MAISHA YA CHUO, MAISHA YA BOOM, MAISHA BAADA YA CHUO

thomas_360

JF-Expert Member
Oct 11, 2015
1,459
1,428
PART A: MAISHA YA CHUONI
habarini wadogo kwa wakubwa kutoka JF:
Napenda kutoa Yale ya moyoni niliyonayo ambayo kwa namna moja am a nyingine yanaweza kuwa fundisho kwa watakaguswa...
Maisha ya chuoni huwa yapo huru Sana, wale wahitimu au continuer watakuwa wananielewa zaidi...Chuoni ni sehemu ambayo hulazimishwi kuingia kwenye lectures, seminars, practicals session, kusoma, kula, kulala, Ila utambue kuwa kwa we unayeenda kuanza maisha ya chuo (FIRST YEAR), ila ukaekutambua kuna washambuliaji watatu matata wakifanikiwa kukushika utapata tabu Sana...hawa ni SUPPLIMENTARY, CARRY OVER NA DISCONTINUATION.
kila chuo inakuwa na system yake kwa hao jamaa watatu mfano kuna vyuo vingine SUPLIMENTARY hutokea pale ambapo unashindwa kupata pass mark kwenye mtihani wa mwisho wa kumaliza semester tunaita UNIVERSITY EXAMINATION (UE), huyu jamaa anayeitwa CARRY OVER yeye huwa anaurafiki wakati mwingine na jamaa mmoja anaitwa COURSE WORK, huyu jamaa anapatikana baada ya kufanya zile tests, assignments na presentations kabla ya kufanya UNIVERSITY EXAMINATION, so huwa kuna wastani wanaweka wa ufaulu ambao utakupa ticket ya kwenda kufanya UE mfano unatakiwa upate marks kuanzia 16 out of 40 marks za total course work so ikitokea umepata below 16 basi hapo hiyo course unakuwa umeibeba (UMEICARRY) so utairudia mwaka unaofuata, Ila hii system kuna vyuo ilikuwepo wakaja wakaiondoa, aina nyingine ni pale ambapo umefanya SUPPLIMENTARY ukashindwa kuchomoa/ kupass so Utalibeba na kulirudia mwaka unaofuata....DISCONTINUATION ( DISCO) huyu jamaa huwa anakuja kwa namna nyingi sana, kuna wakati anakuja automatic, kuna wakati mwingine anakuja kwa ww mwenyewe kumpenda so unatakiwa uwe makini sana!! Unaweza UKADISCO kwa kushindwa kuwa na nidhamu kwa malectures, kwa wanafunzi wenzio hapa namaanisha ugomvi au tabia zinazokiuka kanuni za chuo mfano kutumia simu kwenye chumba cha mtihani, au kutoa offending words ( maneno makali) kwa walimu na wanafunzi wenzako...lakini pia UNAWEZA KUDISCO kwa kuwa na GPA ndogo so kwenye GPA hapa vyuo huwa vinatofautiana viwango kuna wengine below 1.8 au 2.0 so ukipata chini ya halo ujue ni AUTOMATIC DISCONTINUATION. sasa disco ya aina nyingine hii inatokea pale unapofanya mitihani bahati mbaya ukapata supplimentary ukaenda ukafanya, ukaishindwa kupass, ukaibeba yaani ukaicarry hiyo course, mwaka unaofuata ukasoma upya ukafanya UE, ukashindwa kupass, ukaenda ukafanya supplimentary ukashindwa kupass hapo kinachofuata ni kwamba system itakutema direct so hapo napo unakuwa UMEDISCO.
NINI KIFANYIKE? unatakiwa ujitambue kuwa chuoni umefuata nini na usijadanganye na division one yako ya form six ukajua na chuoni utaendelea kuwa kipanga hapana ila jinsi utakavyojiweka ndo utaendelea kuwa kipanga maana elimu ya chuoni kwa wote mliongia chuoni haijalishi umeingia kwa divison 1,2,3 au 4 Ila maisha mnaanza upya so ukiamua kukazaa mwisho wa siku matunda yake utayaona...
SUPPLIMENTARY AU CARRY OVER wakati mwingine hutokea kwa bahati mbaya lakini usibweteke mpaka IKAKUPELEKEA KUDISCO.
Chuoni huzuiwi kuwa na mahusiano ya kimapenz au kutumia vilevi lakini kinachotakiwa ni kuzingatia ratiba za darasani na ratiba zako za kusoma ni ngumu sana kusema muda wote uwe unasoma usiwe na muda wa kujifariji au kula bata cha msingi
TIME TABLE IZINGATIWE.
PART B: MAISHA YA BOOM
MEALS AND ACCOMODATION ( A.K.A BOOM) ni pesa ya kujikimu ambayo huwa inasainiwa baada ya miezi miwili so kwa semester moja inasainiwa mara 2, hapa hupangiwi namna ya kuitumia lakini hakikisha kuwa unaitumia kwa ustarabu, na usiwakere watu wanakuzunguka tumia ukijua kuna Leo na kesho...Kuna watu ambao wanatoka katika familia za kawaida, hebu jaribu kujisomesha kwa boom lako at least wapunguzie majukumu wazazi wako, sometimes kuna ile kutojitambua hata mm wakati nipo mwaka wa kwanza nilikula boom langu vibaya Ila mwaka wa pili na watu nilikuwa najilipia Ada maana kila mwaka nilikuwa naongezea sh. 220000 kwenye tuition fees na gharama zingine mfano direct cost kwa kila mwaka, so kidogo wazaz walikuwa hawaumizi kichwa kuhusu mm,

PART C: MAISHA BAADA YA CHUO
wewe unayeenda kuanza chuo ujue kuna maisha baada ya chuo, ukiwa chuoni unauhakika wakupata hela baada ya miezi miwili kwa wale wenye BOOM lakini hata kwa wale wasio na BOOM najua kuna namna mnapata pesa ya kujikimu so ni swali la kujiuliza baada ya kumaliza chuo utajiendeleza vipi, wengi wanasoma huku wakiwaza sana kuajiriwa mapema lakini nikuambia hakuna ajira ambayo ipo direct wazi inakusubiria ww swala la ajira ni bahati nasibu na hii asikudanye mtu kila ngazi now watu wapo mtaani wanasota au wanafanya kazi sehemu tofauti na carrie zao..kuna wale ambao wanasoma huku wakiwa wanajua kuwa kuna ndugu sehemu ataniunganishia lakini kwa ww mwenzangu usiyekuwa na chanel umejipanga vipi? So tule bata sana chuoni lakini uchangunue ubongo wako baada ya kuhitimu utapambana vipi na maisha? Kuna wale ambao wanawaza kulipwa mishahara mikubwa lakini my dear mtaani kugumu ukipata ujira wa laki 3 usikatae huo ujira wa milioni moja utasubiria sana..piga kazi yoyote cha msingi usiombe pesa ya matumizi nyumbani....
kama utaweza save pesa na anza kuumiza kichwa ufanye nini baada ya maisha ya chuo wengine huwa wanafanya biashara zao akiwa bado anasoma hiyo mayo ni nzuri...

MWISHO NAJUA HAPA NITAWAUZI WATU LAKINI PENYE UKWELI LAZIMA TUWE WAZI...WEWE MWAKA WA 1 BIASHARA ZA KIMTANDAO NAJUA UNAWEZA UKAWA UMEZISIKIA NI VYEMA USIJIHUSISHE NAZO TAFUTA BIASHARA AMBAYO NI YA KUDUMU NA ITAKAYOKUWEZESHA KUPATA PESA AMBAYO UMEIHANGAIKIA. MIMI NIMESHAWAHI KUZIPITIA NA SIJAPATA FAIDA ZAIDI YA KUWAFAIDISHA WATU..BORA UBETI KULIKO KUFANYA HIZI BIASHARA
 
Ntaenda kusoma tena magu akitoka madarakni ngoja niendelee kuwalea watoto wangu kwanza
 
Weka kabisa kwenye PDF maana tutaweza kuisave na kusoma taratibu taratibu, nimeshindwa kusomea hapa.
 
Kufanikiwa kwa mtu ni utayari wa kifikra na maamuzi yasiyo na mipaka kujielewa unahitaji nini. Nini unakitu cha ziada nini ukiendeleze
Kushughulisha akili uliyopewa..
Kuishi kulingana na mazingira yaliyopo..
Maisha baada ya chuo ni maisha halisi yanayopaswa utayari...
 
Back
Top Bottom