Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

Hivi kweli biashara ya sinema hapo Dar bado iko active tena? Nadhani eneo lote la Drive Inn lilichukuliwa na ubalozi wa marekani, na Empress waligeukia biashara ya kubadilisha hela za kigeni (Bureau De Change). Thieta hizo nyingine nadhani zilijifia kifo cha mende tangu ukodishaji wa kanda za video uanze. Nadhani biashara hiyo itaweza kufufuka tena iwapo tu zitajengwa thieta za kisasa zaidi na kufungua mtandao mzuri wa kupata sinema mpya mpya kabla hazijawekwa kwenye DVD.
mambo yamebadilika sana mkuu
 
1. Unajua Tanzania, pamoja na siasa zetu enzi zile, lakini bado tulikuwa na nafasi ya ku-socialize hasa kwenye ma-Disco na muziki wa Dance, kwenye hili ni lazima tuwe fair kuwa Mwalimu hakuwa na tatizo kabisaa.

2. Ni kweli kwamba ex- DJ Gerard, au kama alivyokuwa akifahamika kwa jina la "Jerry Kotto", alitokea kuwa mmoja wa the best DJs mjini Dar, na ni kweli kwamba alikuwa na matatizo ya kusoma, lakini Jerry alikuwa na tabia moja nayo ni akipata Album au Tape hukaa chini na kuisikiliza mwanzo mpaka mwisho, akisikia ngoma anayoamini kuwa ni safi basi husimamisha na kuweka alama kwanza kwenye Tape/Album na pia kwenye namba ya ile song, sasa akingia kupiga Disco huzikumbuka nyimbo zote zilipo na ni zipi, tena bila ya tatizo.

3. Kwa kadri ninavyokumbuka tumewahi kuwa na Ma-DJ waliokuwa waburudishaji na wakali, kwa sababu pamoja na kwamba wao yaani ma-DJ walikuwa sio wapigaji hasa wa zile nyimbo, lakini siku zote mchele ni ule ule, ila mapishi ndio hubadili matokeo, hata ma-DJ nao ilikuwa ni hivyo hivyo, kwa kweli ningeomba kuwakumbuka tena kwa nafasi zao, wale wote yaani ma-DJ waliowahi kutuburudisha mjini Dar kama ninavyowakumbuka na pia msaada unakubalika iwapo kuna niliowasahau au kuwaweka kwenye nafasi wasizofaa:-

1. DJ Justin Kusaga - Clouds (Morogoro).
2. DJ Kali Kali (Kalikawe) - YMCA/Mbowe.
3. DJ Ebbo Night Woo Jack! (Bob Rich Mazula) - Msasani Beach.
4. DJ Chris Phaby "The Lover" - Mbowe/Margott.
5. DJ Choggy Sly (Choggo Salum) & DJ JPP (John Peter Pantalakis) - Msasani Beach/Rungwe Beach
6. DJ Roma Pop Juice (RIP) - Mwanayamala.
7. DJ Jerry Kotto (Gerard) - Mbowe RSVP Club.
8. DJ Nigger Jay - YMCA.
9. DJ DC Washington (RIP) - Rungwe Beach.
10. DJ Lucas
11. DJ Tito Jackosn (Tito Kalumanga) - Rungwe Beach.
12. DJ John Bure
13. DJ Joe Kusaga (Joseph Kusaga) & DJ Stewart (Sterwart Chiduo) - Clouds.
14. DJ Kim (Kim) - Rungwe Beach.
15. DJ Kessy (Kessi) - Blue Sky Disco.
16. DJ Eddy - Magomeni.
17. DJ Super Deo (Deo) - YMCA/Margott.

4. Kwa upande wa muziki wa Dance, pia tilkuwa na bendi za wazawa na wageni, hasa kutoka Zaire na wao pia kulingana na nafasi zao kimuziki as I remmember, na time pia lakini pia msaaada unakubalika:-

1. End of The 60s:-

1. Orch. Morogoro Jazz - Mbaraka Mwinshehe (RIP).
2. Orch. Cuban Marimba - Salum Abdallah (RIP).
3. Orch. Nova Success - Baba Gaston (Nairobi).
4. Orch. Nuta Jazz - Muhidini Gurumo (Ilala - Msondo Ngoma).
5. Orch. Tabora Jazz - Wema Abdalalh/Shem Karenga (Tabora).
6. Orch. Western Jazz - Wema Abdallah (Sikukuu street Kariakoo, Dar).
7. Orch. Dar Jazz - Dar.
8. Orch. Unyanyembe Jazz - (Nyanyembe Tabora.)
9. Orch. Kilwa Jazz - Ahmed Kipande/Juma Mrisho (Kilwa).
10. Orch. Police Jazz - Dar.
11. Orch. Atomic Jazz - John Kijiko (Tanga).
12. Orch. Kilombero Jazz - (Kiwanda cha Sukari Kilombero).
13. Orch. Butiama Jazz - Ifakara.
14. Orch. Boma Liwanza - (Zaire/DSM).
15. Orch. Banangenge - Fataki Masumbuko Ya Dunia (Zaire/DSM).

2. In the 70s. to 80s:-

1. Orch. Super Volcano - Mbaraka Mwinshehe (Morogoro).
2. Orch. TK Lumpopo - Juma kilaza (Morogoro).
3. Orch. Afro 70 - Patric Balisidya (DSM).
4. Orch. Urafiki Jazz - Juma Mrisho (DSM).
5. Orch. Nuta Jazz - Muhidini Gurumo (DSM).
6. Orch. Marquiz du Zaire - Chinyama chiyanzi (Zaire/DSM).
7. Orch. Vijana Jazz - Andoro/Maneti (DSM).
8. Orch. Safari Trippers - Marijani Rajabu (DSM).
9. Orch. Mwenge Jazz - George Mpupua (JWTZ- DSM).
10. Orch. JKT Kimbunga - Mzee Zakaria (DSM).
11. Orch. Kimuli muli - Zahiri Zoro (JKT Mafinga/DSM)
12. Orch. Simba Wa Nyika - Wilson & George Peter (Arusha/Nairobi).
14. Orch. Dar International - Abel Baltazari/Marijani Rajabu (DSM).
15. Orch. Police Jazz - Moshi William (DSM).
16. Orch. BarKeys - George Mhando (DSM).
17. Orch. Sola TV - (Temeke - DSM).
18. Orch. Makassy - Mzee Makassy (Zaire/DSM)
19. Orch. Nkashama Nkoi - Ndala Kasheba (RIP) (Zaire/DSM).
20. Orch. Matimila - Remmy Ongalla (Songea/DSM).
21. Orch. Sunburst - Kassim Magati (DSM).
22. Orch. Tanzanite - Nembo (DSM).
23. Orch. Toma Toma - Thomas (DSM).
24. Orch. Mpakani Kyauri Voice - Mzee Khatibu Itei Tei (DSM).
25. Orch. Mlimani Park - Abel Baltazari/Gurumo (DSM).
26. Orch. Doble O - King Kiki (Zaire/DSM).
27. Orch Safari Sound - Mbombo wa Mbombo-Ka/King Kiki/Ndala Kasheba (Zaire/DSM).
28. Orch. Mk Group - Kossongo Mpinda/shem Karenga (DSM).

Huenda kuna niliowaacha, lakini ninaamini kuwa ma-DJ tulionao sasa na bendi za muziki, ni kuanzia in 90s hadi leo ni almost wale wale na bendi ni zile zile ingawa cha kusikitisha sana ni kwamba kama ni bendi zilizopo leo labda hazizidi nne, zingine zote zilikufa kifo cha mende, lakini ni vyema kukumbuka kuwa katika enzi zile za 70s, 80, na mwanzoni mwa 90s pamoja na msiha kuwa magumu kidogo siku zote tulikuwa na burudani kabambe ambazo some of us zilitusaidia sana kuendelea kuyakabili maisha, knowing kwamba kuna weeek end kwenda kula mangoma na kuku za kibongo bongo.

Heshima Mbele Wakuu.
Wapi DJ Hakim Magomelo Kim and The Boyz???
 
Nilikuwa nagoogle topic fulani, nikalaletewa thread hii. Nikaikumbuka kuwa nilichangia hapa zaidi ya miaka kumi iliyopita, na kwa bahati mbaya picha nyingi zimepotea. Nitatafuta picha ambazo nilitumia kwenye posts zangu ili niziupdate. Nawaomba wote waliochangia kipindi hicho kama wanaweza kiupata picha walizotumia wasaidie kuifanya thread iwe active tena; kuna posts zilikuwa zina make sense tu zikihusishwa na picha zake ambazo sasa hivi hazipo. Najua hiyo itakuwa ni project ya muda mrefu ila nawaomba wanachama husika wafanye kila wawezalo kuipa uhai tena thread hii.
 
i1358_mwalimu.jpg

_________________

Mwalimu (RIP)Baba Wa Taifa Hili, na Mkewe Mama Maria

Wakuu Wote Jamii Forums, Heshima mbele!

Katika hiki kipindi cha mapumziko nimeona sio vibaya tukijikumbusha historia yetu ya taifa katika picha, ninawaomba wakuu wote wenye picha interesting kisiasa kwa taifa letu, tuziweke hapa ili tujikumbushe na kuelemishana kidogo kuhusu taifa letu lilikotoka, unajua wananchi wasiojua walikotoka hawawezi kujua wanakokwenda.

Ahsante wakuu.
Field Marshall...
Nina picha za za kihistoria ambazo nami ningependa kuziweka hapa kama kumbukumbu ya Baba wa Taifa na wazalendo wenzake walipogania uhuru wa nchi yetu.

In Shaa Allah nitaziweka hapa naanza na na hii ya kwanza:

1569037931757.png
Kulia ni Bi. Tatu bint Mzee, Bi. Titi Mohamed na kulia ni Bi. Chiku bint Said Kisusa Julius Nyerere hawa akina mama ndiyo wanachama wa mwanzo kabisa katika TANU hapa wapo Uwanja wa Ndege Dar es Salaam wakimsindikiza Mwalimu Nyerere safari ya kwanza UNO Februari, 1955.
 
Field Marshall...
Nina picha za za kihistoria ambazo nami ningependa kuziweka hapa kama kumbukumbu ya Baba wa Taifa na wazalendo wenzake walipogania uhuru wa nchi yetu.

In Shaa Allah nitaziweka hapa naanza na na hii ya kwanza:

Kulia ni Bi. Tatu bint Mzee, Bi. Titi Mohamed na kulia ni Bi. Chiku bint Said Kisusa Julius Nyerere hawa akina mama ndiyo wanachama wa mwanzo kabisa katika TANU hapa wapo Uwanja wa Ndege Dar es Salaam wakimsindikiza Mwalimu Nyerere safari ya kwanza UNO Februari, 1955.
Field Marshall,
Naweka picha ya pili nikijaribu kufuata mtitiririko wa kuiunganisha picha ya kwanza na hii ya pili:

1569084476353.png

Kushoto ni Iddi Faiz Mafungo, Sheikh Mohamed Ramia, Julius Nyerere, Saadan Abdu Kandoro na Haruna Taratibu Dodoma Railway Station, 1955.

1569090866469.png

Kushoto ni Rashid Sisso, Robert Makanga, Zuberi Mtemvu, Iddi Faiz Mafungo, Julius Nyerere, John Rupia na Titi Mohamed safari ya kwanza ya Julius Nyerere UNO 1955

Huyu Iddi Faizi Mafungo alihudhuria mkutano kwa kwanza wa TANU Ukumbi wa Arnautoglo mwezi Agosti, 1955 na kadi yake ya TANU ni no. 25.

Pamoja na haya alikuwa Mweka Hazina wa kwanza wa TANU na pia Mweka Hazima wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na yeye ndiye alikuwa mkusanyaji wa fedha za safari za Mwalimu Nyerere UNO.

Mwaka wa 1954 wakati TANU inaasisiwa Iddi Tosiri na ndugu yake Iddi Faiz Mafongo walikuwa na umri wa miaka 40 na zaidi kidogo na tayari walikuwa katika siasa za TAA na Al Jamiatul Islamiyya.

Ndugu hawa wawili ni kati ya wanachama wa mwanzo kabisa kujiunga na TANU. Iddi Tosiri kadi yake ya TANU ni no. 24 na Iddi Faizi kadi yake ni no. 25.

Iddi Tosiri alikuwa akiishi Mtaa wa Livingstone na Amani mwendo wa kama dakika 10 hivi kufika ofisi ya TANU New Street. Ndugu hawa wawili walikuwa na kaka yao mkubwa Sheikh Mohamed Ramia wa Bagamoyo, Khalifa wa Tariqa Qadiriyya.

Katika kuipa nguvu TANU na kumtambulisha Nyerere kwa watu maarufu, Iddi Tosiri na Iddi Faizi walimchukua Julius Nyerere hadi Bagamoyo kwenda kumtambulisha kwa kaka yao Sheikh Mohamed Ramia.

Sheikh Mohamed Ramia alikujakuwa rafiki mkubwa sana wa Nyerere wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika. Nimebahatika kuonyeshwa na mtoto wa Iddi Tosiri, Maulid ‘’Chubby’’ Tosiri picha alizoacha marehemu baba yake Mzee Tosiri zikumuonyesha yeye mwenyewe na Nyerere wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Nami kwa hisani ya familia hii naziweka hapa kama kumbukumbu ya mashujaa wa uhuru wa Tanganyika picha hizi tatu zilizofuatana:


1569090513833.png

Iddi Tosiri

1569090600487.png

Wakwanza kushoto mbele ni Iddi Tosiri, watatu ni Julius Nyerere akifuatiwa na Kaluta Amri Abeid. Mstari wa mwisho wapili kulia ni Rashid Sisso. Picha hii ilipigwa miaka ya mwishoni 1950 New Street mbele ya ofisi ya TAPA (Tanganyika African Parents Association)

1569299045934.png

Mkutano wa kwanza wa TANU Ghandhi Hall Dar es Salaam 1955 katika mkutano huu ulihudhuria ujumbe wa watu wawili kutoka Southern Province - Salum Mpunga na Ali Mnjale. Hawa walikuja na ujumbe maalum wa kutaka Nyerere afike Lindi kueleza madhumuni ya TANU kwani serikali na Kanisa walikuwa wanawatisha watu kujiunga na chama.

1569299442175.png

Tawi la TANU la Magomeni Mapipa alilofungua Ali Msham nyumbani kwake Mtaa wa Jaribu 1954 Ali Msham ni wa pili kushoto waliosimama na watatu kushoto waliokaa ni Bi. Titi Mohamed na pembeni yake ni mwanae Halima.

1569299768506.png

Ali Msham kulia wa kwanza siku alipomwalika Rais wa TANU Julius Nyerere kwenye tawi la TANU nyumbani kwake kumkabidhi samani alizomtengenezea kwenye kiwanda chake kwa ajili ya ofisi yake New Street 1955.

1569300018574.png

Tawi la TANU Magomeni Mapipa lilikuwa na nguvu sana kulia ni Sheikh Suleiman Takadiri Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU kushoto ni John Rupia ambae amemziba Julius Nyerere na huyo aliyeshika tama ni Zuberi Mtemvu Katibu wa TANU.

 
Field Marshall,
Hivi nyerere alikufanya nini?
Field Marshall,
Picha hiyo hapo chini ni Abdulwahid Kleist Sykes na mkewe Bi. Mwamvua bint Mrisho maarufu kwa jina la Mama Daisy.

Hawa ndiyo walimpokea Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam mwaka wa 1952 na mwaka wa 1955 baada ya Mwalimu kujiuzulu kazi ya ualimu waliishinae kwenye nyumba yao Mtaa wa Stanley na Sikukuu.

Picha hii ilipigwa Government House kwenye Garden Party ya Mr. na Mrs. Edward Francis Twining miaka ya 1950s.

1570480395052.png
 
Asante nimekumbuka history katika moja ya vitabu nilivyosoma
Field Marshall,

Field Marshall,
Picha hiyo hapo chini ni Abdulwahid Kleist Sykes na mkewe Bi. Mwamvua bint Mrisho maarufu kwa jina la Mama Daisy.

Hawa ndiyo walimpokea Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam mwaka wa 1952 na mwaka wa 1955 baada ya Mwalimu kujiuzulu kazi ya ualimu waliishinae kwenye nyumba yao Mtaa wa Stanley na Sikukuu.

Picha hii ilipigwa Government House kwenye Garden Party ya Mr. na Mrs. Edward Francis Twining miaka ya 1950s.

1572280680743.png

Kulia Abdulwahid Kleist Sykes (1924 - 1968) Hamza Kibwana Mwapachu (1913 - 1962)
Wazalendo hao wawili hapo juu wana historia ya kusisimua ukiisikia kwani hawa wawili ndiyo waliomleta Julius Nyerere katika ulingo wa siasa za TAA Dar es Salaam. Ukijua historia za wazalendo hawa utakuwa umefungua mlango mpya katika historia ya Mwalimu Nyerere, TANU na historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.
 
Mtu anjikumbusha baada ya dhiki sio unajikumbusha wakati unaburuzwa kwenye dhiki angalau kumbukumbu zako ikiwa zitakusaidia kujinasua katika dhiki na kukupeleka katika maisha bora.matumaini ambayo yalijengwa katika harakati za hawa MaCCM ,...maisha bora kwa kila Mtanzania....ni miaka inakatika ,sasa wanatubabaisha kwa kutuletea makampuni ya simu ambayo yanakaribia kuweka simu bure kwa jinsi mirija yao inavyofanya kazi ,sifa za mashirika ya simu ya Tanzania hayapatikani duniani kokote kule isipokuwa hapa eti mnara umeanguka !
Shida zsko na matatizo yako usiysfanye kuwa ya nchi nzima,baki nayo mwenyewe,wewe unaonekana ni lofa mpka kichwani kwako.
 
nani kakwambia kama Nyerere hakulimbikiza mali ,kama unaijua sababu ya Mkapa kufungua genge la biashala ikulu ,usingesema hayo ?
Kifo cha Nyerere kinajulikana ni ni baada ya kufa Jamal ambae ndie aliekuwa anahifazi feza ya Nyerere kwa jina lake,ghafla Jamal alipofariki Nyerere akafunga safari hadi kwa mke wa Jamali na kuulizia ela yake ,mke wa Jamali akamjibu Bana haikuacha kitu kwa jina lako ,hapo ndipo ugonjwa ulipoanza kumtambalia Mwalim na kumuondoa duniani.
Shetani ktk ubora wako
 
Back
Top Bottom