Tukumbushane Maisha Ya Vyuo Vikuu Tanzania Tulivyosoma, Boom Kuchelewa, Vibwanga Na Mikiki Ya Lecturers Nuksi, Wanafunzi Pasua kichwa

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
2,978
2,000
Habari wana Jamii,

Wengi tuliofanikiwa kupita vyuo vikuu tumepitia mengi sana, kama vile wenge la 1st year, kukosa au kuchelewa kwa mikopo (boom), kupanga hostel uswazi take away, mikiki ya malecturer pasua kichwa (anaamka asubuhi kagombana na mwandani wake anakuja kushusha hasira kwenye lecture na assignment au test), mbio za kijiti kukwepa supp/carry/incomplete, madeni kwa mama ntilie na kwa mangi, wazee wa tungi na kurudi hostel asubuhi, wambea na viherehere wa darasa, wazee wa hangover class, teamwork za exams, style za kucheat kwenye exams, lecturer kutongoza wanafunzi (kwa wadada ukigoma mualiko supp au carry inakuhusu), bash, kutereza na kujaza mabinti mimba (una gradu mtoto anatembea na kuongea), kuibiana notes na vitabu, kuchelewa vipindi, kuandikiana attendance na mengine mengi.

Ninaamini humu tupo raia wenye level tofauti kielimu, pia kuna walimu na malecture wa shule na vyuo wengi tu. Wengi wetu tuliofanikiwa kupitia/kusikia mikiki mikiki ya vyuo vikuu tanzania hebu tukutane na tukumbushane.

Hebu shusha "SINTOSAHAU" yako hapa.

Nafungua kikao,

tapatalk_1569613390958.jpeg
f6e3a53954fe4bed8a6e1b46cf6ea95d.jpeg
 

Machozi ya Simba

JF-Expert Member
Feb 23, 2012
3,219
2,000
Dah kuna jamaa alikuwaga kichwa ila ana sifa kishenzi, assignment ikitoka Leo hata kama inakusanywa baada ya wiki 2 yeye anamaliza usiku huo huo anakula kuturingishia kaimaliza, nikaona Huyu mwehu dawa yake ndogo sana, nikaingiza program ukichomeka tu flash mafaili yanajikopi kwenye pc, basi assignment ikitoka jamaa akiimaliza ile mida ya jini najilengesha na pc yangu ili aje kuchomeka flash, Huyu mwehu alifanya elimu yangu iwe mserereko 😂

Kuhusu privacy nakumbuka uvumilivu ulinishinda pale chuga watoto wazuri kila kona nkajivutia moja katikati ya semesta ya kwanza basi kwa vile nipo hostel nikajibana nikaenda kupangisha geto kule lemara relini karibia na idara ya maji nakumbuka nilinunuaga tu godoro, blanketi tu na vipazia,

Chuo kilimalizikaga ila hadi leo naonaga miujiza
 

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
2,978
2,000
Swala la kukopiana Assignment hua ni "IBADA MAALUM CHUO" mkuu.

Mimi nlikua nasoma na mama mtu mzima sana mmoja (age around 58), registration number yake ilikua inafatana na yangu, kwenye paper alikua anakaa jirani yangu, alikua ni bingwa wa kucopy na kuomba point kwenye paper mpaka malecturer walimzoea.

Alishakamatwa kama mara 20 ila anawapiga mistari ya kiutuuzima "acheni hizo watoto wangu, sisi wengine watu wazima, memory card kichwani zimeshajaa, tunalea watoto na wajukuu hapa tulipo, hatuna uwezo wa kushindana na hawa madogo wasiokua na majukumu kukumbuka vipengele vya masomo", basi wakawa wanamsamehe.

Too bad kuna mdada alijinyonga class sememster ya pili mwaka wa kwanza kisa mapenzi, alikua anatoka kijijini, akakutana na vijana wa dar wakamseti akazama mazima mazima, alijikuta amehonga hela ya ada yote na boom kwa msela. Semester ya pili jamaa akakamata demu mwingine. Ile viherehere wa kuingia class saa 12 asubuhu wanareport wakamkuta dada kaning'inia kwenye feni. Kaacha barua ndefu ya kilugha.
 

Next Man

JF-Expert Member
Feb 4, 2019
1,815
2,000
Chuo kimoj cha kifala Sana

Unakuta Semester Moja mtu ana Masomo 8,9 Mpk 12 Alaf usipofikisha CA Somo moja tuu Una rudia Mwaka dadeki

Tabu ya Nini nlikua naingia na Simu nagoogle Au vikaratasi (Vibomu) Sometimes Nlikua Sisomi kabisa ikifika mtihani naandika vikaratasi

Bora Mimi Sasa kulikua Kuna watu wanaingia na Tablet, Walikua wanachat na walioko nje wanatumiwa Majibu
Pepa inapigwa picha inatumwa Wasapu Wauni wanasolve fastaa Wanapiga pich nao Alaf wanarudisha Majibu Sio poa

Mtu akipata idea tuu Solution inaanzaje basi anamalizia

Kuna Mwanang alikua anafanyia watu Sup unamlipa alikua kipanga,Ni uhakika anakuchomolea yaani
 

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
2,978
2,000
Kuna siku tulipigwa msako mtakatifu wakushtukiza wa vibomu na nondo ndani ya paper. Vibomu tu vilikusanywa kama ndoo tatu mamaqe. Halafu malecturer wakatu shuffle siti za kukaa then wakaingia invigilators 6 kusimamia mtihani.

Siku hio kuna watu walipoteza fahamu. Maana matokeo yanatoka wanafunzi 150 kati ya 240 walitakiwa warisiti paper.
 

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
2,978
2,000
SitoSiSit


Mimi chuo nilizama kwenye penzi zito na mtoto mmoja mkali wa kichuga, lakini Daa Mungu si athumani nilitoka na first class. Tukipewa uwezo umepewa tu. Kama sio penzi ningeosha GPA ya 5. Kweli penzi kitovu cha uzembe.
Uliamua kutangaza UMASIKINI kwa mtoto wako wa chuga. Maana walikua wanapiga mizinga kishenz (sijui vocha, hela ya notes ku photocopy, mama anaumwa, hostel nadaiwa, weekend mzinga wa konyagi). Noma sana

Kuingia kwenye mahusiani chuo ni sawa na KUTANGAZA UMASIKINI.
 

bashite kaya

Senior Member
Jan 15, 2018
130
225
Uyo dem ndo alikomeshwa make wanatutesa sana
Swala la kukopiana Assignment hua ni "IBADA MAALUM CHUO" mkuu.

Mimi nlikua nasoma na mama mtu mzima sana mmoja (age around 58), registration number yake ilikua inafatana na yangu, kwenye paper alikua anakaa jirani yangu, alikua ni bingwa wa kucopy na kuomba point kwenye paper mpaka malecturer walimzoea...
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Single Phase

Senior Member
May 5, 2019
150
250
Dah kuna jamaa alikuwaga kichwa ila ana sifa kishenzi, assignment ikitoka Leo hata kama inakusanywa baada ya wiki 2 yeye anamaliza usiku huo huo anakula kuturingishia kaimaliza, nikaona Huyu mwehu dawa yake ndogo sana, nikaingiza program ukichomeka tu flash mafaili yanajikopi kwenye pc, basi assignment ikitoka jamaa akiimaliza ile mida ya jini najilengesha na pc yangu ili aje kuchomeka flash, Huyu mwehu alifanya elimu yangu iwe mserereko 😂...
Ulikuwa KCMC, MUCO, MWECAU au SMMUCo?
 

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
2,978
2,000
Wale wadada waliopata "DEGREE CHUPI" sijawaona wakichangia humu. Waliokua wanavua chupi na kukata mauno kwa malecture ili wapewe "PAPER" kabla ya mtihani au "KUCHOMOLEWA SUPP".

Ilikua ukisikia "PAPER IME LEAK" hata kama umelala hostel na hangover saa 8 usiku, utatoka tu. Kwanza lazima pombe iruke yote. Waliokoa "JAHAZI" mara kibao aisee, au lasivyo jahazi lingezama hasa mwaka wa mwisho (Mwaka wa bata).

Mbinguni watakua na "SPECIAL CORNER" maalum yao tu, yenye "FREE WI-FI" na "SOCKET YA CHARGER" ili wakeshe Insta na Facebook.
 

Philipo D. Ruzige

Verified Member
Sep 25, 2015
6,306
2,000
Kwanza ile kuingia UDOM mwaka 2010na kukabidhiwa T/UDOM/2010/05**** nikakumbana na kisanga cha maji.

Tukaandamana sana, gongwa sana virungu na FFU. Ugomvi ulizidi tulivyokua tunwaita f4 failures.

One time, waziri mkuu anapita anaenda college ya Health huku tumekiwasha balaa, akaja mkuu wa wilaya akadai yeye ni dhamana na mkuu atarudi kutusikiliza, bila kuchelewa wadau wakatoa gari la mkuu wa mkoa upepo kwenye tairi. Big up kwa Prof Osaki wa education, alikua anaheshimika akisema jambo raia wanaelewa.

Ila kuna wana waliliwa vichwa balaa. Kila kitu kina gharama yake aisee.
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
2,978
2,000
Kwanza ile kuingia UDOM mwaka 2010na kukabidhiwa T/UDOM/2010/05**** nikakumbana na kisanga cha maji.

Tukaandamana sana, gongwa sana virungu na FFU. Ugomvi ulizidi tulivyokua tunwaita f4 failures.

One time, waziri mkuu anapita anaenda college ya Health huku tumekiwasha balaa, akaja mkuu wa wilaya akadai yeye ni dhamana na mkuu atarudi kutusikiliza, bila kuchelewa wadau wakatoa gari la mkuu wa mkoa upepo kwenye tairi. Big up kwa Prof Osaki wa education, alikua anaheshimika akisema jambo raia wanaelewa.

Ila kuna wana waliliwa vichwa balaa. Kila kitu kina gharama yake aisee.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kusoma chuo kikuu bongo ni sawa na kupita JKT.

Tuliwahi kucheleweshewa boom miezi miwili, hali ilikua mbaya kweli, kama kawaida taarifa zikasambaa fasta UDSM, MZUMBE, St. JOSEPH, IFM, ARDHI, TUMAINI, KAMPALA kuitisha mgomo wa kuingia darasani J3 yake.

Sijui FFU walipata taarifa vipi, J3 tulikuta defender 3 nje ya vyuo vyote halafu jamaa ndani ya hizo defender wamenuna kinoma. Tukagoma hivo hivo kibishi kibishi. Tulichezea kichapo si cha kitoto, haikuchagua mtu mzima au kijana, mwanaume au mwanamke.
 

Philipo D. Ruzige

Verified Member
Sep 25, 2015
6,306
2,000
Kusoma chuo kikuu bongo ni sawa na kupita JKT.

Tuliwahi kucheleweshewa boom miezi miwili, hali ilikua mbaya kweli, kama kawaida taarifa zikasambaa fasta UDSM, MZUMBE, St. JOSEPH, IFM, ARDHI, TUMAINI, KAMPALA kuitisha mgomo wa kuingia darasani J3 yake.

Sijui FFU walipata taarifa vipi, J3 tulikuta defender 3 nje ya vyuo vyote halafu jamaa ndani ya hizo defender wamenuna kinoma. Tukagoma hivo hivo kibishi kibishi. Tulichezea kichapo si cha kitoto, haikuchagua mtu mzima au kijana, mwanaume au mwanamke.
ila kusema ukweli wale jamaa wanapiga aisee.. huku una wenge la moshi wa mabomu unakutana na mtama, virungu vingi ya magoti.

Wametutesa sana, yan katika siku tuliwahi kuandamana kwa amani ni moja tu kisa Boom tukamrukia DVC mjengoni , akatupangaaaa alafu tukaondoka kinyonge

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Top Bottom