!
 
Doctore mzee vp unazo tape za Sugu, nimezimis sana zile za kuanzia 1995 kipindi anaanza game!
Mkuu mi nasaka album yaka ile ya ndani ya bongo na maisha na muziki.. Dogo alizichukua akeibiwa shuleni!
 
Mkuu hivi kwanza unit kind Di-rob na GK si ndipo walipotokea? Washikaji walikuwa wanachana mbaya duh!

d ro a.k.a zomba ndo alipotekea ku crew na pale maeneo ya o bay ndo ilikuwa ngome yao mpaka IST na coco beach!GK kipindi hiko hakuwa anajulikana kimziki alikuwa ni rafiki wa marehemu D ROB anayeitwa BEIBII na JLT
 
mnaukumbuka ule wimbo wa dully skykes NYAMBIZI? ULIKAMATA MASIKIO YA WATU SANA.
wimbo wa kijinga sana kupata kutokea,sijui kwa nini umeukumbuka,hivi kweli mtu uliyelelewa kwenye maadili unaweza kutunga au kuimba wimbo kama huo?

 
dk, mi nmekuja tu kupata hitimisho,
dalili zinaonyesha kwamba mi nimetharika...........
ninao niiano, subiri vipimo;... ninao nniao;... usikate tamaa ................. huu nao ulitesa!!! ni nani vile?

na ule wa nikimnunulia soda hataki anataka togwa, viatu anaweka ndani ya friji, nafikiri ni wa Prof. J. kama sio maji marefu.
 
Mapenzi matamu - RC

Nakuambia aah siri yangu, inayohusu maisha yangu inayosumbua moyo wangu....... JD
 
Dar DSM sema Dar salaaam ya Sugu, Bongo Dar es slaam ya Prof Jay, Yo Mamsup waaa nipoze moyo mama nimechanganyikiwa penzi lako la maana...HBC, Mtoto wa Gate Kali ya Harouni
 
'angekuwepo duniani nisingewaza,rafiki yangu kipenzi niliempenda,

'hayuko tena duniani swahiba,niliempenda kwa wangu moyo swahiba' *2
 
'kipi kikusikitisha............sikitisha..........sikitisha
kipi kikusikitishacho..........ulichonacho we,shauri yako we!"

nadhani walikuwa Bantu Pound wale jamaa!

afu mheshimiwa mbunge wangu wa sasa akagonga;'nakumbuka nlivoanza na yo rap bonanza,enzi za zazuu,enzi zile we ni zuzu,enzi za tz.

toka tz A,B,C,D itafika mpaka Q wakati bado juu kama nna juju'..
.....dah,sugu weh!iko wapi ile hip hop ya ukweli,ya kina GWM,NWP dip-low-matz nk.!?
 

Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom