Tukumbushane Maisha Ya Vyuo Vikuu Tanzania Tulivyosoma, Boom Kuchelewa, Vibwanga Na Mikiki Ya Lecturers Nuksi, Wanafunzi Pasua kichwa

Kusoma chuo kikuu bongo ni sawa na kupita JKT.

Tuliwahi kucheleweshewa boom miezi miwili, hali ilikua mbaya kweli, kama kawaida taarifa zikasambaa fasta UDSM, MZUMBE, St. JOSEPH, IFM, ARDHI, TUMAINI, KAMPALA kuitisha mgomo wa kuingia darasani J3 yake.

Sijui FFU walipata taarifa vipi, J3 tulikuta defender 3 nje ya vyuo vyote halafu jamaa ndani ya hizo defender wamenuna kinoma. Tukagoma hivo hivo kibishi kibishi. Tulichezea kichapo si cha kitoto, haikuchagua mtu mzima au kijana, mwanaume au mwanamke.
Ila kiujumla sadaka walizotoa wenzetu zimefanikisha mengi sana. Ikiwepo upatikanaji wa uhakika wa huduma na haki za wanafunzi.

Udom ilikuaga kawaida kukata mawiki bila maji. Unanunua uhai ya 6ltrs , sasa hapo utapambana kukata gogo, kuoga, kunawa uso, kunywa n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ila kusema ukweli wale jamaa wanapiga aisee.. huku una wenge la moshi wa mabomu unakutana na mtama, virungu vingi ya magoti.

Wametutesa sana, yan katika siku tuliwahi kuandamana kwa amani ni moja tu kisa Boom tukamrukia DVC mjengoni , akatupangaaaa alafu tukaondoka kinyonge

Sent using Jamii Forums mobile app
Kipigo cha mbwa mwizi, watu miezi 4 mnauguza majeraha ya virungu na mitama. Masikio mwaka mzima yameziba hayasikii kwa makofi ya FFU. Jamaa nuksi wale.

Ila kuna maandamano flani wanafunzi walimdaka FFU mmoja, alichezea kichapo kitakatifu sana.
 
We jamaa nyoko sana
Wale wadada waliopata "DEGREE CHUPI" sijawaona wakichangia humu. Waliokua wanavua chupi na kukata mauno kwa malecture ili wapewe "PAPER" kabla ya mtihani au "KUCHOMOLEWA SUPP".

Ilikua ukisikia "PAPER IME LEAK" hata kama umelala hostel na hangover saa 8 usiku, utatoka tu. Kwanza lazima pombe iruke yote. Waliokoa "JAHAZI" mara kibao aisee, au lasivyo jahazi lingezama hasa mwaka wa mwisho (Mwaka wa bata).

Mbinguni watakua na "SPECIAL CORNER" maalum yao tu, yenye "FREE WI-FI" na "SOCKET YA CHARGER" ili wakeshe Insta na Facebook.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hebu fafanua vizur maana si wengine hatujakatiza huko chuo wazee wa hangover class walikua wana elewa kweli maani lile wenge asubuh hua si la kitoto
 
Mkuu hebu fafanua vizur maana si wengine hatujakatiza huko chuo wazee wa hangover class walikua wana elewa kweli maani lile wenge asubuh hua si la kitoto
Hatari, unaingia kwenye lecture mpaka unatoka haujaelewa kitu, sox mguuni umevaa za rangi mbilo tofauti.
 
"Mwenye njaa ni mwenye hasira" ilitufanya tutoke lecture hall, tuandamane kwenda kwa mkuu wa mkoa tukale kwanza ili tuje kuongea na Principal, hii ni baada ya kucheleweshewa boom.
Third year, 2 second semister niliungana na Ngoswe kwenye kitovu cha uzembe ila Mungu alisimama na mimi nikatoka na Gpa ya 4 na point.
 
Big up mkuu kwa GPA nzuri. Tumepitia mengi sana.
"Mwenye njaa ni mwenye hasira" ilitufanya tutoke lecture all, tuandamane kwenda kwa mkuu wa mkoa tukale kwanza ili tuje kuongea na Principal, hii ni baada ya kucheleweshewa boom.
Third year, 2 second semister niliungana na Ngoswe kwenye kitovu cha uzembe ila Mungu alisimama na mimi nikatoka na Gpa ya 4 na point.
 
Sintosahau:- (1) Mwaka wa kwanza lecturer kutuambia tuko wengi sana kwahiyo watu lazima wapungue kuingia mwaka wa pili (2) Wakati wa supplementary na "vikosi" vya msaada kusubiri ku-solve paper chooni!!! Hivi vikosi vya msaada vilikuwa na ushirikiano sana!
 
Chuo kimoj cha kifala Sana

Unakuta Semester Moja mtu ana Masomo 8,9 Mpk 12 Alaf usipofikisha CA Somo moja tuu Una rudia Mwaka dadeki

Tabu ya Nini nlikua naingia na Simu nagoogle Au vikaratasi (Vibomu) Sometimes Nlikua Sisomi kabisa ikifika mtihani naandika vikaratasi

Bora Mimi Sasa kulikua Kuna watu wanaingia na Tablet, Walikua wanachat na walioko nje wanatumiwa Majibu
Pepa inapigwa picha inatumwa Wasapu Wauni wanasolve fastaa Wanapiga pich nao Alaf wanarudisha Majibu Sio poa

Mtu akipata idea tuu Solution inaanzaje basi anamalizia

Kuna Mwanang alikua anafanyia watu Sup unamlipa alikua kipanga,Ni uhakika anakuchomolea yaani
Hii DIT bla shaka
 
Kusoma chuo kikuu bongo ni sawa na kupita JKT.

Tuliwahi kucheleweshewa boom miezi miwili, hali ilikua mbaya kweli, kama kawaida taarifa zikasambaa fasta UDSM, MZUMBE, St. JOSEPH, IFM, ARDHI, TUMAINI, KAMPALA kuitisha mgomo wa kuingia darasani J3 yake.

Sijui FFU walipata taarifa vipi, J3 tulikuta defender 3 nje ya vyuo vyote halafu jamaa ndani ya hizo defender wamenuna kinoma. Tukagoma hivo hivo kibishi kibishi. Tulichezea kichapo si cha kitoto, haikuchagua mtu mzima au kijana, mwanaume au mwanamke.
khaaaaah kisa boom lol
 
Wale wadada waliopata "DEGREE CHUPI" sijawaona wakichangia humu. Waliokua wanavua chupi na kukata mauno kwa malecture ili wapewe "PAPER" kabla ya mtihani au "KUCHOMOLEWA SUPP".

Ilikua ukisikia "PAPER IME LEAK" hata kama umelala hostel na hangover saa 8 usiku, utatoka tu. Kwanza lazima pombe iruke yote. Waliokoa "JAHAZI" mara kibao aisee, au lasivyo jahazi lingezama hasa mwaka wa mwisho (Mwaka wa bata).

Mbinguni watakua na "SPECIAL CORNER" maalum yao tu, yenye "FREE WI-FI" na "SOCKET YA CHARGER" ili wakeshe Insta na Facebook.
yaan weee lol
 
Swala la kukopiana Assignment hua ni "IBADA MAALUM CHUO" mkuu.

Mimi nlikua nasoma na mama mtu mzima sana mmoja (age around 58), registration number yake ilikua inafatana na yangu, kwenye paper alikua anakaa jirani yangu, alikua ni bingwa wa kucopy na kuomba point kwenye paper mpaka malecturer walimzoea.

Alishakamatwa kama mara 20 ila anawapiga mistari ya kiutuuzima "acheni hizo watoto wangu, sisi wengine watu wazima, memory card kichwani zimeshajaa, tunalea watoto na wajukuu hapa tulipo, hatuna uwezo wa kushindana na hawa madogo wasiokua na majukumu kukumbuka vipengele vya masomo", basi wakawa wanamsamehe.

Too bad kuna mdada alijinyonga class sememster ya pili mwaka wa kwanza kisa mapenzi, alikua anatoka kijijini, akakutana na vijana wa dar wakamseti akazama mazima mazima, alijikuta amehonga hela ya ada yote na boom kwa msela. Semester ya pili jamaa akakamata demu mwingine. Ile viherehere wa kuingia class saa 12 asubuhu wanareport wakamkuta dada kaning'inia kwenye feni. Kaacha barua ndefu ya kilugha.
RIP. Kiama looooj
 
Kuna siku tulipigwa msako mtakatifu wakushtukiza wa vibomu na nondo ndani ya paper. Vibomu tu vilikusanywa kama ndoo tatu mamaqe. Halafu malecturer wakatu shuffle siti za kukaa then wakaingia invigilators 6 kusimamia mtihani.

Siku hio kuna watu walipoteza fahamu. Maana matokeo yanatoka wanafunzi 150 kati ya 240 walitakiwa warisiti paper.
Oshey mr 💰🤣🤣🤣🤣🤣

Daaa
 
Back
Top Bottom