Tukumbushane maisha ya UDSM enzi hizo, wazee wa Bibo na Main Campus

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Feb 26, 2018
2,490
3,534
Haabari wadau..!
Maisha ya UDSM enzi hizo yalikuwa powa sana sijajua kwa sasa.

Tuanzie wapi ,ngoja tuanze na Boom enzi hizo lilikuwa 4000/= kwa siku ila tulivyoingia chuo ikabidi tufanye mgomo Boom liongezwe watoto wa mama hawataelewa.

Maandamano yalianzia Revo Square sijuhi kama watoto wa leo wanaijua Revo Square watu wakatolewa lecture room wajoin movement watoto wa mama wakakimbia ila watoto wa mbwa tukaingia mtaani tulivyofika Mlimani City mabomu yalipigwa kama yote vile tukapoteana.

Kipindi hicho kuna wale wajamaa ndio wakuu wa vyuo wanajiita Tripple M yaani Mkandala,Mgaya na Maboko.

Mgomo ulipoisha chuo kizima tulirudishwa nyumbani kwa mda usiojulikana,baada ya kurudishwa tena sisi waanzilishi wa mgomo tukafukuzwa ila mm nikafanya harakati sikufukuzwa.

Mwaka wa kwanza nilipata room mabibo hostel pale maisha yalikuwa powa sana wale wa mwaka wa pili na kuendelea tukawa tunawabeba yaani kitanda chembamba mnalala wawili kana mpo lupango vile ,usiombe umbebe mtu mrefu.

Mwaka wa pili inabidi huwai chuo kabla akijafunguliwa ukatafute mtu wa kukubeba (kushare naye kitanda).

Ukiwa mwaka wa kwanza ni ngumu sana kupata demu wengi wanadharau mwaka wa kwanza,ila mwaka wa pili ndio mwaka wa kupata demu inabidi uliwahi konteana jipya (first year),asikwambie mtu hapa watoto wa mwaka wa kwanza wanamegeka kiurahini sana .

Boom likiingia safari za mlimani City ,Survey ,Ambiace n.k ila boom likikata tunaanza kupiga pasi ndefu kama hatuna akili nzuri hata lectures hazipandi kipindi hiki mademu wasio na msimamo wanaanza kujiuza ili wapate pesa za kujikimu,yaani kama una demu anaweza kukusaliti boom likikata.

Kipindi cha boom likikata wahuni tunaanza kugonga RB (Rice Beens) wali maharage ambao bei yake ilikuwa 600/=Boom likikata watu wanaanza kusifia wali mahatagr wa Cafe 1 na Coet ndio mtamu.Wazee wa bibo wanapiga tu shato pori mwendo wa kutembea kwa mguu toka main campus aibu washikaji wakikuona wanajua umefua.

Kuishi mabibo ni mateso hakukuwa na Kijazi Flyover foleni mtindo mmoja usishangae kutoka bibo mpk campus ukamaliza masaa zaidi ya matatu ubungo mataa.kukosa lecture au kuchelewa test kawaida kisa foleni ya ubungo mataa.
 
Niliwahi kwenda cafeteria ya hapa karibu na Rev square kulikuwa na bonge la foleni na ni kipindi boom limekata kwa wengi mimi sikuwa napata boom kwa hiyo nilikuwa napata kwa mzazi nilivyoona ile foleni nikasema leo nitachelewa kupiga menu nimekaa kidogo ghafla mhudumu kaja akafuta RB ha ha ha ebana eeh mstari wote ulipotea nikapata menu kwa urahisi
 
Namshukuru Mungu maisha yangu hayakuwa na msoto sana kwa sababu lifestyle ilikuwa ni ileile kuanzia mwanzo wa semester hadi mwisho. Cha tofauti nilichokuwa nafanya boom likitoka nilikuwa nanunua/nashona nguo mbili tatu. Uzuri wali maharage napenda sana kwa hiyo kilikuwa ndio chakula changu kikuu
 
Mambo ambayo sitayasahau pale Mabibo hostel2006-09:

1.Kipigo alichokipata Kibaka Mbele ya Block E.

2.Kifo cha mwanafunzi Bertha,aliyechomwa kisu na mpenzi wake.

3.Bata (ulevi) cafeteria,nasikia kwa sasa hakuna pombe.

4.Sisi wapenda soka tulikua hatukosi common room kuangalia mechi za ligi kuu Uingereza Jmos na Jpili.

5.Shida ya majikpindi fulani tukawa tunanunua nje ya geti kwa 1000 kwa dumu 1 la lita20.

Kiukweli maisha yalikua bomba sana!
 
Muhuni nimepiga udsm 3 years ila sikumbuki jina hata la lecturer mmoja zaidi ya huyu jamaa alikua anapigisha sociology yuko mtandaoni mahusiano motivation speaker... nilikua nakuja kupiga pepa tu chuo na kukusanya madesa

always unanikuta na begi kuubwa mgongoni limejaa ushenzi wa mtaani tu... wakusoma walikua wananiona muhuni tu sijakaa mabibo wala main campus...

daah i wish ningejichanganyaga na life ya chuo yani sikuwaga hata na dem wa chuo mi kitaa tu...

Any way niko kitaa life linasonga mazaga yanapatikana inshallaah tutaulrudi tena kusoma tupate hizo experience zilizotupita
 
18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom