Tukumbushane maisha ya UDSM enzi hizo, wazee wa Bibo na Main Campus

Odong nae alikuwa na nyota mganda yule! Kipindi cha kunji kabla hatujatimuliwa ilikuwa usiku main campus mtu anapiga ile 'Odooooong' kutokea hall five, sauti zinajibu kutoka hall 2 , 'Odwaaaaaaaaa', hahahaaa, ilikuwa burudani sana. Wakaja kumpiga deportation ya saa 24 naskia, wakamrudisha kwao kwa Idd Amin, na sijui ana udugu nae, maana alikuwa copy right na Idd Amin 🤣🤣
 
Kwa hiyo nyie wote mmesoma Udsm enzi hizo?😂😂😂
Ndio mkuu, enzi hizo huyu waziri wa nini sijui, bwana Adolf Mkenda alikuwa anafundisha hapo chuo yeye na mke wake mzambia. Enzi za FASS Night, Five na Mass com, bcom yao ilikuwa inaitwa Managers night sijui, hahahaaa, wa miaka hii sijui hata kama wanaelewa 😁! Mana Fass ikaja kuitwa CASS night.....! UDSM mambo ni mengi muda ni mchache, na kama ndo kwanza umefika 'Daslam' ndo utachanganyikiwa kabisa tutakuokota 'auxiliary police ' huko 😆😆😆
 
Mmmh! Rose wa Sociology ?? Mwaka gani? Mbona kama nakujua?
Hiyo 2006 BA Sociology kulikua na mikwaju balaa Kuna moja bonge la shangazi lilikua linakunywa Sana mipombe ale bar ya DARUSO na Udasa baadae anahamia Meeda anakesha (alone). Kuna siku nililikuta limekua boss ofisi nyeti aisee usimdharau mtu na masomo yake ya UNGWINI. CoET kule mademu walikua wanahesabika na sura ngumu tupu. Mmoja Ni boss mkubwa Magereza. Siku hz mitoto hata haisomi inarukaruka Kama 🍿
 
Ndio mkuu, enzi hizo huyu waziri wa nini sijui, bwana Adolf Mkenda alikuwa anafundisha hapo chuo yeye na mke wake mzambia. Enzi za FASS Night, Five na Mass com, bcom yao ilikuwa inaitwa Managers night sijui, hahahaaa, wa miaka hii sijui hata kama wanaelewa 😁! Mana Fass ikaja kuitwa CASS night.....! UDSM mambo ni mengi muda ni mchache, na kama ndo kwanza umefika 'Daslam' ndo utachanganyikiwa kabisa tutakuokota 'auxiliary police ' huko 😆😆😆
MSAUD forever
 
Nakumbuka wakati huo bwana Odwang Odwar anagombea urais Daruso.Jamaa alikubalika mno ilifikia wakati msemo wa Odooong Odwar the black fire ulikuwa maarufu mno main campus Hadi mabibo hostel.

Imagine usiku wa manane mtu anaamka hall 1 floor ya 4 anashout Odooong mwingine hall 2 floor ya 7 anaitikia Odwar the black fire

Mpaka wakina mkandala wakatishika ikabidi wamfanyie figisu aondolewe kwenye kucontest urais
 
Siku
Kwa huu uandishi wako wa kuchanganya a na ha, u na hu ulisoma UDSM ya wapi, si mnasemaga nyie ni cream ya taifa au ndiyo unathibitisha nyie ndiyo jalalani pro max?!
Sikusoma UDSM ile yenu yakulemba mwandiko nilikula vitu vya Coet Civil Eng ya Dr Nyahoro namba mwanzo mwisho kama ulisoma kule kwa Kadege una haki ya kukosoa uandishi wangu,maana O level kiswahili nina D😂😂
 
Bush bwana, akaongoza mgomo wa boom, chuo wakamuangaliaaa, alipomaliza tu wakamchukua wakamuweka pale utawala ashughulikie mikopo, sasa nenda pale sijui jina lako hujaliona boom blah blah blah, anakujibu shit mpaka unataka kuzimia! Huwezi amini km ndo yeye aliyekuwa anateswa na mkopo mpaka kuwa kiongozi wa migomo!
Hahaha 😂😂😂
 
Halafu Hapo UD vyoo vichafu miaka yote ila vijana wanahitimu fresh tu. Aisee sisi tumezoeshwa shida.
**Nakumbuka Hall 5 unaenda msalani na gazeti la Mzalendo vinginevyo jiandae kutoka na nnya ya aliyekutangulia. Same to vyoo vya CoET hakuna pa afadhali. Aisee acheni tule Pombe tu tumesoma kwa kuunga-unga jamani
 
Bush bwana, akaongoza mgomo wa boom, chuo wakamuangaliaaa, alipomaliza tu wakamchukua wakamuweka pale utawala ashughulikie mikopo, sasa nenda pale sijui jina lako hujaliona boom blah blah blah, anakujibu shit mpaka unataka kuzimia! Huwezi amini km ndo yeye aliyekuwa anateswa na mkopo mpaka kuwa kiongozi wa migomo!
Bush kawa Kama kondoo siku hizi. Anapelekeshwa Hadi na mkewe. Niliwaona Mlimani city mke anamgombeza njia nzima. Kuna kipindi aliendaga UDOM akaleta ukanda maalum enzi za jiwe (wakamtimua) siku hz nadhani karudi UD
 
Back
Top Bottom